Mzee abuni umeme wake "haukatiki, sijasoma nilitengeneza helikopta wazungu wakachukua"

Nimefuatilia hoja zako ziko sawa lakini nadhani tunakosa maelezo ya huyo mzee ili afumbue macho zaidi. Maelezo ya pande zote mbili yataleta uhakika zaidi

Kila technology huwa ina selling point yake, sasa nadhani yeye selling point yake ni jinsi anavyocheza na hizo sumaku hadi kutengeneza hio endless motion(Japo he clearly defies current laws of physics on that). Ila hatuwezi kuwa na uhakika kwamba yuko nje ya laws of Nature coz laws za physics nyingi huwa zina flaws kama vile zamani tulijua newton's laws of motion na equations zake ni DOGMA lakini Einstein akaja kuonesha at the speed of light vitu vina-defy hizo eqns.

Kuna vumbuzi ukiziangalia kwa macho ya physics ya sasa hutoweza kuvielewa lakini bado vinawezekana kwenye nature. Mfano vumbuzi za Nikola Tesla ambazo hadi sasa wengi wanashindwa kuzielewa na kuzifanyia kazi.

Kama kuna video huyo mzee alihojiwa naomba muiweke hapa ili tujue kiundani coz hio machine yake inaweza kubadili dunia .


Cc The Monk
Ushauri kwa huyo mzee achukue hio working prototype (kama kweli inafanya kazi) aitengenezee patent sio tu Tanzania bali worldwide alafu baada ya hapo ndio atoe maelezo kwa public hapo kila mtu atakayetengeneza atamlipa na atapewa credit..

Haitakuwa jambo jema aseme wazi inavyofanya kazi bila patent sababu ataibiwa...,

ila kama ni attraction and repel of magnets kumbuka kwenye attraction huenda usitumie energy (sumaku zitavutana) ila zikishavutana utahitaji the same energy kuzitenganisha na hata ukiweka mpangilio kwamba zivutane kabla hazijavutana vizuri zitengane ni energy kiasi gani itatoka ? Na ukiweka load (yaani matumizi) je zitaendelea kuvutana ... , mfano kuna toy ilishatengenezwa Drinking Bird inayoendana na evaporation na condensation ya alcohol kwenye kichwa cha hio toy ila quantity ya nishati ikawa mediocre (hence it being a toy), yaani ukishaweka load, friction n.k. huwezi kupata chochote... Hata hivyo hio toy nishati yake ilikuwa ni hayo maji ambayo yanasababisha temperature difference...

 
In Physics,, Vyote vilishavumbuliwa na sasa ni matokeo ya application of physics laws
Hii Jamani sio ugunduzi acheni ujinga jamani
Hawa Tanesco waliokuja ni mafundi mchundo tu

Apeleke COET wakamueleze vizuri, na kumpongeza kwa kujaribu lakini it is not feasible, sababu sumaku kwa muda mrefu wa matumizi inapoteza nguvu.

Kina Tesla na kina Weber ambao wameacha majina yao kwenye sumaku, hawa walikuwa wanakula, kunywa na kulala sumaku
Walipitia yote haya kugundua kuwa sio efficient

Sasa wazungu wanatengeza magari ya umeme kwa kwenda mbele, yanatumia Lithium battery
Kwanini wasiyajue hili , haya ni majaribio ya maabara

Ok lakini najua kenge watarudi na majibu ya kishabiki pasipo ushahidi wa kifizikia

Hongera Mzee Msuya, umeleta mwamko wa kisayansi kwa kujaribu lakini POLE hii haiendi popote.
 
Kwa nchi ya siasa kama hii usitarajie makubwa Msuya,,, sogea kwa watu weupe
 
Generator inatumia mafuta yeye anatumia sumaku tu (magnet)
Point yangu ni kwamba asilimia kubwa ya umeme unaoutumia unatokana na sumaku na wire Faradays law of electomagnetic Induction..., ukimove sumaku sambamba na conductor unapata voltage.., kwahio iwe umeme wa upepo au wa maji au wa petroli au wa steam au wa hewa, mwisho wa siku ni umeme wa sumaku hizo mechanical energy zinatumika ku-move either conductor au sumaku...

