Mzee Cleopa Msuya: Suala la Katiba Mpya haliepukiki kwani Katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,667
Waziri mkuu mstaafu mzee Msuya amesema suala la marekebisho ya Katiba haliepukiki kwa sababu katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu aliyeziumba mbingu na dunia.

-----
Alisema hayo katika mahojiano na Kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na runinga ya ITV kuhusu tathmini ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika mambo yaliyofanyika kipindi hicho na yaliyofanyika sasa.

"Katiba si kitu ambacho ni kama jiwe au kama amri ya Mungu, katiba ni kitu ambacho kitarekebishwa from time to time kulingana na mazingira yanayojitokeza," alisema.

Msuya alisema kwa msingi huo, marekebisho hayo ya katiba yatategemeana na makubaliano ya vyama au waliopo kwenye madaraka 'how to move' (namna ya kusonga mbele) na katiba iliyotengenezwa au watakuwa na mpangilio mwingine kwa kuondoa vile vitu wanavyoona havifai.

ASIFU HATUA YA JK
Alisema Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alikwenda vizuri katika suala hili la katiba kwa kuunda Tume ya Jaji Warioba ambayo ilizunguka nchi nzima wakatengeneza mapendekezo na likaundwa Bunge Maalum la Katiba ambalo lilipendekeza Katiba Pendekezwa ambapo ilibaki stage (hatua) moja tu ya kuipitishwa na wananchi kwa kura ya maoni.

VYAMA VYA SIASA
Akizungumzia kuhusu demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwa siasa, Msuya alisema inashangaza kuona Tanzania kuna utitiri wa vyama kati ya 19 hadi 22 vilivyosajiliwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

"Sasa unajiuliza Tanzania hii demokrasia tunaiyotafuta kwenye vyama 22 ni nini hasa, wakati bado tuna sehemu ambazo watu wana njaa, bado tuna sehemu ambazo wabunge wanaomba barabara zijengwe, hivi kweli seriously unasema tuna haja ya vyama vingi?" Alihoji.

Msuya alisema demokrasia anayoiona isiwe na utititri wa vyama vingi vya siasa bali kutafutwe njia ya kuwa na vyama vichache kama vitatu au vinne na isiwe kulazimisha bali wananchi waulizwe kwa kupiga kura na mwisho wa matokeo ya kura utakuta kuna vyama ambavyo hawavitaki.

"Kuna vyama katika hivi 22 kwenye uchaguzi havikupata hata kura 1,000, nchi nyingine wanachokifanya ni kuwa vile ambavyo havikufikia kiwango fulani wanavifuta na kubakia vile ambavyo kiasi fulani vinakubalika," alisema, ambaye alikuwa waziri mkuu katika uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere na Ali Hassan Mwinyi.

Msuya alisema kimsingi si vizuri kuwa na chama kimoja tu cha siasa, maana watu wakikaa na chama kimoja wanaweza wakajisahau, hivyo kunahitajika watu ambao wanapiga kelele wanapoona watawala au chama wanaficha madhambi yanayotendeka katika system (mfumo).

"Mimi nakubali mfumo wa vyama vingi uendelee kuwapo, lakini vyama visiwe vingi kiasi hicho, na sasa hivi mtu akishaitwa mwanasiasa anazungumza hata mambo ya uongo, lakini lile lengo la kusaidia serikali inayokuwapo madarakani halipo, wanataka tu wao waingie," alisema.

Aliongeza kuwa kule ambako tumefungua milango kwenye utitiri wa vyama na utitiri wa wanasiasa imekuwa ni shida, inahitaji kuwa na vyama vichache kwani si wengi wanaoelewa dhana ya kuwa na vyama vingi na wanaweza kuwa serikali mbadala kwa kuchunguza makosa ambayo yanafanywa na serikali iliyopo.

Msuya alisema mataifa kama Ujerumani, Korea Kusini, Japan, Malaysia na Singapore yameweza kupiga hatua haraka kimaendeleo kutokana na ushirikishaji wa wananchi katika maendeleo, lakini si kwa kuwa na utitiri wa vyama.

