Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Unajielewa kweli!??? Priority iko wapi!??? Hizo fedha kwa nini hazikamilishi miradi iliyosimama kwa muda mrefu!??? Mishahara na maboresho ya wafanyakazi!??? Miundombinu!??? Kwani sasa hivi the so-called wageni mbalimbali wa Kimataifa wanapokelewa gereji!??? So, JKN aliyefariki before hajapewa kasri yake hakuwahi kuwapokea hao wageni!??? Hivi huna umaskini wa kufikiri kweli wewe!???
 
Hao wageni anaowapata ni wake,
atumie tu portion ya marupurupu yake mengi tu kujijengea badala ya kututwisha sisi wananchi mzigo mzito.
Kumbuka hawa huwa hawatozwi hata kodi wakiwa madarakani kwa hiyo wana priviledge nyingi tu.
Mtu ana nyumba nyingi tu, halafu unamuongezea na nyingine ili iweje?
 
Wote ni Wanyonyaji tu. Hivi Magufuli hakujiuliza kwa nini we zake hawakujengeana mpaka yeye akaamua kuwajengea wote.... Tatizo lilikuwa wapi?

Kikwete anadai ni haki yake, mbona sasa yeye hakumjengea Mkapa na Mwinyi mpaka wakasubiri Magufuli awajengee...!!

Kwa maoni yangu binafsi, huu ni muendelezo wa kujirundikia mali na matumizi mbaya ya pesa za wananchiy
Nasikia Kuna sheria inaruhusu basi tuifute
 
Kumbe Kikwete naye ni FISI
1620592606899.jpeg
 
Unajielewa kweli!??? Priority iko wapi!??? Hizo fedha kwa nini hazikamilishi miradi iliyosimama kwa muda mrefu!??? Mishahara na maboresho ya wafanyakazi!??? Miundombinu!??? Kwani sasa hivi the so-called wageni mbalimbali wa Kimataifa wanapokelewa gereji!??? So, JKN aliyefariki before hajapewa kasri yake hakuwahi kuwapokea hao wageni!??? Hivi huna umaskini wa kufikiri kweli wewe!???
Hiyo nyumba hata isingejengwa.

Bado wewe na ukoo wako mngeendelea kubaki masikini.
 
Alikuwa anasubiri nchi ifikie uchumi wa kati, wakati ambapo maisha ya watanzania yatakuwa bora kama yalivyo sasa. Siku hizi kuna ma-flyover, madaraja yanakatisha bahari na maziwa, SGR, madege n.k.!
Huo uchafu ndio mwaita flyover?,madaraja haahaa poleni mdanganye makenge wenzenu ambao wamezinda ndani Tu hawajawahi toka nje
 
The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani, na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
wewe una tatizo kichwani hiyo nyumba si imejengwa na magufuli au unajichomoa akili, sisi watanzania sijui tunataka nini yaani kila kitu tunalalamika ni race ya ajabu sana kwa kweli..
 
Ndiyo maana mtutu wa bunduki unatumika kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Yule Mkurugenzi wa Ubungo anastahili hekalu maana alihakikisha anabana mpaka penalty kwa wapinzani katika uchaguzi wa 2020
 
Wanasiasa wa bongo wanaishi kama wako Ulaya wakati watu wao wanaishi kama wako Afrika. Hawa viongozi hawaakisi uhalisia wa wananchi wao

Zijengwe nyumba kama hizo kama 5 tuwe nazo. Ziwe mahususi kwa marais na pengine mawaziri wakuu wastaafu na wenzi wao mpaka watakapokufa. Tutakuwa tumeepusha gharama kubwa za kumjengea kila Rais.

Rais mstaafu aishi humo mpaka atakapo tangulia mbele ya haki ila asilazimishwe. Akiamua kukaa kwenye 'kajumba kake' isiwe nongwa. Akiamua kukaa nyumba ya Rais mstaafu iwe sawa.

Ziwe nyumba bora kwelikweli. Na kwa wenye wake wengi ahesabiwe mmoja kati yao maana Rais anaweza kuwa na wake 4 halafu wa mwisho ana miaka 20 by the time Rais ana fariki. Sasa huyo kuachia nyumba hesabuni miaka 80 ijayo

Kuna wachangiaji wa huu uzi wanasema nchi hii si masikini kushindwa kumjengea Rais mstaafu nyumba. Hii si kweli. Ukitaka kujua umaskini wa nchi angalia jinsi inavyotoa huduma zake za msingi kama afya na elimu kwa watu wake. Bado huduma ni.mbovu na hicho ndo kielelezo cha umaskini wa nchi hii.

Hata kama wabunge nao tunawapa hela nyingi kila wakistaafu ndo yaleyale tu ya kwamba vipaumbele vyetu ni vibovu ndo maana tunaelekeza nguvu nyingi kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya kazi waendao bungeni kuongea badala ya kuwekeza nguvu kubwa katika maarifa ya vijana wetu
 
Prime minister wa uingerezaYuko Chini ya uchunguzi Kwa kukarabati flat wanakolala mawaziri wakuu lililo no 11 downing Street Kwa kuwa alitumia michango bila kutangazia umma nchi Tajiri kabisa inayojiweza walau.nchi yenye ufukara wa kutupwa wanajengeana ma kasiri na kuopeana hadharani kabisa mbele ya mafukara na ufukara wao. Matusi haya ya watawala wa kiafrika unahisi tuyakomeshe Kwa kuwaadhibu hasa CCM inayotuketea hawa wachumia tumbo.
 
Back
Top Bottom