Mzee Butiku kwahiyo na Wewe ulivyokuwa Ukilalamika sana Kipindi cha Rais Kikwete ulikuwa na Shida na Mjinga au?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
"Watanzania wa Siku wamekuwa ni Watu wa Kulalamika tu sijui kwanini na sababu za Kulalamika huwa ni Mbili tu ambapo Kweli Mtu huwa ana Shida na nyingine ni Mtu tu kuwa Mjinga na kutojua Mambo mengi" Mzee Butiku Kada wa CCM na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Chanzo: ITV Tanzania

Mzee wangu na Poti ( Mwetu )wangu kabisa wa Kizanaki Mzee Butiku ( Baba Mbeza au Baba Sangu ) ulikuwa Timamu kweli ulipotoa Kauli hii au yawezekana labda ulionja kidogo Brandi ile ya Kizanaki?

Mimi Mwanao GENTAMYCINE wala sikusemi hapa ila nakuacha Watanzania waseme nawe ila Mimi nitakuja Kwako hapo Mabwepande kukusema vizuri au kama baadae utaenda Kumsalimia Binti yako Kipenzi aliyeolewa na Mzungu ( Mjerumani ) pale Ilala Bungoni Gereji jirani na Chuo cha Uandishi wa Habari cha DSJ tutakutana hapo hapo unieleze Mwanao ulikuwa na maana gani hasa ulipoitoa Kauli hii.

Wazee wetu henu pumzikeni kwa sasa.
 
Back
Top Bottom