Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,382
2,000
images (10).jpeg

Barua ya wazi kwa Rais mstaafu Kikwete.

Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu

Nakuandikia barua hii mimi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonesha kukasirishwa, kutopendezewa na kitendo cha serikali yetu kukujengea Jumba kubwa utadhani Kasri la Wafalme na wewe bila haya au aibu unalipokea kwa bashasha bila kujali kuwa nchi hii bado ni masikini sana na bado ina uhitaji mkubwa sana wa kila senti kwenda kuondoa umasikini wa kutisha wa watu wetu.

Ninafahamu kuwa mlijitungia sheria kuwa mstaafu akistaafu basi apewe pakeji nono ikiwemo kujengewa nyumba, licha ya kwamba hukuwa rais wakati sheria hiyo inatungwa, lakini ulikuwemo serikalini wakati inatungwa, baadae ukawa rais na hukuirekebisha hiyo sheria!, Na wala hujawahi kusikika popote kuonyesha kutofurahishwa na Mzigo mzito wa sisi wananchi kuwagharamieni nyinyi wastaafu kupitia kodi zetu.

Ndugu Jakaya Rais mstaafu, hebu niambie, wewe kama mtu uliyefanya kazi kwenye chama na serikali toka mwaka 1975 hadi mwaka 2015 ina maana hadi ulipostaafu, yaani jumla ya miaka 40 hukujenga nyumba yoyote?, ina maana miaka yote hiyo ulikuwa unapanga? —ina maana uliacha kujenga nyumba ukitarajia kuwa one day utakuwa raisi ili ukistaafu ujengewe nyumba kwa kodi za wananchi?

Ndugu Jakaya, Je nyumba yako ya Msoga haikutoshi? Unataka tena hilo hekalu ulipeleke wapi? Unataka umuachie urithi Ridhiwani?, umuachie urithi Miraji?, Umuachie urithi Mama Salma kupitia jasho la wananchi?

Nakuandikia barua hii nikitambua kuwa ulikuwa kijana wa TANU wewe, na nyie vijana wa kipindi hicho mlikuwa mkituaminisha kuwa mmeiva kwenye Itikadi za kukataa "unyonyaji",Najiuliza, kama mliweza kuwaaminisha wananchi kuwa siyo wanyonyaji na wakawaamini mpaka kuwapa nyadhifa kubwa huko mbeleni, mbona basi mnageuka wanyonyaji katika kustaafu kwenu?—Ina maana mikogo yenu ile ya kipindi hicho ya kujifanya siyo wapenda kujitajiriisha kwa kutumia kivuli cha nyadhifa zenu ilikuwa feki?. Mnapata wapi usingizi wa kuenjoy mimali yote hii katikati ya lindi zito la umasikini wa watu wenu tena kwa kujitajirisha kupitia jasho lao?

Ndugu Jakaya, mimi sitaki kukueleza umasikini wa nchi hii kwa sababu unaujua, Umeujua ukiwa bado kijana na unaujua ukiwa mzee—Hebu tutazame sisi wananchi walalahoi machoni, ambao masilahi yetu tunaambiwa hatuwezi kupata kwanza kwa sababu uchumi wa nchi umeshuka, kisha tuambie ndugu Jakaya, hilo hekalu lako ulilojengewa na serikali uliyopambana sana kuiweka madarakani linatusaidiaje sisi wananchi kuondoa adha za ukosefu wa maji, Ukosefu wa madawa, ukosefu wa madawati, upungufu wa ajira kwa vijana wetu, masilahi ya wakulima na wafanyakazi?

Ndugu Jakaya, wewe unalipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani, hivyo ndivyo nyie wanene mlivyojipangia, Unashindwaje kwa mshahara kujijengea nyumba nyingine ukiihitaji mpaka serikali ikujengee Hekalu lote hilo kwa kodi za wananchi?

Najua unaweza kusingizia kuwa eti hivyo ndivyo sheria inavyotaka, lakini je kwani ungekataa kujengewa hilo hekalu ungelazimishwa?, Na kama ukilazimishwa kwani huwezi kulikataa?