Aidha, alisema Tanzania ina uhuru sana wa watu kujieleza, lakini shida iliyopo ni baadhi ya watu wenye kutoa manung'uniko kuvuka mipaka na hata baadhi ya watumishi wa serikali wa vyombo vya dola kuna wakati wanazidisha udhibiti wa hali hiyo.

RUSHWA
Msuya akizungumzia kuhusu rushwa, alisema bado ipo sana na hii imetokana na mfumo wa sasa wa kupata viongozi wa njia ya kuchaguliwa kupigiwa kura.

"Suala la rushwa linachanganya sana, zamani kabla hatujaleta mambo ya viongozi wa kuchaguliwa tulikuwa na mfumo wa machifu ambao walikuwa wanatozana tozana wanakula katika maeneo yao," alisema.

Alisema baada ya kufuta mfumo huo na kuja na utaratibu wa kuchagua watu mpaka mwenyekiti wa kijiji na kitongoji anachaguliwa na anataka kila kipindi apigiwe kura, anajenga utaratibu wa kununua watu ili wamchague.

"Utitiri wa vyama nao umeongeza kuwepo kwa rushwa, kwani ili ugombee udiwani au ubunge unalazimika uzunguke huku na kule na wanatumia pesa kuhonga wapigakura maana wanajua nini watakwenda kukipata wakishachaguliwa," alisema.

Alisema ili kukomesha tatizo hilo kunahitajika kuwa na judiciary system (mfumo wa kimahakama) na investigations system (mfumo wa uchunguzi) ambayo itakuwa inafanya uchunguzi haraka na wahusika wanachukuliwa hatua. Aliyolea mfano kwa Singapore kuwa wanafanya hivyo na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha rushwa.

Chanzo: Nipashe
 
Wazee wetu wastaafu asanteni sana kwa kujitokeza kuokoa nchi yetu, ni ninyi tu mliobakia, bado naamini Mzee Mwinyi pia yuko na sisi upande wetu .

Ona tunaibiwa kweupe kila mtu kimya, 30 million Dollars zetu zimekwenda hivi hivi na huu ndio mwanzo tu wa wizi.
 
Wazee wetu wastaafu asanteni sana kwa kujitokeza kuokoa nchi yetu, ni ninyi tu mliobakia, bado naamini Mzee Mwinyi pia yuko na sisi upande wetu .

Ona tunaibiwa kweupe kila mtu kimya, 30 million Dollars zetu zimekwenda hivi hivi na huu ndio mwanzo tu wa wizi.
Mtanikumbuka!
 
Kweli mzee wetu, inatakiwa katiba mpya ya wananchi, yenye misingi, taratibu na miongozo ya nchi, itayokuwa na credibility na accountability kwa viongozi na wananchi kwa ujumla,

Haiwezekani kiongozi awe na power ya kuchagua judges, tume ya uchaguzi, baraza ya mawaziri, wakuu wa mikoa, wakurugenzi, wabunge wa viti maalum...khaaa!
 
Sio marekebisho Katiba iliyopo tayari ina viraka vyakutosha, kinachohitajika sasa ni Katiba Mpya ije kugawanya majukumu ya kila ofisi na mipaka yake, na atakaekiuka aijue adhabu yake.
Unamaanisha Katiba yote haifai?!
 
Kweli mzee wetu, inatakiwa katiba mpya ya wananchi, yenye misingi, taratibu na miongozo ya nchi, itayokuwa na credibility na accountability kwa viongozi na wananchi kwa ujumla,

Haiwezekani kiongozi awe na power ya kuchagua judges, tume ya uchaguzi, baraza ya mawaziri, wakuu wa mikoa, wakurugenzi, wabunge wa viti maalum...khaaa!
Kwa udini wa watanzania,rais sharti awe na nguvu,maana dini Fulani wakiwa wengi bungeni,Basi rais atayumbishwa sana
 
Waziri mkuu mstaafu mzee Msuya amesema suala la marekebisho ya Katiba haliepukiki kwa sababu katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu aliyeziumba mbingu na dunia.

