Mzee gani anaweza akasimama na kutoa mwongozo wa mwelekeo wa taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee gani anaweza akasimama na kutoa mwongozo wa mwelekeo wa taifa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumaku, Dec 23, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  (Mjadada umechokozwa kule mtandao wa kwanzajamii. Nimeunasa)
  22 December 2009 1 views No Comment
  Mdau said:
  Ni mchomeko tu, wadau hii imekaaje?
  Mzee gani anaweza akasimama na kutoa mwongozo wa mwelekeo wa taifa?
  MWANDISHI WETU
  Tangu mwaka 1990 Rais Ali Hassani Mwinyi alipoanza muhula wa pili wa kipindi chake cha uongozi wa awamu ya pili, suala la mwelekeo wa taifa na hatma ya uongozi lilikuwa ndiyo ajenda kuu ya kisiasa.
  Kwa bahati nzuri alikuwepo Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alikuwa na uwezo mkubwa kifikra na kiuongozi. Jambo kubwa ambalo lilikuwa linamnyima usingizi Mwalimu Nyerere ni usalama wa Tanzania kama taifa huru na hatma ya uongozi.
  Toka mwaka 1990 mpaka sasa miaka 19 imepita, matukio mengi yamepita. Wazee wetu wapo japo Mwalimu Nyerere aliishatutoka. Swali ambalo tukijiuliza tutashindwa kupata jibu rahisi, ni Mzee gani anaweza kusimama na kutoa mwelekeo wa taifa?
  Wazee wengi tulio nao hivi leo, kwao itikadi ya ukombozi siyo hoja, wamekubali dunia, ikiwa ni pamoja na Tanzania yetu iongozwe na mfumo wa ubepari. Na wakati huohuo wako tayari kukemea maovu katika jamii bila kutambua kwamba maovu hayatokei hivihivi bali yanazalishwa na mfumo fulani na kutambua mfumo unaoyazalisha ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
  Kuingia kwa utandawazi na kukumbatia siasa za kiliberali kuliondosha Tanzania hususani Chama Cha Mapinduzi katika njia ya itikadi ya ukombozi.
  Mwalimu Nyerere aliliona hilo lakini hakutetereka katika imani yake ya kupinga mfumo wa ubepari na kutetea mfumo wa Ujamaa.
  Alitumia Chama Cha Mapinduzi kuchangia hoja pale palipohitajika kufanyika maamuzi makubwa. Alitumia vyombo vya habari kutetea itikadi ya ukombozi na kutetea ulazima wa kuwepo mshikamano na umoja ndani ya Chama.
  Wakati hakuficha kile alicho nacho moyoni, alikuwa anaheshimu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na vikao vikuu vya taifa vya chama.
  Hakuwa mtu wa makundi, bali alikuwa mtu wa mashauriano. Leo hii kuna madai kwamba Rais Kikwete ameshindwa kuongoza serikali na nchi na hivyo asigombee tena. Wengine walianza na wanaendelea na mzee Yusuf Makamba.
  Wengine ni Kikwete tu ndiye anayeweza kuiokoa CCM. Na wengine akina Reginald Mengi na wapambanaji dhidi ya ufisadi wanataka mafisadi waondoke waiache CCM mikononi mwa watu safi .
  Kwa mtu ambaye amekaa kando anasikiliza sauti hizo zote, huyu anasema hili na yule anasema lile, atafikiri kwamba hawa wanao sema hovyo hovyo wameingiwa na ugonjwa uliowakumba wajenzi wa Mnara wa Babeli!
  Rais Jakaya Kikwete anamaliza kipindi cha kwanza akiwa na kila sababu ya kujivunia kufanya kazi aliyochaguliwa na kutimiza ahadi alizozitoa kwa wananchi sehemu mbalimbali za Tanzania .
  Hapana shaka kwamba leo hii Tanzania ni maabara ya utekelezaji wa miradi mbalimbali; midogo, ya kati na mikubwa kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi kule walikotoka ngazi ya vijijini, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na taifa.
  Ujenzi wa shule za kata umefanyika nchi nzima. Kuna michango ya watanzania wa makundi mbalimbali; wakiwemo raia wakazi, Halmashauri, ruzuku kutoka serikali kuu, wafadhili na michango ya watu mbalimbali wenye maslahi tofauti. Kama kuna kazi imefanyika kuna waliobuni mradi huo, waliopitisha uamuzi na waliosimamia zoezi zima. Na si katika sekta ya elimu tu! Ni katika sekta mbalimbali za jamii ambapo miradi ya maendeleo imetekelezwa.
  Na wazee wetu waliopo, wamekuwa wapi miaka yote hii mpaka Rais Kikwete akashindwa kuongoza hili taifa?
