Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Hao Chadema sasa ndio wajifunze! Sio kila mtu anayawenza mapambano ya upinzani. Imagine! Leo palikuwa na rundo la polisi ndani na nje ya ukumbi, na pia palikuwa magari mawili ya polisi yanaranda randa hapo chini. Hakunaga mpinzani analindwa hivyo na polisi zama hizi.

CHADEMA waache kupokea makorokocho ya CCM! Especially yaliyofikia umri wa kustaafu. Wawajenge watu wao wenyewe tangu wakiwa vijana. Acheni kuokoteza majitu ya CCM yanayowazia matumbo yao, si kila mtu kaumbwa kupambana kutetea wengine! Haya ndio matokeo.
 
Mkuu labda hujanielewa , umesema "waruhusu "mgombea binafsi ndipo labda ww utagombea, ndipo nikakuuliza Nani aruhusu mgombea binafsi?

Hapo hata sijaonesha fikra zangu uzisemazo kuwa ninazo , labda umenishambulia tuu pasipo kujua msingi wa swali langu ulitoka wapi..
Tayari una negative thought. Kwamba mgombea binafsi haitakaa iwepo.Tupambane katiba iruhusu wagombea binafsi.
 
Kuwepo nafasi ya mgombe huru hata mm nitagombea maana kwenye vyam wapo mnyungu watu 2015 ilikuwa chagua jpm na ccm tukamuamini tukampa anachapa kazi vzr watanzania hawana shida na vyama wanashida viongozi Bora waadilifu na wachapa kazi leo kuna watu ccm wanatamani magufuli aondoke madarakani waendelee kuchukua Kodi za majengo ya ccm
 
Mimi tatizo langu ni kule kunyimwa haki ya kugombea [kama katiba inaruhusu] na haki ya kuchaguliwa au kutochaguliwa. Nadhani tuzungumzie misingi halisi ya demokrasia ambayo Chadema inapenda kuonyesha kwa umma kuwa wanastahili kupewa dola.
Kwasasa CHADEMA wamejifunza makosa waloyafanya kwa Lowassa pia ni yeye ndio kwenye kelele .

KUBENEA
LOWASSA
SUMAYE
MGEJA
KISHOA

Narudia tutakuwa salama ndani ya chama.
 
Nilitaadhalishwa..sumu huwa haionjwi
The Mafiaso Inc
Tena uongozi wa Chadema Makao Makuu uliniomba mimi kutochukua fomu ya kuomba uongozi wa Kanda ya Pwani ili kumheshimu Mzee Sumaye , kilichobaki ilikuwa yeye kujinadi kwa wajumbe tu , zaidi ya ilichofanya Chadema isingewezekana kuwalazimisha wajumbe .
 
Kwasasa CHADEMA wamejifunza makosa waloyafanya kwa Lowassa pia ni yeye ndio kwenye kelele .
Tatizo langu ni ile dhana ya kuwa na haki ya kugombea. Tatizo hili hujitokeza kila mara inapokaribia uchaguzi wa chama na hasa nafasi ya mwenyekiti. Ni aibu sana kwa chama kinachojinasibisha na demokrasia na mmbadala wa CCM kuwa na hulka hizi.
 
Tatizo langu ni ile dhana ya kuwa na haki ya kugombea. Tatizo hili hujitokeza kila mara inapokaribia uchaguzi wa chama na hasa nafasi ya mwenyekiti. Ni aibu sana kwa chama kinachojinasibisha na demokrasia na mmbadala wa CCM kuwa na hulka hizi.
Narudia chadema wamejifunza makosa waloyafanya kwa Lowassa Nini shida mzee.
 
Sasa alikuwa hajui kama ndani ya Chadema hakuna demokrasia ? Kwani Lowassa aliwekwa vipi kuwa mgombea Urais Chadema ? Chadema hakuna demokrasia wala maendeleo.
We mwanamke natafuta sana kukuelewa ila sijawahi kukuelewa
 
Haya semeni tena wajinga na manyumbu mnaeburuzwa na Mbowe! Tukiwaambia mbowe anahusika na zile risasi za Lisu mtabisha, sasa mmeona? Mbowe ndiye mmliki wa chadema hakuna wakumtoa pale yyte anaetishia nafasi yake anamng'oa mapema mfno mzuri ni tukio la Lisu, Chacha wangwe na Zito ongezea na hili la Sumaye...nawahakikishia chadema inakufa kifo kibaya na muuaji wake ni Mbowe! Mwakani mkipata hata viti vitano vya ubunge utakuwa ni muujiza wa kugeuza maji kuwa diesel .
Kama kinakufa wewe shida yako nini.
 
SUMAYE TULIA USOME MCHEZO
CHADEMA ingeambia nini watu?
How come? Mtu atoke CCM na kujiunga Chadema mwaka 2015 halafu baada ya miaka minne tu atoshe kuwa Mwenyekiti wa Chadema iliyoanzishwa mwaka 1992?

Edward Lowasa alipotoka CCM alipewa nafasi ya ugombea Urais kimkakati, na kweli alipata kura nyingi kuliko wagombea wote wa Urais, dola ikamdhulumu. CHADEMA haikukosea kumpa Lowasa nafasi ya ugombea Urais lakini ingekosea sana kumpa nafasi ya uongozi mkubwa ndani ya Chama. Maana yake hata kama Lowasa angeingia ikulu bado chama kingekuwa mikononi mwa wanaChadema. Na huwezi kuwa Rais bila chama. Ni karata za siasa ambazo watoto wadogo hawawezi kuzicheza.
Hadi anaondoka Chadema, Lowasa alikuwa akitajwa kama mjumbe wa kamati kuu na mgombea Urais wa mwaka 2015, ndio maana kuondoka kwake hakujawa na madhara yoyote kwa Chadema.

Vipi kama Lowasa angesubiri kipindi cha uchaguzi agombee nafasi ya uongozi wa kitaifa wa Chama, angepata? Sidhani.

Itoshe kusema Mh. Sumaye aliaminiwa na wanachama kiasi cha kupewa nafasi ya uongozi wa kanda ya Pwani, lakini hakuaminiwa kiasi cha kupewa uwenyekiti wa Chama - Taifa. Na ndio maana wanachama wa Pwani wakaamua kumkataa mara tu alipotaka kujifanya anatosha zaidi ya uongozi wa kanda.
Demokrasia sio kuchaguliwa tu, ni pamoja na kukataliwa pia. Huwezi kusifu Demokrasia kwa sababu ya kuchaguliwa tu, isifu pia unapokataliwa.

CHADEMA ni chama kikubwa, chenye wanachama na wafuasi wengi, na pia maadui wengi wakiongozwa na CCM. Itakuwa kosa la kimkakati kwa Chadema yote kuwa chini ya mgeni kutoka CCM, hata dunia itashangaa sana.

Rai yangu kwa Mh. Sumaye, asifikiri amedhulumiwa wala asidhani Chadema hakuna Demokrasia. Demokrasia ipo ila imemkataa. Wanachadema wamejeruhiwa sana wakati huu na hawako tayari kuchezea nafasi ya uwenyekiti-Taifa, hiyo ndio nafasi pekee ambayo CCM wakiweza kuihujumu watavua nguo kwa shangwe. Inawezekana kabisa Sumaye akawa na nia njema, hilo anajua yeye, lakini kwa siasa za sasa Chadema haina nafasi ya kufanya majaribio kwenye uwenyekiti wa Taifa. Atulie, ausome mchezo.
 
Mabina ambaye alikuwa Katibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema hadi mapema leo amewasilisha barua ya kujiuzuru nafasi hiyo.
 
Back
Top Bottom