George Smiley
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 471
- 266
Clips zake zimezagaaa kwenye whatsapp na kwa kweli katika walio rekodi voice notes kumjibu wameishia kutapa tapa tuuu. Mzee Baraka anasema kuwa kumekuwepo kwa systematic misrepresenataion ya Mzanzibari na asili yake. Kuanzia utamaduni mpaka siasa.
Na tatizo ni kuwa kuna slave mentality kubwa sana kisiwani kule. Historia imekaa kuwasifia na kuwapa heshima kubwa sana former ruling elites na Slave owners (watawala wa kiarabu toka Oman). Wengine wanadiriki kusema kuwa kule visiwani Zanzibar kulikuwa hakuna watu mpaka walipokuja Waarabu.
Hivi jamani kweli historia ya hivyo visiwa imeanza baada ya kuja mwarabu? Na baada ya mapinduzi yaliyomletea heshima mwafrika leo tunaambiwa kuwa waarabu walinyanganywa mashamba yao kinguvu.
Hii ni sawa na vita ya Mugabe na waingereza kudai ardhi. Mtu katoka kwao arabuni kisha anakuja kuchukua ardhi ya watu kwa nguvu na baada ya kutimuliwa na wa aAfrika leo tunaambiwa kuwa si sawa na wengine wamesusia sherehe za mapinduzi ya kumwondoa mkoloni mwarabu.
Kitu kingine huyu mzee anazungumzia issue ya utamaduni na asili ya mzanzibari. Sielewi kwa nini watu wamehamaki na kushindwa kujibu hoja za msingi. Utamaduni wa mzanzibari si huu wa kiarabu ambao tunalazimishwa kwenye hii miaka ya karibuni tuikubali. Ukweli ni kuwa wazanzibari wenyewe hasa hatuonyeshwi na wamefutwa kabisa kwenye kila sehem.
Hii inaitwa cultural imperialism. Hawa hawa wanaotetea waarabu ukiwauliza hao mnao watetea wana wa treat vipi waafrika huko arabuni wako kimya. Inshangaza sana
Nakumbuka memba wetu PASCO aliwahi kusema kuwa hata hicho kitabu kinacho sifiwa kuwa kimeweka sawa historia ya mzanzibari kimejaa revision ya kuwafanya waarabu wastaarabu na waliofanya mapinduzi ni watu wa ovyo.
Leo baada ya kumsikia huyu mzee nimeamini kuwa ni kweli huyu mzee anasema maneno na hamumunyi kama Mugabe. Na kama kuna mtu hapendi anaweza kuondoka akaishi Oman ambako kuna mafuta na gesi na hali nzuri za kimaisha.
Kwanini watu hawataki kukubali kuwa Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar yalikuwa ni ya kumkomboa Mzanzibari mnyonge na mtumwa toka kwa Mkoloni na mtawala Mwarabu?
Hebu msikilize hapa:

Last edited by a moderator: