kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,147
- 2,745
Habari za wakati huu waungwana?
Jamanimwenzenu nina changamoto nimeipata kuhusiana na mzazi mwenzangu.
Iko hivi huyu mwanamke tumezaa mtoto ambae kwa sasa ana umri wa mwaka mmoja na miezi 7. Kiukweli toka ajifungue huyu mtoto nimekuwa nikitoa pesa za matunzo vizuri tu bila shida, ofcoz naye amekuwa akinisaidia katika malezi kwa sababu ni muajiriwa mahala fulani
Sasa basi toka mwaka juzi niliamua kwenda shule kujiendeleza, nilimshirikisha na nikamwambia kwa vile ntakuwa masomoni hivyo hata biashara zangu huku hazitakuwa zinaenda kama ambavyo nipo mimi mwnyewe hivyo nikamuahidi kuwa nampa kiasi cha 150k kutoka 250k kila mwezi kama matumizi ya mtoto
Nashukuru alinielewa,tatizo limiejitokeza mwaka huu, kwa wakazi wa Arusha mtakuwa mashahidi. Toka hii kitu inaitwa covid-19 iingie biashara zimeyumba sana pale Arusha, hivyo na mie nimejikuta nimeyumba kiuchumi,kwa hivo nikashusha kiwango cha kumtumia kama matumizi ya mtoto kutoka 150k mpaka 70k nikamueleza hali halisi.
Toka wakati huo hatujawahi kuwa na maelewano kabisa, anaona kama namfanyia makusudi lakini ukweli ni kwamba siko vizuri kiuchumi kabisa, nimemtumia watu wake wa karibu wamueleweshe lakini ni kama hanielewi vile.
Leo asubuhi kanipigia simu ananiambia kesho anaamkia Ustawi kunishtaki eti nimemtelekeza mtoto wakati sio ukweli, ikumbukwe mwezi wa tano nilimtumia 70k ya matumizi akairudisha akisema eti ndogo haitoshi hata kununua maziwa ya mtoto hivyo mwezi huu sijamtumia kitu bado kwa sababu bado hatujakubaliana kiasi cha kutumiana.
Kiukweli wakuu sina kitu kwa sasa na biashara haziko poa kabisa.
Je, nimuache aende tu huko ustawi au nifanye kitu gani anielewe?