Mzee asaka aliyemkata nyeti

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI wa Kijiji cha Kibuta wilayani hapa, Bw. Abdallah Kifo (67) ameiomba serikali kumsaka kijana anayetuhumiwa kumkata sehemu zake za siri ili
achukuliwe hatua za kisheria.

Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Bw. Seleman Jafo juzi, Bw. Kifo alisema kijana huyo ambaye alitenda unyama huo anajitokeza kijijini hapo nyakati za usiku na kutamba huku viongozi wa kijiji hicho hawachukui hatua.

"Mtuhumiwa huyu akionekana kijijini hapa ananitishia kuniua wala sijui ni kwa nini hakamatwi kupelekwa polisi," alisema Bw. Kifo.

Bw. Kifo alisema alipatwa na mkasa huo Oktoba 22, mwaka jana alipovamiwa nyumbani kwake na vijana watatu waliomkaba na kumkata nyeti zake.

Alisema baada ya tukio hilo alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) ambako alilazwa na kutibiwa ambako sasa anaendelea vizuri lakini amekuwa mlemavu.

Bw. Kifo alisema chanzo cha mkasa huo ni fedha alizokuwa anadaiwa sh. 450,000 alizokopa kwa mtu mmoja (jina tunalo) lakini alishindwa kuzirudisha kwa muda waliokubaliana, hivyo kumnyang'anya mabati 20.

Alisema alilipa sh. 300,000 na kubakiza deni la sh. 150,000, hivyo kutaka arudishiwe mabati yake ambayo aligoma kuyatoa.

Bw. Kifo alisema kulitokea mtafaruku mkubwa uliosababisha mtu huyo awalipe fedha vijana watatu ili wamkate nyeti kumkomoa.

Anasema ulemavu huo umemsababishia mtafaruku mkubwa katika familia yake na anaishi kwa kuomba kwani anashindwa kufanya kazi za kutumia nguvu na anajisaidia haja ndogo kwa taabu.

Mbunge wa Kisarawe, Bw. Jafo aliahidi kumsaidia matibabu na kufuatilia tukio hilo polisi kujua sababu zinazokwamisha kumkamata mtuhumiwa huyo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibuta, Bi. Mwanjaa Manoza alisema mtuhumiwa huyo bado anawindwa akikamatwa atafikishwa katika vyombo vya sheria.
 
Back
Top Bottom