Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Mbowe anastahili pongezi kaweka mambo sawa kwamba upande wa pili unabebea mabango mambo ya ndani ya Chadema.
 
Mkubwa unahangaika bure tu kujaribu kuweka sawa uelewa na ufahamu wa jamaa wa chama cha kijani ambao wameamua kutoa tafsiri yao ya jambo rahisi linaloeleweka kama hili ili mradi tu kupaint picha waitakayo juu ya mtu huyu wanayemchukia kupita maelezo ya kawaida.....

Kwenye hotuba hiyo hiyo ametoa statement nyingine inayofanana na hii hii inayotafsiriwa na kila anayeamua kupotosha ili mradi tu kila asiye mpenda Bw Freeman Mbowe afurahishe nafsi yake kwa muda fulani....

Katika hotuba hiyo amesema pia hivi;

"......baada ya chaguzi hizi, CHADEMA inakwenda kuunda KIKOSI HATARI...."

Sasa sijui wasiompenda Freeman Mbowe, watatengeneza tafsiri gani tu ktk kauli hii kwa mara nyingine.....

Usishangae baadaye kwenye platforms mbalimbali za propaganda za jamaa wa nguo za kijani kukutana na vijihabari vya umbea na title za habari kama;

"MBOWE ASEMA ATAUNDA KIKOSI HATARI KUVURUGA AMANI YA NCHI"

au

"MBOWE AAHIDI KUUNDA KIKOSI HATARI CHA KURUSHA MABOMU"
 
THE SEAL,
Kwa mawazo haya mkuu inaonyesha kabisa ya kuwa tuna safari ya miaka zaidi ya 1000 kufikia kuwa na wananchi wengi wenye fikra huru ktk Tanzania yetu.

Japo inasikitisha, ila kwa kuwa ndio uhalisia bhac hatuna budi kukubaliana nao
 
Haya ndo wanajadiliana saivi,
Ndiyo mawaziri wakuu ambao hawana misimamo, mpaka hivi sasaa
Je lowasa ungeshinda urais ingekuwaje
FB_IMG_15754680778779794-01.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba hao wazee walipojiunga na Chadema walipitia wakati mgumu sana wa kunyang'anywa mali zao yakiwemo Mashamba walikuwa wanaenda kufilisiwa na CCM

Ndani ya roho zao wanaijua CCM ilivyowaonea kwa kuwazulumu sasa UvCCM wanachapisha hizi picha na kuulaumu Upinzani
 
Back
Top Bottom