Mzazi kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Mzazi mwenye uwezo kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu? Na kumnyima napo ndio kumjenga?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, nilipokuwa form one mnamo mwaka 2000 katika shule moja ya secondary tulipata kupewa T-shirts flani hivi rangi ya dark blue ambazo tulikuwa tunavaa siku ya Ijumaa kama sare ya shule kwa maana siku ile (Ijumaa) ilipangwa kuwa ndio siku ya michezo kwa wanafunzi. Hivyo ikifika saa 6 mchana tu baaaaas masomo yote husitishwa na wanafunzi wote huenda viwanjani kwa ajili ya michezo huku ndugu zetu waislamu wakielekea misikitini (Masjid) kwa ajili ya swala ya Ijumaa.

Sasa bwana ile t-shirt yangu nilikomaa nayo miaka mitatu. Yaaani form one yote ninayo, form two bado ninadunda nayo mpaka form three hiyo mwaka 2002 ngoma ninakomaa nayo ingawa akawa imepauka sana kwa maana wanadai zilikuwa zimetengenezwa kwa cheap cotton hivyo zilikuwa zinatoa rangi wakati wa kufua.

Ilipofika mwezi wa sita, baada ya kufungua likizo ndefu, basi toleo jipya la t-shirt likatolewa, t-shirt nzuri hiiiiizooo, dark blue flani hivi zinavutika vutika mkikaa pale assembling point basi zinang'aaaaa mpaka raha.

Karibia nusu ya rafiki zangu wengi walizinunua t-shirts zile mpaka wasichana. Nikawa ninajisikia inferior sana mbele za wenzangu.

Baada ya kuona vile, mimi niliporudi home tu nikasubiri jioni muda wa kula nikamwambia mama yangu kwa maana shida nyingi huwa ninaongea na mama na sio baba. Mama akalifikisha lile suala kwa mzee baba. Aisee mzee baba aliwaka sio mchezo. Mzee alikuwa anasema "mama Hassan (hilo Hassan ni jina la uongo) hawa watoto ukiwaendekeza kuwapa chochote wanachokitaka utawaharibu hawa, tukifa watashindwa kuishi kwa ndugu" ingawa ilipofika mwisho wa mwezi mama alipewa pesa na baba kisha akanipa mimi nikaenda nunua t-shirt mpyaaaa na mimi nionekane msafi mbele ya mademu wa form 3.

Wazazi mlipo humu Jamiiforums eti ni kweli kumpa mtoto kile anachokitaka ni kumharibu? Na kumyima napo ndio kumjenga?

Ninakaribisha maoni yenu.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mi nadhani si kweli sana japo inategemea anataka nini mtoto na kwa wakati gani.

Mfano suala lako...umekaa na tisheti miaka 3 mzazi anadai unaharibiwa? Wakati wapo wazazi walikuwa wakinunua sare kila muhula mtoto anarudi na sare mpya na mabegi. Au wengine kila mwaka watoto hununuliwa sare mpya.

Mi mwanangu wa miaka 4 Nampa kila analotaka...akitaka kwasasa...alikataa ugali anataka wali nampa, akikataa wali anataka chipsi Nampa, akikataa juisi akataka soda nampa.

Maisha yenyewe mafupi haya....nikifa atazoea tu maisha magumu

Maisha magumu hayana experience.

Wapo watu wametoka maisha ya chini lakini wanapenda maisha ya juu, wapo watu wamedekezwa lakini wameishi poa tu kwenye maisha magumu.
 
From my own experiance sidhani kama ningelikua hivi nilivyo leo kama Wazazi wangu wangenipatia kila nilichokitaka back then wakati nasoma Primary, O na A-Level hence naunga mkono hoja, kumpa mtoto kila anachotaka ni kumharibu

Nadhan mtoto anatakiwa kupewa kile ambacho ni lazima kwa yeye kukamilisha maisha fulani (kama ni mwanafunzi daftari, uniform vitabu etc) the rest ni option ya mzazi kama ataamua kumpa au lah.
Kwa mleta uzi, hiyo T-shirt mpya hailuwa muhimu saana as long as haikuchanika. Naamin ulijifunza kitu kutokana na hatua ya Baba yako

Nawasilisha
 
Marahaba last born!
Kupewa mahitaji ya muhimu siyo kumuharibu..
Mfano ungenunuliwa tsheti Jan bora tu wenzako wamenunuliwa mpya June nawewe ukataka huko ni kukuharibu..

Umenielewa dogo!?

