Mzee Akilimali:" Mkwasa ni tatizo nipeni uwenyekiti niwasaidie sijaitwa Abramovich kwa bahati mbaya

junky

JF-Expert Member
May 11, 2017
413
976
AKILIMALI:- MKWASA AMEYATAKA MWENYEWE

-Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali naye ametoa neno kuondoka kwa kocha wa Yanga, George Lwandamina na kujiunga na klabu ya Zesco United.

-Asubuhi ya leo mzee akilimali amesema
"Lwandamina ni kocha mzuri sana tukubali tu timu yangu imepoteza mtu sahihi, Yanga ilikuwa inamhitaji bado Lwandamina ila viongozi wa Yanga ndio wamesababisha yote haya"

"Katibu tumempigia kelele kila siku atangaze mchakato wa uchaguzi ili nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo ijazwe ila yupo kimya. Timu imekosa fedha za kujiendesha kwa sasa ila angekuwepo mwenyekiti angekuwa na yeye ana mawazo chanya ya kupata fedha"

"Wamevunja Katiba ya Yanga kwa matakwa yao wenyewe, matatizo ambayo yapo kwa sasa klabuni hapo yamesababishwa na viongozi waliopo kwa sasa kwa kukumbatia mambo wenyewe wamekuwa wasiri kila jambo ona sasa wanaumbuka"
Alisema Mzee Akilimali

-Mzee akilimali alipoulizwa swali yeye kama katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga inaisaidiaje klabu hiyo kwa sasa na matatizo ambayo yaliyopo mzee Akilimali alijibu

"Katibu atangaze mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa na Bwana Yusuph Manji iwapo wana Yanga watataka niwe mwenyekiti wa klabu hiyo nitaisaidia kwa moyo mmoja"

"Watu hawajui jina la abramovich limetoka wapi mimi sishindwi kuisaidia klabu ya Yanga kwa sasa ila nitaisaidiaje niko nje ya mfumo"

Alisema Akilimali kwa sauti ya upole.

FB_IMG_1523793294282.jpg
FB_IMG_1523793433661.jpg
 
Mjini was mjini huyo hana lolote. Mwanzoni alikuwa mfuasi wa Manji hadi kifurushi kilipokata. Huo ukatibu wa baraza la wazee upo kwenye katiba ipi ya Yanga?
Hilo baraza lenyewe lina katiba au kanuni? Wazee wepi walimchagua?
Uchaguzi kilabuni huwa msimu wa mavuno kwake.
 
Nimecheka sana hii habari ilipoambatana na picha ya Akilimali na Abramovich....mzeee njaa inamsumbua sana ujana wake sijui alikuwa anafanya nini
 
Hawa wazee wapo halfway, yapo wanayoyasimamia ni ya kweli lakini sehemu zingine wanakosea.
Mimi ni Simba fan, na haya yanayoelezwa na Mzee Akilimali, yapo yanayoakisi ukweli.Kwa suala la timu kukaa bila kuziba pengo la Mwenyekiti, hilo ni tatizo.Wanachama wanapaswa kuwa majasiri ili kuziba ombwe la uongozi lililopo mitaa ya Twiga na Jangwani.
 
Yaani huyo Mzee ndio awe mwenyekiti wa Yanga? Dah!

Na aliyemwambia Akilinywele kuwa Lwandamina alikuwa kocha mzuri ni mganga, si vinginevyo.
Kwa suala la Lwandamina, mimi ninakubaliana na huyu babu kuwa alikuwa mzuri though mbinu zake za ufundishaji na upangaji wa timu zilikuwa zinapishana kwa kiasi kikubwa na mtangulizi wake Babu Hans Van Pluijm.
 
Kwa suala la Lwandamina, mimi ninakubaliana na huyu babu kuwa alikuwa mzuri though mbinu zake za ufundishaji na upangaji wa timu zilikuwa zinapishana kwa kiasi kikubwa na mtangulizi wake Babu Hans Van Pluijm.
Tangu aje Yanga timu imepoteza rhythm. Tunaungaunga tuuu na limwili lake kubwa kama soseji ya kuchoma. Babu Hans aliifanya Yanga ivutie, uswahili wa hivi vibabu ukamuondoa
 
Yanga inahitaji iongozwe na watu wenye exposure kubwa na wasomi..hawa wazee wapumzike pembeni..hawa wazee wapo yanga miaka mingi sana ila timu haina hata uwanja wala hosteli za wachezaji zakueleweka
Timu ya chama hiyoo
 
Back
Top Bottom