Mzee Butiku: Hili la Rais kutoka au kutotoka ni la utaratibu

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,763
35,205
Akimalizia mazungumzo yake kwenye mdahalo wa CCM unaorushwa mubashara TBC muda huu Mzee Butiku ameuliza "mbona Uingereza malkia yupo....., mbona Angela Merkel yupo miaka 16? Mradi tufate taratibu"

=======

MZEE BUTIKU: Mimi nampenda sana Rais Magufuli, ngoja niseme hili hapa leo. Watu wengi wanasema mkali, mimi ningependa awe mkali zaidi. Kweli ningependa huko aliko mkali zaidi kwasababu tusipojipanga vizuri na chama cha mapinduzi kisipojipanga vizuri kikasimia serikali yake vizuri, hatuwezi kuvuka sasa hivi katika dunia ya sasa hivi ya ushindani, dunia ya Marekani, dunia ya Wachina, Wahindi, dunia ya watu wanaoongezeka haraka, hatutavuka.

Kwahiyo mnataka Rais ambae ni mpole lakini ni mkali.

Hili la kutoka kutotoka ni la utaratibu, ameniuliza jana mtu wa Deustchwele mambo ya kung'atuka, sikutaka kuzungumza hilo. Nikasema mambo ya kuacha ni mambo ya kuzungumza tu, mbona waingereza, wazungu wameongoza miaka mingapi? mingi masultani haya yamekaa yanaendesha nchi zao, nani aliwauliza? Waongo tu, Waingereza hapo wana malkia, nani anamuuliza? Huyu mama Makel mwaka huu wa ngapi? Wa 16, kwa hiyo watanzania tuwe huru tukitaka kuzungumza mambo haya ya wakati, wakati ukifika tunazungumza tu, ni mambo ya kuzungumza mkitaka kuamua mnafanya.

Lakini yasitupotezee muda, sijui 10, 5, sijui atoke lini! Priority ya sasa hivi ni maendeleo ya wananchi. Lakini tufate utaratibu, hapana mazungumzo ya holela hapa, mazungumzo yanafata utaratibu.
 
Akimalizia mazungumzo yake kwenye mdahalo wa CCM unaorushwa mubashara TBC muda huu Mzee Butiku ameuliza "mbona uingereza malkia yupo....., mbona Angela Merkel yupo miaka 16? Mradi tufate taratibu"
Hata hivyo ukiachana na precedent ya marais wa huko nyuma kuondoka madarakani, hakuna kitu kingine cha kumzuia.

Watanzania washapigika kikamilifu, njaa na kukata tamaa. Tayari wako KIBRA.

Wanaishi kwa matumaini tu.

Ni yeye tu aamue kubaki au kustaafu, hakuna wa kusema chochote wala kumzuia.

Kama ni katiba anaivuruga kila siku.( Angalia suala la Wabunge wa CHADEMA maarufu kama COVID-19 ).

Kwasasa ana uwezo wa KUFANYA CHOCHOTE wakati WOWOTE.
 
Nitapita kitaa kusikilizia maoni ya wasiokua na access ya mitandao maana Butiku amesema " Madaraka yote ya serikali na ya chama cha mapinduzi yanatoka kwa wananchi"
 
Hata hivyo ukiachana na precedent ya marais wa huko nyuma kuondoka madarakani, hakuna kitu kingine cha kumzuia.

Watanzania washapigika kikamilifu, njaa, kukata tamaa. Tayari wako KIBRA.

Ni yeye tu aamue kubaki au kustaafu, hakuna wa kysema chochote wala kumzuia.
Ila kusema ukweli kama huyu mzee ana huruma na Watanzania, basi hiyo miaka yake 10 inamtosha sana. Akiongeza mingine isiyo na kikomo, basi tutarajie kuona baadhi ya Watanzania wakiikimbia nchi kwa kasi ya ajabu.

Huenda yale ya wahamiaji kutoka Ethiopia, yakahamia kwetu. Hii ni kutokana na Serikali yake kutumia nguvu nyingi kwenye miundombinu, huku maeneo mengine yanayo gusa maisha ya watanzania moja kwa moja mfano ajira kwa vijana, mzunguko wa fedha mtaani, nk. Yakiendelea kupuuzwa.
 
Nitapita kitaa kusikilizia maoni ya wasiokua na access ya mitandao maana Butiku amesema " Madaraka yote ya serikali na ya chama cha mapinduzi yanatoka kwa wananchi"
Hakuna haja. Tayari lipo bunge ambalo ni wawakilishi wa hao wananchi, tena wengine walipita bila kupingwa kwa jinsi wanavyopendwa.

Watanzania kwasasa ni waoga sana, ni ngumu kwao kutoa Mawazo huru mtaani. Wengi wao wanakwepa kuzungumzia siasa mitaani, vijiweni mpaka kwenye simu.
 
Back
Top Bottom