Source: Nipashe
Now wanaongea sababu hawana chakupoteza ...tunataka kumsikia Mkwere nae
 
Waziri mkuu mstaafu mzee Msuya amesema suala la marekebisho ya Katiba haliepukiki kwa sababu katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu aliyeziumba mbingu na dunia.

Source: Nipashe

..wakati Magufuli yuko madarakani asingeweza kutamka hivyo.

..nakumbuka Mzee Msuya aliunga mkono amri ya kuzuia mikutano ya hadhara akidai Rais ni sawa na Baba kwenye nyumba hatakiwi kupingwa.
 
Waziri mkuu mstaafu mzee Msuya amesema suala la marekebisho ya Katiba haliepukiki kwa sababu katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu aliyeziumba mbingu na dunia.

Source: Nipashe


Nathubutu kusema hawa viongozi wastaafu wote wanaojitokeza leo kuzungumzia kuhusu katiba mpya ni wanafiki, kwani kipindi walipokuwa viongozi (kwenye ulaji) hawakuona kwamba katiba hii inayomapungufu??!---- mbona walikaa kimya?!, walikuwa wanalinda matumbo yao!!--- iweje sasa ndio wanajitokeza??, hata hao akina Mama Samia na Majaliwa wakitoka tu madarakani na kuingia uraiani utawasikia wakiimba nyimbo hiyo hiyo ya katiba mpya.

Tena unafiki wa mithili hiyo ulianzia kwa Baba wa taifa, kipindi alipokuwa madarakani kamwe hakuzungumzia juu ya kuanzishwa kwa vyama vya upinzani lakini mara alipong'atuka (alipojiuzulu) madaraka na kumuachia Mwinyi na hapo hapo akaanza harakati za kuanzishwa kwa vyama vya upinzani nchini, huo ni unafiki.

Ni bora hao viongozi kwanza wakiri na kutubu makosa yao mbele ya Mungu na Watz na ndipo watetee katiba mpya ama sivyo wakae kimya kwani hawana "Moral authority" ya kutetea katiba mpya.
 
Wazee wote waliodhani Wana hati miliki ya nchi wao na watoto wao na familia zao wakiona watoto au familia zao hawako kwenye uongozi wa juu Wana kelele hasa kuanzia familia ya Nyerere ,akina warioba,akina akina Msuya ,akina Karume ,mzee kinana ,mzee Makamba nk

Mikelele yote hiyo kwenye awamu yeyote wanachobweka Ni kutaka familia zao wawemo juu serikalini

Watoto zao au wanafamilia wakipewa mivyeo wanaufyata

Nchi hii Hawa vikongwe nao sio wa kuwaamini Sana hiyo wanaita katiba mbovu waliinyamazia kimya wakila kuku kwa mrija wanataka vizazi vyao viendelee Mama Samia Mimi Kuna Mengi huwa nakukosoa lakini Hawa vikongwe wasikupelekeshe kutaka Koo zao zote zijae bungeni na serikali ni vyeo vya juu Ni unfair

Kikwete Mwanae Mbunge ,mkewe mbunge no huwezi kuona Kuna kelele kipindi Cha Magufuli

Hao wanalia Lia wanadhani Wana hati miliki ya utawala kwenye nchi

Mama Samia jiongeze.Wakipiga Mikelele si lazima ufanye watakavyo watakuyumbisha hao
 
Suala la Katiba alianza kuliona Nyerere, yeye Msuya akiwa kiongozi mkubwa awamu ya pili na ya tatu.... alichukua hatua gani kuhakikisha watanzania wanakuwa salama?...

Utagundua Mzee nay ni mnafiki tu kama wanafiki wengine, utagundua pia hata Makonda alikuwa sahihi kumtandika vibao Warrioba.... Mateso yote wanayopitia watanzania kwasasa ni msingi mbovu na dhaifu ulioachwa na hawa wazee huko nyuma..
 
Back
Top Bottom