Mzee Ally Hassan Mwinyi pekee alijaribu, alivunja Baraza la Mawaziri la Muungano mwaka 1990 alipoona kuna shida mahala

Tarehe 13 mwezi August mwaka 1990 magazeti yote ya Tanzania yalikuwa na vichwa vya habari vilivyohusu kujiuzulu kwa baraza la mawaziri jana yake yaani tarehe 12.

Taarifa hizo zilisema kuwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais mzee Ally Hassan Mwinyi aliwaambia mawaziri wote wakiongozwa na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, Joseph Sinde Warioba kwamba, wajiuzulu na warudi makwao na wampishe atengeneze baraza jingine la mawaziri.

Taarifa hizo zileendelea kutaarifu kuwa Rais Mwinyi alisema kuwa shughuli zote za baraza la mawaziri zingekuwa chini ya makatibu wakuu wa wizara.

Baraza hilo pamoja na mzee Warioba lilikuwa na waziri wa Fedha Cleopa Msuya, waziri wa serikali za mitaa Paul Bomani rip, waziri wa mambo ya Nje Benjamin Mkapa rip, na mzee Rashid Mfaume Kawawa rip ambae alikuwa waziri asie na wizara maalum.

Wengine ni mzee Al Noor Kassum rip ambae alikuwa waziri wa madini na nishati, Jackson Makweta rip waziri ofisi ya Rais(Ulinzi) na mzee Muhidin Kimario rip ambae alikuwa waziri wa mambo ya Ndani.

Hawa mawaziri ni baadhi ya mawaziri wa serikali hiyo ambayo iliundwa mawaziri 26 na manaibu waziri 14.

Kama kawaida mawaziri waliwasili Ikulu siku hiyo kwa mkutano wa baraza la mawaziri ambao ungechukua hadi masaa matatu.

Kwa mshangao wao kikao hicho kilichukua dakika tatu tu pale Rais Mwinyi alipotamka kwamba anataka mawaziri hao wote wajiuzulu na warudi makwao.

Waziri wa mambo ya nje, mzee Mkapa(RIP) alichanganyikiwa na kumwambia Rais kuwa alikuwa tayari ana "engagement" za mikutano Ulaya na akaambiwa "Cancel it".

Wakati hayo yote yakifanyika mwenyekiti wa CCM hayati baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa angani akielekea Rome nchini Italia.

Mwalimu pamoja na kuongea sana na siasa thabiti, moja ya udhaifu wake ulikuwa ni kutowachukulia hatua mawaziri ambao walikuwa wanamuangusha kwenye idara ya kuwajibika na ufisadi.

Kuna kipindi hayati Mwalimu aliwahi kutembezwa maeneo ya Msasani na Mikocheni na kuonyeshwa nyumba za baadhi ya mawaziri wake na alifahamu walipata kiasi gani cha mshahara kulinganisha na majumba aloyaona lakini alibakia kushangaa.

Hivyo mzee Mwinyi akiwa anaelewa hayo alimfuata hayati Mwalimu uwanja wa ndege kabla hajatimkia Rome na kuhakikisha ameondoka kabla ya kurudi Ikulu na kuchukua maamuzi hayo magumu.

Hayati Nyerere alipofika Rome na kupokelewa na vijana wa pale wakampasha habari za Dar-es-Salaam na akashangaa kweli, ila kimoyomoyo alishukuru kuona angalau Mwinyi ameweza.

Baadae, Rais Mwinyi akiongea na vyombo vya habari alitoa sababu za msingi za kuwataka mawaziri wake wote wajiuzulu na akasema kuwa ni vitendo vya rushwa na kutowajibika kwa mawaziri kulikokithiri khasa katika wizara zao.

Alitoa mifano ya wachuuzi kuombwa kitu kidogo pale walipotaka haki zao na hata wastaafu hali ilikuwa ni hiyohiyo, na hata kuambiwa "njoo kesho, njoo kesho".

Msemo wa njoo kesho ulikuja kupata maarufu baadae pale ulipotumika kukemea vitendo vya rushwa na ufisadi na hata kutungwa wimbo wa FAGIO LA CHUMA KUWAKUMBA WALE WASOWAJIBIKA.

Huku kukiwa na shauku ya kutaka kufahamu baraza jipya la mawaziri laja, wananchi walianza kuvumisha kuwa kutakuwa baraza jipya kabisa lenye sura mpya, lakini wakikatishwa tamaa pale mzee Joseph Sinde Warioba alipotangazwa ndiye waziri mkuu anaeendelea.

Si kwamba Mzee Warioba nae alikuwa ni fisadi au mla rushwa lakini wananchi walitegemea Rais Mwinyi angebadilisha kila kitu na kuanza upya "once for all" au "the beginning of new chapter".

Hivyohivyo kwa baraza la mawaziri mawaziri saba walipoteza nafasi zao Al Noor Kassum, Aaron Chiduo, Muhidin Kimario, Damian Lubuva, Chrisant Kissanji, Arcado Ntagazwa na mama Getrude Mongela.

Mzee Mwinyi akatolea mfano wa yeye mwenyewe akiwa waziri wa mambo ya ndani ilibidi ajiuzulu pale yalipotokea mauaji yasiyoeleweka kule Shinyanga ambapo polisi walihusika na mauaji yale.

Lakini uamuzi wa mzee Mwinyi kuwataka mawaziri wake wajiuzulu haukutoka bure bali kuliktokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na kamati kuu ta CCM au CC kama inavyojulikana na kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mwalimu iliabaini taasisi na wizara zipatazo 12 ndizo zilikuwa na shida.