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Haswaa, mtoto anatakiwa ajue tangu akiwa mdogo kuwa si kila anachokitaka atakipata. Umenikumbusha ninapoingia form two zilikuja t-shirt nzuri sana, kwa sababu sister alikuwa amepanga kunihamisha kwenye ile shule alikataa katakata kuninunulia. Matokeo yake mwaka mzima nilisomea tshirt chakavu nilikuwa najisikia vibaya sana ikawa ni mimi na sweta mwanzo mwisho
 
Kulea mtoto ni falsafa ya mtu na kila mtu anastyle yake. Wengine sisi wazazi wetu walijali vitu 3 tu.ule tena mlo wenyewe lazma mhakikishe mumeosotea mfano maziwa lazma ukachunge ng'ombe ndy ukamue unywe!
Yaani hakuna kitu tulikipata Bila kuchangia nguvu kazi. Mzee alikua matata sana..alikua na wake 5 na watoto 38. Hakuna mtoto legelege pale nyumbani .tumekua kijeshi mambo ya kulialia eti Sina kiAtu sjui nguo nini haikuepo hii..kama huna kalime vibarua upate hela ukanunue viatu. Dah yule Mzee akikusaidia sana nguo ikichanika matakoni atashona kwny cherehani yake ila kwa kukufundisha siku nyingne ushone mwenyewe!!Mzee alikua matata hatar..
Watoto wote hakuna legelege na wengi wametoboa!!
Tuna miaka 18 Mzee alifarki lakini mama zetu wanamkumbuka Mzee alovyokua shupavu..na kila tukienda home wanasema Mzee wetu alikua mwanaume mfano!!
Lea watoto ukiwandaa juu ya kesho yao. Usidhani kumpa kila kitu ni kumpenda Bali ni kumnyima ujasir na ubunifu wa maisha yake ukiwa haupo!!
Teach and treat your children to be independent in time your mouth is shut off!!wakati ni sasa si kesho!!
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Mzazi mwenye uwezo kumpa mtoto chochote anachokitaka ni sawa na kumharibu? Na kumnyima napo ndio kumjenga?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, nilipokuwa form one mnamo mwaka 2000 katika shule moja ya secondary tulipata kupewa T-shirts flani hivi rangi ya dark blue ambazo tulikuwa tunavaa siku ya Ijumaa kama sare ya shule kwa maana siku ile (Ijumaa) ilipangwa kuwa ndio siku ya michezo kwa wanafunzi. Hivyo ikifika saa 6 mchana tu baaaaas masomo yote husitishwa na wanafunzi wote huenda viwanjani kwa ajili ya michezo huku ndugu zetu waislamu wakielekea misikitini (Masjid) kwa ajili ya swala ya Ijumaa.

Sasa bwana ile t-shirt yangu nilikomaa nayo miaka mitatu. Yaaani form one yote ninayo, form two bado ninadunda nayo mpaka form three hiyo mwaka 2002 ngoma ninakomaa nayo ingawa akawa imepauka sana kwa maana wanadai zilikuwa zimetengenezwa kwa cheap cotton hivyo zilikuwa zinatoa rangi wakati wa kufua.

Ilipofika mwezi wa sita, baada ya kufungua likizo ndefu, basi toleo jipya la t-shirt likatolewa, t-shirt nzuri hiiiiizooo, dark blue flani hivi zinavutika vutika mkikaa pale assembling point basi zinang'aaaaa mpaka raha.

Karibia nusu ya rafiki zangu wengi walizinunua t-shirts zile mpaka wasichana. Nikawa ninajisikia inferior sana mbele za wenzangu.

Baada ya kuona vile, mimi niliporudi home tu nikasubiri jioni muda wa kula nikamwambia mama yangu kwa maana shida nyingi huwa ninaongea na mama na sio baba. Mama akalifikisha lile suala kwa mzee baba. Aisee mzee baba aliwaka sio mchezo. Mzee alikuwa anasema "mama Hassan (hilo Hassan ni jina la uongo) hawa watoto ukiwaendekeza kuwapa chochote wanachokitaka utawaharibu hawa, tukifa watashindwa kuishi kwa ndugu" ingawa ilipofika mwisho wa mwezi mama alipewa pesa na baba kisha akanipa mimi nikaenda nunua t-shirt mpyaaaa na mimi nionekane msafi mbele ya mademu wa form 3.

Wazazi mlipo humu Jamiiforums eti ni kweli kumpa mtoto kile anachokitaka ni kumharibu? Na kumyima napo ndio kumjenga?

Ninakaribisha maoni yenu.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hapo uliposema ukapata t shirt ukaonekana msafi mbele ya mademu wa form 3...

Hapo mwanangu unaonyesha unapenda sana chini, ila nakukanya kama mzazi shule na mambo ya mademu ni vitu viwili tofauti.
 
Haswaa, mtoto anatakiwa ajue tangu akiwa mdogo kuwa si kila anachokitaka atakipata. Umenikumbusha ninapoingia form two zilikuja t-shirt nzuri sana, kwa sababu sister alikuwa amepanga kunihamisha kwenye ile shule alikataa katakata kuninunulia. Matokeo yake mwaka mzima nilisomea tshirt chakavu nilikuwa najisikia vibaya sana ikawa ni mimi na sweta mwanzo mwisho

Kwahiyo unaona ungenunuliwa angekuharibu?

Daaaaaa
 
Back
Top Bottom