#COVID19 Mzee Hashimu Rungwe aiunga mkono chanjo ya Covid-19. Agusia suala la tozo na katiba mpya

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amezungumzia mvutano uliojitokeza kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, akimtetea waziri huyo kuwa hahusiki na mapendekezo.

Rungwe aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya Kiti cha Rais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliopita, akitamba na ahadi yake ya ubwabwa shuleni, amesema waliopendekeza wananchi wachanjwe ni kamati iliyoundwa na Rais Samia Suluhu.

Akizungumza na Nipashe Kinondoni, Dar es Salaam jana Rungwe alisema wanaombebesha lawama Waziri Dorothy kuhusu suala la chanjo hawako sahihi kwa kuwa kamati iliyoundwa na Rais Samia ndiyo iliyoishauri serikali nini kifanyike kupambana na corona.

Alisema kuletwa kwa chanjo ya corona nchini ni moja ya mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo. "Baada ya serikali kujiridhisha juu ya usalama na ubora wa chanjo, sasa inatekeleza wajibu wake," alisema.

Rungwe alisema anaamini kuletwa kwa chanjo hiyo ni neema kwa taifa kwa kuwa nchi imepata mwangaza wa kukabiliana na ugonjwa huo na wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo.

"Mimi nimepata chanjo tayari, hata watu wangu wa karibu katika chama chetu wamepata chanjo. Dhumuni ni kuhakikisha tunapata kinga ya ugonjwa huu hatari, hivyo ninawaomba Watanzania wote wajitokeze katika vituo vya afya kuhakikisha wanapata chanjo.

"Hawa wanaoipotohsa jamii, mimi naweza kuwaita ni washamba na wana mawazo ya kizamani. Mataifa mengi sasa wanahimiza watu wao kupata chanjo. Sisi tumeipata kwa nini tusichanjwe?" Rungwe alihoji.

Alisema kama watu hao wanaona chanjo haifai basi serikali iwape eneo waanzishe viwanda vya kutengeneza chanjo zao ili wawaletee wananchi chanjo sahihi na si kuishia kuongea tu.

TOZO ZA MIAMALA
Akizungumzia tozo za miamala ya simu na utaratibu mpya wa kulipa Kodi ya Majengo kwa LUKU, Rungwe alisema serikali inawabebesha mzigo wananchi wenye maisha ya chini. Kwa kutambua hilo, aliishauri serikali kutafuta njia mbadala ya kuimarisha makusanyo yake bila kuumiza Watanzania.

Alisema zipo njia mbadala za kupandisha uchumi wa nchi kama kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali kama vile safari na kubana kodi kwa bidhaa zinazoingia nchini ili kukusanya mapato mengi zaidi.

KATIBA MPYA
Kuhusu hoja ya kudai Katiba Mpya inayotiliwa mkazo na baadhi ya vyama vya siasa nchini vikiwamo CUF, CHADEMA na ACT-Wazalendo, Rungwe alisema serikali iliyopo ifungue milango na kukaa mezani na vyama vya upinzani ili kujadili masuala yanayohusu suala hilo. Alisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, watahakikisha katiba hiyo inatungwa kwa manufa ya nchi kwa kujenga demokrasia safi na usawa katika nyanja za kisiasa.
 
Safi sana mzee wa ubwabwa. Hekima yako tumeiona. Hao wapinga chanjo wana ajenda zao za siri. Issue siyo chanjo,wana jambo lao.
 
👇👇👇

Rungwe ni very smart sana.
 
Back
Top Bottom