Rejao
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 9,220
- 4,056
kuna Taarifa kuwa David Mosha aliyekuwa mkurugenzi wa Inter consult amefariki dunia kwa ajali leo mchana
Dkt. David Marshall Mosha , Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi za Wakurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya Inter-Consult pamoja Akiba Commercial Bank, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo kiasi cha saa Tano asubuhi katika mji wa Kibuku, kilometa kadhaa toka Korogwe, mkoani Tanga.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Inter-Consult Dkt. Startto P. Mosha kathibitisha habari hizo punde, na kusema kuwa mareheu alikuwa akisafiri yeye na dereva wake kutoka Dar es salaam kuelekea Moshi, kabla gari lake aina ya Toyota Double Cabin halijaacha njia na kupinduka kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.
Dkt Stratto Mosha amesema mipango ya mazishi itafanywa baada ya mwili wa marehemu ambao uko katika chumba cha maiti cha hospitali ya Wilaya ya Korogwe utapoletwa nyumbani kwake Mbezi Chini, karibu na mafleti ya BOT, na kwamba tayari timu imeshaondoka kwenda Korogwe.
Source:MICHUZI