Kwahio bila ya kujua ufanisi ni vigumu kujua how big is the breakthrough..., ingawa kama inatoa power kubwa zaidi kuliko currently available generators basi asibakie kuongea na Tanesco tu, bali ulimwengu mzima unamuhitaji ukizingatia energy is very important...
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Huo ndo umaskini wa akili...angeuza hiyo teknolojia pia wangekubaliana kwenye mkataba apewe hisa kwenye hyo kampuni
 
Shule ikitumika vibaya ni hatari sana! Nimejaribu kupitia majibu na maswali ya wachangiaji wengi kwenye huu uzi nikaona bado tunasafari ndefu sana.

Binafsi nampongeza kipekee huyu mzee, alichonifurahisha, ubunifu wake wa kutumia sumaku kama chanzo cha mwendo. Akishapata mzunguko ndio unazungusha kifaa kinachofua umeme sasa.

Wachangiaji wengi wamekariri kwamba umeme wowote chanzo chake ni usumaku, hiyo ni kweli na haina ubishi, hapa mzee ameenda mbali zaidi kwa kutumia usumaku kusababisha mzunguko kama unaotengenezwa na injini za mitambo mbali mbali ikiwemo magari.

Generator ya kawaida inatumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mzunguko ambayo nayo inazungusha kifaa cha kufua umeme.

Huyu mzee badala ya mafuta kuwa chanzo cha mzunguko, anatumia sumaku.

Hii ikiendelezwa, italeta mapinduzi kwenye mambo mengi sana ikiwepo vyombo vya usafiri visivyotumia mafuta wala battery kuviendesha ( itategemea na nguvu ya huo mzunguko unaozalishwa).
Wewe umeelewa hasa kuhusu ubunifu wa huyu mzee sio hawa wengine wazee wa madesa wa COET
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Unakataa wakati huna mtaji wa kufanya mass production! Kuna msenegali nae amebuni mtambo awa mawäjuliano ambao unakasi kuliko hii minara ya sasa cha ajabu amegoma kuwauzia wazungu.Sasa inakuja mitambo ya 5G ya wa wachina mtambo wake atawasiliana na mkewe.
Ndugu zangu wana JF ni ujinga kuamini kuwa teknolojia unayogundua utaweza kuikuza peke yako, hata makampuni makubwa hushirikiana tuache ujinga, ukipata teknolojia uza.Mbona wazungu waliobuni wasap waliuza,waliobuni gari ya umeme ya TESLA waliuza.Kwa nini ung'anganie vitu usivyoviweza?
 
Free energy techology/ devices is not a new teknology.Ninacho kitabu cha Free energy technology kimeeleza teknolojia nyingi sana za kuzalisha energy.Sio jambo jipya ila inabidi uingie gharama kununua vifaa. Mfano Gyroscope generator, wabunifu wake wanakutumia vifaa vyote ufanye utafiti for your own risk.
Nilikuwa mfuatiliaji sana sana hizo tech nikaanza kuzipotezea baada ya kugundua zina complication halaf hazilipi.
Binafsi nilidizaini mifumo 3 . mmoja unahitaji nutumie fresnel lens ambayo kuipata hapa bongo ni ishu. Mfumo wa pili unatumia gravty + harmonic motion. Diagram zake nimezitupilia mbali.
 
Create a story that will improve lives of your fellow citizens....sio ku-fubricate story za uongo kuyumbisha watu waache kujadili mambo ya msingi
Mambo ya msingi ni yepii? na una uhakika gani kama hili sio jambo la msingi?
 
Free energy techology/ devices is not a new teknology.Ninacho kitabu cha Free energy technology kimeeleza teknolojia nyingi sana za kuzalisha energy.Sio jambo jipya ila inabidi uingie gharama kununua vifaa. Mfano Gyroscope generator, wabunifu wake wanakutumia vifaa vyote ufanye utafiti for your own risk.
Nilikuwa mfuatiliaji sana sana hizo tech nikaanza kuzipotezea baada ya kugundua zina complication halaf hazilipi.
Binafsi nilidizaini mifumo 3 . mmoja unahitaji nutumie fresnel lens ambayo kuipata hapa bongo ni ishu. Mfumo wa pili unatumia gravty + harmonic motion. Diagram zake nimezitupilia mbali.
Kwahio hao wabunifu wameona tabu kutengeneza wenyewe working prototype na kuiuza ulimwengu mzima wameona wauze vifaa ili mtu atengeneze mwenyewe ?

Hii haina tofauti na masharti ya mganga wa kienyeji ambaye hawezi kujiganga
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Muongo huyo anatafuta kiki tu. Njaa ilivyo mbaya akatae cash money?
 
Back
Top Bottom