Mzee abuni umeme wake "haukatiki, sijasoma nilitengeneza helikopta wazungu wakachukua"

Tunafanya makosa makubwa sana kudhani kusoma ni mpaka uende shule au ubunifu na akili ni mpaka uwe na cheti HAPANA ubunifu na akili / fikra ni watu wanaofikiri nje ya box na kutumia material katikati ya masikio yao kufanya vitu endelevu

Faraday mwenyewe hakusoma (ni self Taught)
Ndiyo hiyo kwa Tanzania inakuwa ngumu kama hujafika shule, mbona zamani wazee walikutumia wanafua majembe, shoka lakini walienda wapi si wakaanza kuleta ya China kila mwaka mkulima unanunua? Watanzania ni wengi sana wabunifu lakini hiyo nafasi hakuna, Mimi mwenyewe kwetu alikuwepo kijana STD 7 alikuwa anaunganisha mazagazaga yake umeme kwa Bibi yake muda wote taa inawaka
 
Kutana na Rojas Mathayo Msuya mkazi wa Kawe Dar es salaam ambae amebuni mtambo wa kuzalisha umeme unaotumia nguvu ya sumaku na good news ni kwamba mtambo huo wa umeme ukishafungwa kwenye nyumba yako haulipiwi tena baada ya kutoa gharama za kutengenezewa.

Rojas anasema "Taaluma hii sijasoma, nimejifunza mimi mwenyewe kupitia kwa baba yangu, zaidi ya robo tatu ya umri wangu nimetumia kujaribu kuunda vitu vingi.

Mimi ndie mtu pekee niliyeunda Helikopta iliyotumia sumaku hapa nchini na ikaruka"

*Mtambo huu wa kufua umeme hapa ulipo unaweza kufanya kazi, mainjinia wa Tanesco walikuja wakapima na wakaona upo sawa kabisa kwa matumizi ya nyumbani, naibu waziri alikuja tarehe 25 January kuangalia" Rojas.
Hongera sana mzee kwa kujitahidi kufanya kitu cha maendeleo
 
Kuna ukweli au ni kawaida ya kutengeneza story ili kuwayumbisha wadanganyika.

Mwendo wa sasa ni VAA BARAKOA, JILINDE NA KUWAKINGA WENGINE. CORONA INAUA!!!

Kuna watu wako busy kutengeneza miswada ambayo lengo lao wanalijua wenyewe.

Acheni kutengenza miswada inayokwamisha na kuua ndoto za watanzania na wawekezaji, kujeni na miswada itakayokwamua nchi. Ebooooo

HUU NI WAKATI SAHIHI WA KUDAI KATIBA MPYA, Ikiwezekana mihula ya Urais ipunguze kuwa miaka minne.Sio mitano tena
Safi sana minne tu inatosha
Nalog off
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Ni kheri angewauzia wazungu, Hawa jamaa wa awamu ya tano watampatia kitu fresh amvacho hatasahau maisha yake yote.
 
Ni kheri angewauzia wazungu, Hawa jamaa wa awamu ya tano watampatia kitu fresh amvacho hatasahau maisha yake yote.
AUZE KAMA HUYU Mtanzania aliyeuza teknolojia yake kwa bilioni 57.6

Mtanzania Andron Mendes ameuza mfumo wa mita ya kulipia ya kulipia gesi ya kupikia kadri unavyotumia (PAYG) kwa Kampuni ya Circle gas ya Uingereza kwa Sh.57.6 bilioni ili isambazwe kwa nchi za Afrika.

"Hakuna sababu ya kushikilia Teknolojia ambayo inapunguza matumizi ya Mkaa kwa sababu tu umeigundua. Nimeamua kuiuza Teknolojia hiyo kwa watu wenye fedha ili waisambaze Afrika" alisema Mendes wakati wa hafla ya mauziano ya Teknolojia hiyo iliyofanyika jijini Nairibi nchini Kenya.

Yaani ni Mtanzania lakini hafla inafanyikia Kenya, nasisi tunajimwambafy tuna viongozi!
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Uzalendo wa hivi utakufa maskini wenzako wanajenga chattle
 
Yaani ni Mtanzania lakini hafla inafanyikia Kenya, nasisi tunajimwambafy tuna viongozi!
Kenya soko la hisa liko open kwa kila mtu wa kutoka popote duniani sisi soko letu nadhani watanzania haturuhusiwi kwenda kununua hisa masoko ya hisa ya nje ya nchi na watu wa nje waweza nunua baadhi ya hisa za mashirika kadhaa tu sio yote sokoni
 
Niliiona hii habari ya ulee mtambo, na serikali ime thamiria kununua iyo teknolojia coz huyo mzee msuya ana dai alishawahi kufatwa na ma don toka nje ya nchi wakiwa na cash Us dollar wakitaka wauziwe iyo technology lkn huyo mzee alikataa
Ana haki miliki?
 
Ngoja tuone taifa litakavyomtumia huyu mtu. Hii lazima kujua hatima yake, kuna watu wana vitu tatizo taifa halionyeshi ku-support wabunifu hawa wakubwa tunabaki na viji-organization ambavyo vina deal na ubunifu ambao kiuhalisia ni copy and paste.
 
Back
Top Bottom