Mzazi, mlezi usitumie lugha ya matusi unapomfunza mtoto

ShalomP

Member
Jun 14, 2019
97
154
Kuna siku nilipita mitaa fulani,nilikuwa nimetoka kwenye harakati za mapambano ya maisha na uchumi.

Nilikatiza uchochoro fulani hivi mbele yangu nilikutana na Baba mmoja yupo na mtoto mdogo mwenye miaka kati ya miwili au mitatu.

Bila shaka alikuwa mzazi wake sasa yule mtoto alikuwa anatembea huku baba yake kamshika mkono.

Hatua za mtoto na mzazi zilikuwa tofauti mtoto akawa anatembea huku viatu vikimsumbua Baba yake akaanza kumpolomoshea matusi mazito na ya nguoni.

Nanukuu "Unadhania hela tunaokota...tembeaga vizuri ukichana viatu hivyo Nita........ unajua hela tunakotafuta tembea vizuri,"

Matusi mengine ni mazito na makali siwezi kuyaaandika kwenye media hapa nitawakwaza baadhi ya watu.

Kwa kweli nilijisikia vibaya mtoto mdogo kumtukana matusi mazito kama yale.

Je,mtoto anajifunza nini kutoka kwa mzazi?

Yaani stress za maisha ziishie kwa mtoto jamani, daaah hata kama umekwazana na mtu hasira ukazimalizie kwa mtoto mdogo asiyeelewa kitu.

Tuwaoneshe upendo watoto tuwaelekeze na kuwafunza kwa upendo wataelewa unapomuhadhibu kwa viboko muadhibu kwa kumfundisha sio kwa kumkomoa, unakuta mtoto anakuogopa mzazi kutokana ukali uliopitiliza mpaka vitu vya msingi anashindwa kukueleza.

Kuna haja kwa baadhi ya wazazi wapewe Elimu kliniki jinsi ya kutumia lugha nzuri kwa watoto wao ndio maana wanasemaga wababa muwasindikize wake zenu kliniki ili mjue jinsi ya kuongea na watoto wenu hamtaki ndio maana mtoto akikosea unatukana tu tusi lolote litakalokujia iwe la nguoni unaona sawa.

Tujifunze lugha za kutumia mbele za watoto wadogo, maana wapo kwenye hatua za kujifunza katika ukuaji wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusi ndio kiboko cha baba kwa mtoto, akizingua anatandikwa kofi

Toka akiwa mdogo inabidi ajue gharama za maisha kama wimbo wa taifa_hatutaki mahanisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom