Mzee Bruno Mpangala aaga dunia

pole sana famila..

huyu mzee tulikua naye karibu wakati alipokuwa katibu wa ccm Arusha..enzi hizo cham kinashika hatamu ..ilikuwa kofia zimetenganishwa....kabla ccm kuja na kofia mbili yaani mkuu wa mkoa anakuwa katibu wa ccm...hapo yeye akahamishiwa mbeya...baaaye TFTU Akiwa na mzee peter nyamhokya...hawa ndio waliomualika nyerere may day akatoa ile hotuba yake maarufu..

nilimuona mzee bruno mwaka jana ...huyu pamoja na watu kama kina paul kimiti walikuwa watu waadilifu sana....lakini kinasikitisha sana kuwa mfumo wa mafao ya kustaafu ulifanya watu kama bruno waishi maisha ya taabu kidogo baada ya kustaafu....sidhani kama maisha yake ya ustaafu yalikuwa na furaha sana..kama kawaida ya watu waliofanya kazi enzi za mwalimu!!!
RIP

kuhusiana na pension yake
yeye mwenyewe na familia yake waliponda sana maisha wakati wa enzi za uongozi wake

pension moja inatosha kama wewe ukiwa na mke wako tu na sio familia kubwa ya kuhudumia, ukiwa na majukumu mengi inabidi ulipe pension kubwa au ulipie pension zaidi ya moja (hata nchi za ngambo watu wanalipa pension zaidi ya moja)

RIP bruno
 
duh.. wiki hii iliyopita nilikuwa nimejiuliza sana juu ya mzee huyu na hasa wakati naandaa kurusha ile hotuba ya Nyerere. Wafanyakazi wamepata pigo kubwa leo. Mungu ailaze roho ya Marehemu pema peponi na kuwapa faraja familia yake.
 
kuhusiana na pension yake
yeye mwenyewe na familia yake waliponda sana maisha wakati wa enzi za uongozi wake

pension moja inatosha kama wewe ukiwa na mke wako tu na sio familia kubwa ya kuhudumia, ukiwa na majukumu mengi inabidi ulipe pension kubwa au ulipie pension zaidi ya moja (hata nchi za ngambo watu wanalipa pension zaidi ya moja)

RIP bruno

Pensheni ipi unayoizungumzia? ya Sh. 20,000 ama chini yake kwa mwezi hadi iliporekebishwa mwaka jana na ambayo inapatikana baada ya miezi sita? Zingatia kwamba hiyo ndiyo pensheni waliyokuwa wakiipokea wazee hawa waliolitumikia Taifa kwa uaminifu mkubwa.
 
Bruno alikuwa mzalendo sana, MUNGU AILAZE ROHO YAKE mahala pema PEPONI. AMEN.
 
kinachonishangaza ni kuwa Waziri mkuu akiacha kazi kwa mtindo wa Lowassa bado analipwa sijui Asilimia 80 ya mshahara wa current PM. Hivi kwanini wasitumie kigezo hiki hiki kwa wafanyakazi wote?
 
buriani e Mpangala,
ulazwe pema pahala,
nasi twakuombea sala,
peponi pema mahala.

utakumbukwa daima,
hasa kwa yako mema,
umetuachia hekima,
hatutachoka kusema.

wewe umetangulia,
na pema kujikalia,
hata yule simbakalia,
daima atakulilia.

kwaheri Bruno kwaheri,
tunakuombea heri,
tutadumisha kweri,
daima si kwa shari.
 
Pole kwa akina Danford Mpangala & family popote pale mlipo.. Mungu amlaze mahali pema peponi!
 
Pole wafiwa.
Pole wafanyakazi wa Tanzania
Pole wote walioguswa na kifo chake
 
Mzee mpangala Mungu akulaze pema peponi na mwanga wa milele akuangazie. Wafiwa Mungu awafariji
 
RIP Mzee Bruno Mpangala. Mungu aipe nguvu familia ya Mzee Mpangala, ndugu, jamaa na marafiki zake wote katika kuvumilia msiba huu mkubwa.

Mzee Mpangala ataendelea kuishi katika kumbukumbu zetu kama mtu alietumikia Taifa kwa uwezo mkubwa, uaminifu na uadilifu.
 
Back
Top Bottom