Mzazi umejipangaje kumnusuru mtoto wako anaekaribia kubalehe kwa huu utandawazi?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Suala la ukuaji wa watoto kwa asilimia kubwa sisi wazaz ndio inabidi tuhusike pakubwa , kuwapa Watoto wetu elimu na miongozo katika hiki kipindi ni muhimu sana,tukigoma kuitoa sisi wazazi basi tutambue ya kwamba watu ambao sio sahihi ndio wanaweza kuwa walimu wake.

Ni haki ya mtoto atambue kila badiliko la mwili wake na changamoto zake, kwa saizi utandawazi umekuwa mkubwa sana hasa katika kipindi hiki ambacho simu imekuwa kama kiungo kwenye miili yetu, kwenye hizi simu janja kuna mambo meusi ambayo yanaweza kumteketeza mtoto wako mifano ni

kuanza sex katika umri mdogo risk ikiwa ni mimba za udogoni ama magonjwa– hapa siku hizi kuna magrupu ambayo ni sumu kwa mwanao, mfano kuna magrupu ya kutafuta Malaya ama wachumba, kuna magrup ya fb, whatsapp, badoo, n.k sasa hapa mwanao anakuwa yupo kwenye kipindi ambacho ngono imemtawala kichwa kwa kiasi kikubwa, bila muongoza atakurupukia huku na akapata magonjwa kama ukimwi, kaswende, gono, n.k pia anaweza kuwa baba au mama akiwa na umri mdogo sana

Ushoga / Usagaji - kuna mtoto wa rafiki yangu mwaka fulani tulikuwa tunahangaika kumtafutia shule mpya maana alifukuzwa baada ya kubainika kwamba ana tabia za kishoga kama kukiss wenzake, kukumbatiana nao, kuvaa mavazi yanayotia shaka, huenda alisaanza kuf***a, yote kwa yote kijana alipobanwa alikazana kwamba hakuna kosa kuwa shoga, na bla bla nyingi ambazo zilishaashiria katoa points hizo kwenye mitandao inayojikita kulinda mashoga, ndio hivyo tena yani mtoto kaharibikiwa.

Motivational speakers wanaohamasisha shule si kitu – hapa napo Watoto wakisikiliza sana wanapunguza bidi shuleni.

Punyeto + video za X – sote tunajua vifurushi vya data hapa nchini ni bei rahisi, nchi yetu ipo katika nchi zenye gharama nyepesi sana za internet, lakini pia hii imechochea uangaliaji wa video za x zinazopelekea vijana wengi kupiga punyeto kitu ambacho kinakuwa uraibu ambao unaharibu nguvu za kiume, waweza kumzawadia mtoto simu ila kama hujampa elimu ataangamia.

Bongo flava – nako huku siku hizi Sanaa imegeuka kuhamassha ngono, pombe, bangi, n.k wasanii ndio kioo cha jamii, watoto wanaweza kuna ni ujanja kufat nyayo za maisha yanayoonekana kwenye videos za miziki

Binafsi nimejenga urafiki na watoto wangu, bado ni wadogo ila wa kwanza imebaki miaka michache tu abalehe, kwa kutambua hili, niejenga urafiki nae wa karibu kitu ambacho kimemfana awe huru kuongea na mimi kwa kujiamini endapo ana shida, katika kujenga nae urafiki mbinu nazopenda ni kumfundisha kucheza muziki, kucheza nae mpira, n.k hii inasaidia sana hata nikimtia bakora anapokosea huwa aarudi tu, naamini hii angalau itanisaidia hapo mbele hasa pale atakapokuwa anapata changamoto

1625205116568.png

 
Ili swala ni kumuomba Mungu kwasana tu maana hii dunia ya sasa aisee..Mtoto akifaulu anapewa zawadi ya simu janja kumbe ndo anapewa kaa la moto kama ni KE atanyanduliwa kirahis coz umemrahisishia mawasiliano kama ni ME atapiga nyeto mpk mkuyenge uombe Poo aisee ushaur kwa wazazi walee watoto wao kwa msingi ya dini ipasavyo labda atakua na ile Hofu ya mungu
 
Ili swala ni kumuomba mungu kwasana tu maana hii dunia ya sasa aisee..Mtoto akifaulu anapewa zawadi ya sim janja kumbe ndo anapewa kaa la moto kama ni KE atanyanduliwa kirahis coz umemrahisishia mawasiliano kama ni ME atapiga nyeto mpk mkuyenge uombe Poo aisee ushaur kwa wazazi walee watoto wao kwa msingi ya dini ipasavyo labda atakua na ile Hofu ya mungu
Asee umegonga mulemule mkuyenge lazma uombe pooo kila siku kusuguliwa s mchezo
 
Ili swala ni kumuomba mungu kwasana tu maana hii dunia ya sasa aisee..Mtoto akifaulu anapewa zawadi ya sim janja kumbe ndo anapewa kaa la moto kama ni KE atanyanduliwa kirahis coz umemrahisishia mawasiliano kama ni ME atapiga nyeto mpk mkuyenge uombe Poo aisee ushaur kwa wazazi walee watoto wao kwa msingi ya dini ipasavyo labda atakua na ile Hofu ya mungu
Mbaya zaidi simu zimekuwa bei rahisi mno yani hata elf 80 unaipata,

Huko mitandao ya kijamii ndo kabisa, watu wanafanya mambo na watoto wadogo hata wa darasa la sita wenye smartphone wanayaona
 
Suala la ukuaji wa watoto asilimia 70 ,wazaz tunausika pakubwa , tena hii elimu ya ukuaji inaitajka pakubwa sema itolewe na mtu sahihi katka mazingira ya sahihi ,ukigoma kuitoa ww mzazi basi tambua watu ambao sio sahihi ndio watampa na hapo ndio utakua unkwisha!!
Lazima mtoto atambue kila badiliko la mwili wake , na madhara yake yapoje!
 
Selfie mtu huanza peke yake. Sikuwahi fundishwa ila nilijifunza nikaona naumia nikaacha,.

Kuhusu bangi inategemea makundi rika aliyo nayo na uelewa wake kuhusu maisha, wanafunzi wengi hupotea sekondari boarding

Kuhusu porn, huwezi control maana ukimpa simu lazima ata google tu

We mfundishe Neno la Bwana hayo mengine atajiongeza
 
Nikukaa nae na kumweleze ukwel pasipo kumuonea aibu. Mwambie ukwel wa matokeo ya kila hatua atakayo ipitia kabla na baada ya barehe/kuvunja ungo, kumjengea hali ya kujikubali na kucontral madiriko atakayo yapata mwilini mwake in positive ways, mpe nafasi ya kukueleza changamoto anazozipitia kutokana na mabadiriko yake na kubwa zaid muombee kwa Mungu wako amuepushe na mabalaa ya dunia hii ya leo
 
Mtoto akishabalehe anaanza kuwasikiliza marafiki zake na info za mtaa kuliko wewe kutokana na peer pressure (hapa utaona hakusikilizi au kiburi) hivyo, kabla hajafikia huko ni vyema kumpa space ya urafiki ili awe open kwako kiasi cha kuweza kumpa taarifa sahihi kuhusu masuala ya ngono ili awe na uwezo wa kuzichuja hizo story za mtaa. Pia ni muhimu kumuweka karibu na imani ambayo itamcontrol kiasi pia
 
I believe in early marriage. Only solution. By 18 - early 20s oa/olewa. Otherwise uliyotaja hapo juu hayakwepeki. Sex is a natural human need, tuwatengenezee mazingira ya kujitosheleza in a proper way. Wahindi/Waarabu wameweza kuendeleza huu utamaduni though nao ukisasa ushawaingia.

Tatizo wazazi wenyewe hamtaki watoto wenu wakue na wenyewe utoto hawautaki. Sex inaonwa kuwa taboo in such a way that it brings more harm than good.

Wazazi wanachofanya sasa hivi ni kama mbuni anavyochimbia kichwa ardhini ili ajifiche, akifikiri haonekani. Parents have burried their heads in the sand. Yani for as long hawaoni tatizo basi tatizo halipo. Cha muhimu wanachozingatia wazazi siku hizi ni elimu na kazi tu, by default their children's sex lives are inexistent, hadi watakapooa/olewa by 30s huko.

Yani dunia ya Leo with all the readily available information, and the oversexualized media/entertainment, unategemea mwanao anayeoa/olewa by 30 kuwa 100% innocent in that department is overly ambitious in my opinion, and selfish!