Nakuandikia haya huku nikijua kuwa Rais Mkapa alijengewa Jumba lake, Mwinyi akajengewa Kasri lake na wewe leo umekabidhiwa Hekalu lako. Katika wote hao nimeamua nikuandikie wewe barua hii ya wazi kwa sababu Mzee Mkapa hatunaye, hawezi kujibu, Mzee Mwinyi ni mtu mzima sana, ni dhahiri anasukumiziwamo tu, Ila wewe bado una nguvu uko active na bila shaka unafuatilia kwa karibu sana yanayojiri nchi hii!

Kuna swali moja tu ningependa unijibu, JE TANU ILIWAFUNDISHA VIJANA WAKE MKIPATA MADARAKA AU KUSTAAFU MGEUKE WANYONYAJI?

Jakaya nakuomba kwa heshima na taadhima, wewe umeshiba, wenye njaa nchi hii ni wengi, wananchi wenye uhitaji wasioweza kumudu mahitaji yao ya msingi ni wengi, Hilo hekalu lako linaweza kujenga maelfu ya vyumba vya madarasa kusaidia watoto ambao wanafaulu darasa la saba lakini hawawezi kuendelea kutokana na upungufu wa madarasa nchini. Hilo hekalu lako ni zaidi ya Zahanati 50, Hilo hekalu lako ni zaidi ya madawati 5000.

Hebu niambie Jakaya mtu mwenye majumba, una familia yenye kipato kizuri, Unawezaje kukubali kuwa na Hekalu lote hilo kwa jasho la wananchi wenye uhitaji wa kila senti ya jasho lao?

Tafadhali rudisha hilo hekalu kwa wananchi liwasaidie, ukifanya hivyo utakuwa muungwana sana!
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,957
2,000
Mbona Mkapa na Mwinyi hawajarudisha na walipewa na Magufuli
Wote ni Wanyonyaji tu. Hivi Magufuli hakujiuliza kwa nini wenzake hawakujengeana mpaka yeye akaamua kuwajengea wote.... Tatizo lilikuwa wapi?

Kikwete anadai ni haki yake, mbona sasa yeye hakumjengea Mkapa na Mwinyi mpaka wakasubiri Magufuli awajengee...!!

Kwa maoni yangu binafsi, huu ni muendelezo wa kujirundikia mali na matumizi mbaya ya pesa za wananchi.
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,957
2,000
Sheria ilikuwepo lakini marais wote waliona Haya kuitekeleza,akaja Jiwe mwenye PhD ya unafiki akawajengea wote Kwa mpigo.Lawama ni Kwa Jiwe sio JK
Hata JK a atakuwa kuona haya... Hii ni kama vile dhuluma kwa walipa kodi... Ndiyo maana yeye hakufanya hivyo kwa watangulizi wake.

Kama kweli serikali inataka kuwatunza basi iwaweke kwenye nyumba za serikali mpaka Siku wao na Waja wao waondoke duniani. Yaani hizo nyumba ziwe ni mali ya serikali.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,246
2,000
Wanajimegea tu keki ya Taifa bila kujali umasikini wa wananchi wetu

The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,382
2,000
The problem tuu ni kwamba wanafanya mchana kweupe bila haya wala woga, they know hamwezi kufanya lolote. Mfano mechi ya jana. Ingekuwa JPM lazima papohapo angepiga simu laivu uwanjani, na mechi ingechezwa saa kumi na moja kama ilivyopangwa. Huu ni ushamba na ulemavu wa akili uliokithiri.
Yaani hawaoni aibu hata kidogo, wanakula mpaka wanavimbiwa na bado wakipewa wanapokea tu!
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,872
2,000
Hatuna umasikini huo WA kushindwa kuwajengea Ma Rais wastaafu..

Nyumba hiyo moja thamani yake si pesa za mbunge aliestaafu?Na wabunge wako wangapi?..

Kama tuko serious tuanze na kupunguza mishahara ya wabunge...na posho na kiinua mgongo...

Mtu akishakuwa Rais hata akistaafu anapata wageni mbalimbali wa wa kimataifa

Tuache kuwaza kimasikini kuwa nyumba ni sehemu Tu ya kulala...

Sioni tatizo kabisa Kwa wastaafu kupewa nyumba wala magari...

Hata makampuni huwa yanatoa bonuses Kwa ma CEO wao...hata kama mishahara ya watu wa chini midogo..

Urais ni ofisi hata ukisha staafu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom