Mzazi mwizi


tetere

tetere

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
961
Likes
26
Points
35
tetere

tetere

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2006
961 26 35
Siku baba yako akikubaliana na baadhi ya watoto wake wakamwibie jirani yao, hiyo ndio siku ya mwisho ya baba huyu atakuwa baba wa familia hiyo. Malalamiko yanayoendelea yamenifundisha hili, kwamba baba akishatiliwa mashaka uadilifu wake kuanzia kwa wanae hadi kwa majirani, hawezi kuitwa baba teana. Maana kuwa baba kuna sifa zake na sifa hizi haziwezi kuwa compromised no matter what are your circumstances . Kiongozi anapotuhumiwa kuiba si kitu kizuri. Na kiongozi huyu akaamua kufanya mchezo wa kuwazomea wanaolalamika kuibiwa badala ya kijibu tuhuma hizo ni jambo serious zaidi.
Huu ni mwendelezo wa tabia za kifisadi. Unatuhumiwa kuiba pesa, unadanganya danganya na hakuna lolote linalotokea. Unatuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umma, unacheka cheka tu - hakuna lolote linalotokea. Unatuhumiwa kuwa wewe sio makini unaanza mchezo wa kuonyesha statistics ili mradi tu ushinde kwa kuongea, na sio kwa matendo au reality on the ground.

Sio kila mtu atakuwa baba,sio kila mtu ataweza kuwa kiongozi. Sasa kama baba yako ni mwizi na wewe unajua ni mwizi, utafanya nini? mchekee!!!
 

Forum statistics

Threads 1,235,139
Members 474,353
Posts 29,213,115