Nilikuwa na rafiki yangu wa kiarabu chuo alivyofika 18 mama yake alimwambia kama unataka kuolewa sema. Binti akasem no mimi nasoma. Wengine Hadi late 20s tumeambiwa bado wadogo kuolewa!

End result ni watu kuwa na msururu wa mahusiano, people have emotional baggages, tunaoa/olewa na wake/waume za watu, people are overall just never satisfied, always looking for something better.....

Kama unavyojipinda kutafuta school fees jipinde kumuwezesha kuwa financially independent by that age. It might help reduce the modern sexual deviances!

Otherwise, we're on a road to a totally different world, nothing much you can do.
 
Main solution ni UKWELI NA UWAZI

Wazazi kaa na mwanao mpe picha halisi ya ujana na mambo yake, usimfiche mwanao na usimuone kama ni mtoto sana kumpasha habari za kikubwa.

Jenga urafiki wa karibu na mtoto tengeneza uhuru wa mtoto kuongea na wewe kuongea akijiamini.

Watanzania tuna katabia ka kudharau watoto kuwaona kama hawajui kitu, hii mbaya sana kwenye balehe, ukimu under rate sana mtoto yeye ndo atakuonesha maajabu kukuprove kuwa anajua.

Shortly ni ukweli na uwazi ndio jinsi ya kumuandaa mtoto kwenda keenye balehe yake. tuachane na zile mama ametoka kujifungua alafu anamwambia mwanae mkubwa ametoka kununua mtoto
 
I believe in early marriage. Only solution. By 18 - early 20s oa/olewa. Otherwise uliyotaja hapo juu hayakwepeki. Sex is a natural human need, tuwatengenezee mazingira ya kujitosheleza in a proper way. Wahindi/Waarabu wameweza kuendeleza huu utamaduni though nao ukisasa ushawaingia.
Mkuu nikiri kusema wewe ume elimika (huenda ni msomi mwenye veti ama huna vyeti), vp mwenzetu una elimu gani, huwa una soma vitabu?
 
Suala la ukuaji wa watoto kwa asilimia kubwa sisi wazaz ndio inabidi tuhusike pakubwa , kuwapa Watoto wetu elimu na miongozo katika hiki kipindi ni muhimu sana,tukigoma kuitoa sisi wazazi basi tutambue ya kwamba watu ambao sio sahihi ndio wanaweza kuwa walimu wake.


Haya mambo yanaanza tokea anakua.

Ukitaka kumcontrol ukubwani wakati anabaleghe hapo inahitaji nguvu ya ziada.

Ila tokea utoto wake wewe unafanya kazi ya kumprogram tuuu
 
main solution ni UKWELI NA UWAZI

wazazi kaa na mwanao mpe picha halisi ya ujana na mambo yake, usimfiche mwanao na usimuone kama ni mtoto sana kumpasha habari za kikubwa,

jenga urafiki wa karibu na mtoto tengeneza uhuru wa mtoto kuongea na wewe kuongea akijiamini

watanzania tuna katabia ka kudharau watoto kuwaona kama hawajui kitu, hii mbaya sana kwenye balehe, ukimu under rate sana mtoto yeye ndo atakuonesha maajabu kukuprove kuwa anajua.

shortly ni ukweli na uwazi ndio jinsi ya kumuandaa mtoto kwenda keenye balehe yake. tuachane na zile mama ametoka kujifungua alafu anamwambia mwanae mkubwa ametoka kununua mtoto
Hhahahah.

Mkuu kama mtoto anafikia hatua ya kumuuliza mama kwamba huyu mtoto mpya katoka wapi basi bila shaka anahitaji jawabu halisi.

Kama mtoto anauliza maswali halisi inabidi apewe majibu halisi.

Mtoto anatakiwa ajue nature kabla hajaifikia na hakuna madhara kujua nature hiyo.
 
Haya mambo yanaanza tokea anakua.

Ukitaka kumcontrol ukubwani wakati anabaleghe hapo inahitaji nguvu ya ziada.

Ila tokea utoto wake wewe unafanya kazi ya kumprogram tuuu
Tatizo ndio hapo lilipo, kina baba wengi wabongo ni makauzu sana kwa watoto, na hata akiwa sio kauzu sana basi anamelemaza sana mtoto wake kwa kumpa kila kitu kwa kisingizio cha hataki aishi kama maisha aliyopitia kumbe ndo anamharibu,
 
Back
Top Bottom