Mzee Cleopa Msuya: Suala la Katiba Mpya haliepukiki kwani Katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu

N warioba pekee aliyekuwa anasimama hata enz za dikteta kuwa katiba n muhimu

Hao akina msuya wametokea wapi tena
Msuya anayumba sana kwenye kuliongelea hili swala la KATIBA. Kinachohitajika siyo marekebisho ya katiba, ni KATIBA MPYA.

Anauma huku anapuliza. Hatuhitaji katiba inayopendekezwa (ile inapendekezwa na CCM), tunahitaji Rasimu ya Warioba ndiyo inayotakiwa kujadiliwa.

Anaogopa kuukata mkono uliomlea, anayumba sana mzee. Atulie kwenye kuliongelea hili vinginevyo akae kimya.

Kuna maeneo anaongea kama vile hataki vyama vingi, halafu anakuja anarekebisha hoja yake kwamba vyama vinavyotakiwa visiwe vingi sana. Anatembea kwa kukanyaga kwa uangalifu sana ili asiwaudhi wana CCM wenzake. Akae kimya tu mzee wetu.
 
Unamaanisha Katiba yote haifai?!
Ana maana wakati wa kuunda KATIBA MPYA kuna vitu kutoka katiba ya zamani visivyofaa vitatupwa na vile vinavyofaa vitachukuliwa. Swala liwe kuunda KATIBA MPYA, hii habari ya marekebisho ya KATIBA limefanyika miaka nenda miaka rudi. Sasa ni KATIBA MPYA.
 
Kazungumza haya sababu hayupo kwenye mfumo wa kula,sahani zingekuwa zinamtembelea asingesema
 
Ana maana wakati wa kuunda KATIBA MPYA kuna vitu kutoka katiba ya zamani visivyofaa vitatupwa na vile vinavyofaa vitachukuliwa. Swala liwe kuunda KATIBA MPYA, hii habari ya marekebisho ya KATIBA limefanyika miaka nenda miaka rudi. Sasa ni KATIBA MPYA.
Katiba mpya ya kizazi cha sasa na sio kushona viraka
 
Wazee wote waliodhani Wana hati miliki ya nchi wao na watoto wao na familia zao wakiona watoto au familia zao hawako kwenye uongozi wa juu Wana kelele hasa kuanzia familia ya Nyerere ,akina warioba,akina akina Msuya ,akina Karume ,mzee kinana ,mzee Makamba nk

Mikelele yote hiyo kwenye awamu yeyote wanachobweka Ni kutaka familia zao wawemo juu serikalini

Watoto zao au wanafamilia wakipewa mivyeo wanaufyata

Nchi hii Hawa vikongwe nao sio wa kuwaamini Sana hiyo wanaita katiba mbovu waliinyamazia kimya wakila kuku kwa mrija wanataka vizazi vyao viendelee Mama Samia Mimi Kuna Mengi huwa nakukosoa lakini Hawa vikongwe wasikupelekeshe kutaka Koo zao zote zijae bungeni na serikali ni vyeo vya juu Ni unfair

Kikwete Mwanae Mbunge ,mkewe mbunge no huwezi kuona Kuna kelele kipindi Cha Magufuli

Hao wanalia Lia wanadhani Wana hati miliki ya utawala kwenye nchi

Mama Samia jiongeze.Wakipiga Mikelele si lazima ufanye watakavyo watakuyumbisha hao
Acha upuuzi.
 
ccm watapinga Katiba mpya kwasabu uwezekano wakukata watu mapanga wizi wa kura itakuwa ngumu
 
Ngoja waje UVCCM kumporomoshea mitusi mzee wa watu, kwamba Katiba mpya si ajenda ya CCM, kwa sasa ni ujenzi wa taifa kazi iendelee - sasa mzee anayetaka katiba mpya atoke CCM aende akajiunge na hao wapinga maendeleo mabarabarani.
Walishajaa akina Yehodaya
 
Ana maana wakati wa kuunda KATIBA MPYA kuna vitu kutoka katiba ya zamani visivyofaa vitatupwa na vile vinavyofaa vitachukuliwa. Swala liwe kuunda KATIBA MPYA, hii habari ya marekebisho ya KATIBA limefanyika miaka nenda miaka rudi. Sasa ni KATIBA MPYA.
Hayo ni marekebisho makubwa ya Katiba
 
Wazee wote waliodhani Wana hati miliki ya nchi wao na watoto wao na familia zao wakiona watoto au familia zao hawako kwenye uongozi wa juu Wana kelele hasa kuanzia familia ya Nyerere ,akina warioba,akina akina Msuya ,akina Karume ,mzee kinana ,mzee Makamba nk

Mikelele yote hiyo kwenye awamu yeyote wanachobweka Ni kutaka familia zao wawemo juu serikalini

Watoto zao au wanafamilia wakipewa mivyeo wanaufyata

Nchi hii Hawa vikongwe nao sio wa kuwaamini Sana hiyo wanaita katiba mbovu waliinyamazia kimya wakila kuku kwa mrija wanataka vizazi vyao viendelee Mama Samia Mimi Kuna Mengi huwa nakukosoa lakini Hawa vikongwe wasikupelekeshe kutaka Koo zao zote zijae bungeni na serikali ni vyeo vya juu Ni unfair

Kikwete Mwanae Mbunge ,mkewe mbunge no huwezi kuona Kuna kelele kipindi Cha Magufuli

Hao wanalia Lia wanadhani Wana hati miliki ya utawala kwenye nchi

Mama Samia jiongeze.Wakipiga Mikelele si lazima ufanye watakavyo watakuyumbisha hao
Hayo ni "mafikra" yako tu.Kila mmoja anawaza kadiri ya uoni wake.
 
Wazee wetu wastaafu asanteni sana kwa kujitokeza kuokoa nchi yetu, ni ninyi tu mliobakia, bado naamini Mzee Mwinyi pia yuko na sisi upande wetu .

Ona tunaibiwa kweupe kila mtu kimya, 30 million Dollars zetu zimekwenda hivi hivi na huu ndio mwanzo tu wa wizi.
 
Back
Top Bottom