Mzazi kuuza mali kwa mtoto moja kati ya watoto wake

Msandawe Halisi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
647
350
Hii imekaaje wakuu.
Mfano huu hapa katika famili hii.
Baba ana watoto 6, mama katangulia mbele ya haki. Baba maisha yake yanamwendea mrama sana kimapato. Katika watoto 6 wa kwanza ni Dr.
Baba amejenga nyumba ambayo anaishi na watoto wake 2 ambao awajaanza kujitegemea.kwa bahati nzuri katika hiyo nyumba kuna sehemu ya uwanja umebaki ambao anaweza kujenga nyumba nyingine ili apangishe kuongeza kipato cha familia.
Baba uwezo wa kujenga haupo tena, ila mtoto wake fisrt born Dr, ana uwezo wa kujenga kutokana na kipato chake kuwa vyema.

First born Dr, amemwambia Baba yake yupo tayari kujenga. Sharti amuuzie kwanza huo uwanja.
Je magreater thinker, hii imeekaaje.
Je ni vyema mzazi kumuuzia uwanja au kitu chochote mtoto mmoja kati ya watoto wake.
 
Mtoto ana haki ya kununua chochote kutoka kwa baba, na baba pia ana haki ya kuuza chochote kwa mtoto, hayo ni makubaliano ya wahusika. Ila mzazi anapaswa kuifahamisha familia yake juu ya uamuzi huo ili watoto wengine wasinung'unike.
 
Je! Inakuaje Mzazi kumuuzia mtoto ambaye alimtengenezea mazingira mazuri ya mafanikio yake ya kimaisha. Kumpatia elimu nzuri tofauti na wengine ambao awajapata fursa hiyo kutokona na mabadiliko ya kipato cha mzazi. Je ni uungwana mtoto kununua sehemu ya familia ili hali alitakiwa ajenge kumsaidia mzazi wake na mali iwe ya familia.
 
Hapo kuna mambo mengi yanaingia kati, huyo mtoto wa kwanza i.e Dr anahitaji ajijenge yeye na familia yake (kama anayo ama aitarajiayo) so anaogopa kujenga katika kiwanja cha baba yake sababu binadamu hatuaminiki, anahofia leo na kesho baba yake anaweza fariki kukaibuka tafrani kuhusu nyumba aliyoijenga yeye kwa jasho lake na nyumba hiyo kujumlishwa kwenye urithi wa baba na hivyo kugawana pasu kwa pasu na hata kama atashinda kwa kuwashawishi nduguze basi kukabaki na kisasi baina yake na wao.

Na pia kama alivyosema mdau hapo juu, baba ana haki ya kuuza na mtoto ana haki ya kununua, ila itakuwa busara zaidi kama baba ataita wanawe wote na kuwaambia uamuzi huo wa yeye kuuza ili baadae pasije kutokea ugomvi baina ya watoto pale baba atakapofariki. So kwangu mini sioni tatizo juu ya hoja yako.
 
Je! Inakuaje Mzazi kumuuzia mtoto ambaye alimtengenezea mazingira mazuri ya mafanikio yake ya kimaisha. Kumpatia elimu nzuri tofauti na wengine ambao awajapata fursa hiyo kutokona na mabadiliko ya kipato cha mzazi. Je ni uungwana mtoto kununua sehemu ya familia ili hali alitakiwa ajenge kumsaidia mzazi wake na mali iwe ya familia.

Alimtengenezea mazingira mazuri kivipi.? Hao watoto wengine hawakutengenezewa mazingira mazuri kivipi.? Je huyo mtoto wa kwanza alikuwa akifeli na yeye baba akawa anatumia pesa kumsomesha.? Je hao wengine hawakupata kwenda shule kabisa kutokana na baba kupungukiwa kipato.? Je alimpatia mtoto wa kwanza mtaji. Fafanua hili kwanza ndio mada iendelee.
 
Ubinafsi unakujaje.?
Yeye kapata fursa ya kufaidi jasho la baba yake wakati akiwa katika hali nzuri. Hawa wachini pia wanaitaji fursa kama aliyeipata kaka yao. Wanapenda waende shule ila uwezo aupo.
 
Yeye kapata fursa ya kufaidi jasho la baba yake wakati akiwa katika hali nzuri. Hawa wachini pia wanaitaji fursa kama aliyeipata kaka yao. Wanapenda waende shule ila uwezo aupo.

Mleta mada angekuja kuelezea kisa chote kilivyokuwa hapo mwanzo. Isije ikawa ni nguvu zake mwenyewe leo hii ikasemekana baba ndiye aliyembeba mwanawe wa kwanza. Lazima tujaribu kuwa fair kwa pande zote.
 
Back
Top Bottom