Mzazi kumzuia mtoto wake kumuoa/kuolewa na mtu fukara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzazi kumzuia mtoto wake kumuoa/kuolewa na mtu fukara

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by donlucchese, Apr 2, 2011.

 1. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,349
  Likes Received: 3,478
  Trophy Points: 280
  Nilikua naangalia muvi ya kihindi iitwayo 'Khabi Kush Khabi Gham' ambayo kwa wale walioiona ni yakuteka hisia. Kwa kifupi inahusu kijana ambaye ni mtoto wa tajiri mkubwa lakini akatokea kuzimika kimapenz kwa mtoto wa maskini ambaye mama wa binti huyo ni mfanyakazi kwenye kasri la baba yake na huyo kijana. Kitendo hiki kilimkera mzee wake na kijana hata kupelekea kumfukuza kijana wake huyo ili asitie aibu familia. Sasa inakuaje kwa mzaz kuingilia penz la mwanaye? Na je,unaweza pata laana kwenda against na mzaz wako kwa kitendo cha kufuata moyo wako? Mapenz sidhan kama yanaangalia vigezo ivi,japo ashakum c matusi hawa watanzania wenzetu wenye asili ya kiarabu ni mwiko kuolewa na mtu wa nje ya race yako(mweus) au mtu maskin. We unaonaje? Unaweza kwenda against na mzaz wako 4the sake of yo own happiness?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Wazazi wanaweza kabisa kuwa washauri wa mtoto wao inapokuja kwenye maamuzi ya kuoa au kuolewa lakini ni lazima wamuache mtoto wao afanye maamuzi mwenyewe bila kumuingilia katika uhuru wake wa kuchagua ni yupi ambaye angependa kumuoa au kuolewa naye bila kujali vigezo vya wazazi kama vile dini, kipato n.k.

  Inapendeza sana kama ndoa inakuwa na mafanikio pale mtoto anapoamua kufanya maamuzi tofauti na wazazi wake na kuamua kuolewa/kumuoa yule anayemtaka yeye na siyo yule ambaye Wazazi wake wanamtaka na mara nyingi ndoa hizi huwa zina mafanikio makubwa sana maana wanandoa hujituma zaidi ndani ya ndoa yao ili kuwaonyesha Wazazi walioweka pingamizi kwamba uamuzi wa wanandoa haukuwa na makosa.

  YouTube - Tinie Tempah - Written In The Stars ft. Eric Turner
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Moooooods!
  Tunaomba jukwaa la movies.
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Hayo mambo kama yamepitwa na wakati vile Wazazi na mapenzi yenu wapi na wapi??
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,257
  Trophy Points: 280
  Hapa kinachosababisha ni matarajio kwa mtoto!!!au kusema mtoto wangu akaolewe mahali ambapo hatapatashida au kumwokoa kwenda ktk famili fukara!!! hivyo kufanya hivyo nimakosa mimi narafiki yangu alikuwa na mpenzi wake lakini katoka ktk famili tajiri rafiki yangu famili yakawaida,lakini uwezi kuamini upande wa msichana walikataa kuja ktk harusi na mtoto akawambia naolewa na huyu huyu!!Kwa hapa Tanzania tabia hii wanayo Wachga,Wahaya!
   
 6. donlucchese

  donlucchese JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 9,349
  Likes Received: 3,478
  Trophy Points: 280
  asante sana mkuu kwa mchango wako
   
 7. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Sometimes naungana na wazazi wa aina hiyo, Kijana tafuta pesa sio kujipaka ma 'calorite' halafu hunakitu kinachofuata ni kutesa watoto wa watu.. Mwanaume tafuta hela kwanza :disapointed:
   
 8. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huo ni ukoloni.
   
 9. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mapenzi ni ya wawili wapendanao,inakuwaje mzazi anaingilia mapenzi ya mwanawe? mimi naona mzazi wangu akiniingilia kwenye sekta hiyo hatutaelewana. sababu at the end of the day ni mm ndie nitakaeishi na huyo mtu
   
Loading...