Wizara ya sheria, mambo ya ndani, wizara ya afya na wizara ya ardhi zilisemwa kuwa hali ya rushwa na ufisadi ilikuwa imefikia kiwango cha juu.

Mwalimu akaamuru wahusika wote ambao ni mawaziri wafike kwenye kikao cha kamati kuu lakini uamuzi huo ukapigwa chenga na mawaziri khasa mzee Kimario wakaamua kujiuzulu kuliko kwenda kwa CC kujibu masuali ya Mwalimu na wajumbe.

Ila tatizo kama kawaida likajirudia na mzee Mwinyi akawarudisha mawaziri wake waandamizi kama Mkapa, Msuya, na wengine akawabadili wizara.

Ila kukaja sura mpya kama mzee Nalaila Kiula ( kukawa na kichwa cha habari kilochosema "Nalaila Kiula aula"), mazee Jakaya Mrisho Kikwete akawa waziri wa nishati, madini na maji, Charles Kabeho (elimu).

Akijitetea raisi Mwinyi akasema hakutaka kubadili baraza zima kwa sababu ilibakia miezi minne kabla ya kuvunja bunge kwa ajili ya maandalizi ya uchuguzi mkuu.

Hata hivyo raia Mwinyi aliagiza kuwepo uwajibikaji, kuondoshwa kwa vitendo vya rushwa, kupunguza safari za nje na semina zisizoeleweka.

Kuhusu balozi zetu nje, akaagiza kuwepo balozi na msaidizi wake mmoja tu na kila mwezi atakuwa akifanya mikutano na wananchi.

Wananchi wenye shida mbalimbali za ardhi, mikopo, mafao na kesi kucheleweshwa zote raisi Mwinyi alikuwa akizishughulikia mwenywe na wasaidizi wake pale CCM Lumumba.

Hata kule Zanzibar raisi Idris Abdul Wakil nae alifanya hayo na kukutana na wananchi kusikiliza shida zao na aliwaita polis, maofisa wa wizara na CCM kujibu masuali kadhaa.

Ninachotaka kusema ni kwamba matatizo ya nchi yetu hayakuanza leo na wala hayataisha leo.

Tunahitaji viongozi wetu kujituma na kufanya maamuzi khasa ya kuokomboa nchi yetu kiuchumi.

Raisi aweza kufanya mabadiliko ya hapa na pale katika baraza lake la mawaziri lakini tatizo lipo kwenye mfumo wote na khasa kule chini ambako mkurugenzi wa maendeleo au afisa mtoza ushuru ana uwezo wa kukwapua fedha za umma na kujilimbikizia mali bila kugundulika mapema.

Serikali itengeneze mifumo sahihi iliyo na ufanisi na uelevu wa kubaini wizi na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Raisi aliepo sasa asimwonee mtu aibu, kama kuna waziri hawajibiki ipasavyo apishe na kama ni baraza zima ( kwa Tanzania Bara) halielewi linafanya nini liondolewe na aanze upya hadi 2025.
Hebu tuondolee upupu wako!
 
Hayati Nyerere alipofika Rome na kupokelewa na vijana wa pale wakampasha habari za Dar-es-Salaam na akashangaa kweli, ila kimoyomoyo alishukuru kuona angalau Mwinyi ameweza.
Hah hah , nacheka lakini nimejifunza kitu kikubwa ktk uzi huu kupitia historia ya tukio hili.

2021 kuna kila haja ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na pia kutimuliwa kwa viongozi wote wa idara muhimu katika nchi hii, lakini sijui kwanini kuna kusitasita wakati mazingira yanafanana kama vile Mwl. Nyerere alivyokuwa Rome Italy. Mwaka huu 2021 'mwenyewe' aliyeteua baraza hili na watendaji wakuu wa idara zote maalum hayupo pia hawezi kurudi kushangaa kama Mwalimu Nyerere.
 
Dogo mwaka 2007 JK alilazimika kuunda upya serikali baada ya EL kujiuzulu uwaziri mkuu
Mie sio Dogo kama unavyodhani au watania? ;)

Mzee Edward Lowasa alipeleka barua ya kujiuzulu rasmi kwa raisi Kikwete na pia mawaziri watatu akiwemo Dr Msabaha walijiuzulu.

Hali hiyo ni tofauti kabisa na nilichokieleza katika mada yangu kuzingatia mazingira ya kuvunja baraza la mawaziri.

Pia Mzee Mwinyi alivunja baraza lote la Muungano na mawaziri kama Hassan Diria rip wa kutoka Zanzibar nae alikumbwa na uamuzi huo.

Na nikasema hata raisi wa Zanzibar Idris Abdul Wakil nae akashiriki machakato wa maamuzi mapya baaya ya kuundwa baraza jipya.

Hivi mbona baadhi ya watu humu JF ni wagumu hivyo kusoma kitu na kukielewa?
 
Unfortunately hakuna miradi ilifanyiwa uchambuzi,sasa wewe reli ya kwenda Mwanza inafaida gani ikiwa mzigo wote unaenda Burundi,Rwanda na DRC ? Ukikopa kujenga hiyo reli inakumala
Tunatakiwa tuwekeze kwenye utafiti ili kama tunafanya mradi basi utafiti uwe umeshafanyika tujue kabla ya kuweka fedha au kukopa fedha
 
Back
Top Bottom