  Wale wanaosema Rais Kikwete ameshindwa kuongoza, ainisho lao la uongozi ni kukemea, kunyamazisha mijadala na kuwa na nongwa na kuwasikiliza wapiga porojo. Hebu jiulize, Joseph Butiku, Salim Ahmed Salim na Joseph Warioba, hiyo Taasisi yao ya Mwalimu Nyerere imefanya utafiti gani (wa kura za maoni ya wananchi kuhusu Kikwete kushindwa kuongoza) kama ikitokea watu wakaulizwa Taasisi ya Mwalimu Nyerere inafanya kazi gani, ni watu wachache wataelezea inafanya nini. Kwa upande mwingine likiulizwa swali, je, taasisi hiyo inaongozwaje? Watu wengi watashindwa kujua, nani anamchagua nani kwa kipindi gani?
  Wazee tulio nao sasa si ndio hao akina Butiku, Warioba na Salim. Wote hao walikuwa kundi moja la kutafuta Urais 2005. Hawajakubali kwamba walishindwa na hivyo kukaa chini na kuwaachia walioshinda waendelee. Butiku analeta uchambuzi gani kuhusu nafasi ya utu katika mfumo wa ubepari? Aliwasilisha mada akizungumzia utu, haki na katiba kama hivi ni vitu vinatokea popote bila kuwepo mazingira ya kijamii na katika mfumo fulani wa jamii.
  Sasa hivi Tanzania tunaendesha uchumi wetu kwa misingi ya mfumo wa ubepari. Mbona taasisi ya Nyerere haichambui mfumo huo na kuutangaza kwamba ndiyo unatufaa na badala yake wanapapasa kingo zake na kujidai kwamba wamefanya uchambuzi wa hali ya kisiasa na kiuchumi ya Tanzania .
  Warioba anatuambia kwamba maamuzi magumu lazima yafanywe. Kwa nini kuzungumzia kwenye nahau na kwa ndimi, badala ya kutamka wazi (yeye kama Mwanasheria na kiongozi mstaafu) kwamba njia iliyo wazi kwa Rais, DPP au Mwanasheria Mkuu ni kumkamata Edward Lowassa, Rostam Azizi na Nazir Karamagi na kuwaweka kizuizini, ieleweke!
  Angalizo! Kama ikitokea hivyo Warioba atakwepaje kuwekwa kizuizini kuhusiana na Mwananchi Holdings? Philemon Sarungi na Wakuu wa majeshi waliopita watakwepaje katika Sakata la Meremeta na makampuni mengine ya kuchimba dhahabu? Waliokuwa wanatoa zabuni za kuingiza silaha na vifaa vya kijeshi watakwepaje? Waliobinafsisha mabenki, TBL na makampuni mengine ya umma watakwepaje kwenda kizuizini?
  Udhaifu wa hoja ya Warioba ya kutaka Rais Kikwete afanye maamuzi mazito ni kwamba anataka afanye maamuzi mazito dhidi ya kundi lile ambalo Warioba analiona kama mahasimu wao kisiasa siyo kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba kila kiongozi ambaye anaishi bado kama amehujumu uchumi wa nchi hii, basi apelekwe mbele ya sheria! Tunampa changamoto Warioba atoe wazo la namna hilo ambapo iundwe Tume ya kuchunguza viongozi wa Tanzania na wafanyabiashara wakubwa walipataje mali zao.
  Itakuwa kazi kubwa na kufanya pendekezo la warioba kuwa kiama!
  Na kwa upande wa Salim Ahmed Salim, anasema kwamba watu wanaotaka kugombea Urais 2010 wajitokeze na kwamba Tanzania imekithiri kwa rushwa.
  Je, kuna mtu amekatazwa kujitokeza kugombea ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi? Na, je kugombea urais ndiyo ajenda kuu ya kuondoa umaskini na kumaliza matatizo ya watanzania? Kwa upande mwingine, rushwa anayozungumza Salim, ni katika sekta zipi? Watu wengi wakiwemo wanazuoni na viongozi wanazungumzia rushwa katika sekta ya umma na sekta ya siasa, bila kuzungumzia rushwa na ufisadi katika ujumla wake.
  Kwa upande mwingine, kuna rushwa katika sekta binafsi na pia uhusiano wa viongozi na maswahiba wao nje ya mfumo wa dola.
  Mbona Salim hazungumzii kwa kina tukamwelewa? Kikwete amezungumzia mambo makubwa mawili, kutenganisha siasa na biashara na pia kudhibiti matumizi ya fedha katika shughuli za vyama vya siasa na kampeni za uchaguzi. Kikwete ametambua tatizo na akachukua hatua, wakati “wazee” wa chama wanalalama!
  Source: TAIFA Tanzania , Desemba 18, 2009
   
Loading...