Mzazi kuaanza kukutegemea wewe kwa kila kitu bila kujali mshahara wako mdogo

Tuwasamehe wazazi wetu kulingana na background yao, ni jukumu letu sasa kuhakikisha tunaweka asset tusije kuwa tegemezi kwa watoto uzeeni..Jamii yetu sasa ndio ilete mabadiriko ili tuondoe hii dhana..
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng

kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza

mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza

hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote

jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz
Umenikumbusha nilipopata kazi tu mshahara wa kwanza nimejipanga naenda kulipia kwa fundi kitanda sababu nilikuwa nimeweka oda na nyingine nilipie kodi. Mzee wangu akiniomba nimsaidie. Ikabidi nimueleze tu ukweli.

Baada ya kama miezi sita nikaanza kuwaboreshea makazi pamoja na kuwawekea umeme ambapo ila mwaka uliofuata nikaamua kutoa majukumu yakaongezeka.

Pamoja na majukumu kuongezeka najitahidi kusapoti upande wa shule wadogo zangu 4, 2 wakike naishi nao 1 fomu 1 mwingine la 7, 2 wakiume 1 anamaliza fomu six mwezi wa 5 mwaka huu mwingine yuko fomu 3 nimempangishia yuko shule za kata hawa nawasapoti kuanzia mavazi matumizi hadi Ada bado nasaidia gharama za kuhudumia shamba ninapokuwa na unafuu lakini baba anapoomba nimsaidie nikakutwa sina kwa wakati huo analalamika sana. Maneno anayoyasema kwa watu Mmh! Unaweza kupata tamaa.

Kwa hiyo bwana wazoee tu.
 
Haya yote tu ni kwa sababu ya umaskini, ukiangalia katika familia zenye kipato kizuri Hakuna mzazi anayehitaji Masada wa kifedha kutoka kwa mwanae na hata ukiangalia familia za kizungu wao ndo wapo tofauti kabsa unakuta kijaana wa kizungu kasomeshwa kapata kazi ameoa ana mshahara Mzuri lakini bado anapata financial support kutoka kwa mzazi wake kwahyo haya yote ni mawazo ya kimaskini tu wala hamna jipya kikubwa ukipata usisahau utokako ishi na wazaz wako vizur
 
Uislam haukuwahi kumtweza mtu nguvu, kumlazimisha kufanya jambo nje ya uwezo wake.

Hili la kuhudumia wazee ni jukumu la wajibu lakini linakwenda sambamba na uwezo wa huyo mtoto, sio wewe unakula kuku wao mlenda wale mlenda tu ikiwa wanapenda kufanya hivi.

Ila la muhimu hakikisha unayafanya majukumu haya ya kuwatunza wazazi kwa uwezo wako wote(to the maximum) kwani hii ndio maana halisi ya ihsani na allah atakulipa ujira mkubwa sana hapa duniani na kesho akhera.

Na uyafanye haya juu ya wazazi wako bila malalamiko, sijui mama hivi sijui baba hivi. Fanya bila ya kulalama na ujione fahari kuwahudumia wazee wako wakati wako hai.

Mtume wa allah asema"amepata hasara, amepata hasara, amepata hasara/pua yake imegusa mchanga(ameangukia pua) yule ambaye ataishi na wazazi wake kisha wazaza wake wakafika uzee na kufa na isiwe sababu ya yeye kupata pepo"kwa ihsani hii kwa wazazi.

Kumbuka:
Mali ulizonazo ni za wazazi wako pia
Kuna swahaba aliwahi kwenda kumshtakia mzee wake kwa mtume kuwa "baba yangu amekuja nyumbani kwangu amechukua hiki na kile bila ruhusa yangu, nifanyaje??"
Mtume wa allah akajibu "anta wamaluka liabika" (wewe na mali zako ni za baba ako)
Hasante sana ninaomba kujua hukumu kwa mzazi mwenye uwezo wa kufanya kazi lakini akawa hapendi kufanya kazi eti kwa sababu mtoto wake ana kazi?
Swali lingine ni kuhusu mimi, wazazi wangu wanajiweza kwa kiasi fulani kwa hiyo huwa hawahitaji msaada wowote kutoka kwangu nifanye kitu gani kwa wazazi ili kuwatendea hisani?
 
1.Kibongobongo huwezi kukwepa kuwasaidia wazazi
2.Ishi mbali na wazazi ila hakikisha mawasiliano yanakuwepo muda wote
3. Weka kiasi maalumu na muda(fixed amount and time) wa kuwatumia hicho kiasi kila baada ya muda flani.
4. Punguza Starehe

Naomba kuwasilisha
 
Kwangu mimi kuhusu wazazi hainipi shida sababu najuwa qalinipigania sana kufika hapa nilipo.

Huwa nakumbuka mama yangu nikiwa shule alikuwa akiuza maziwa, barafu, mkaa kuna muda pesa yote nabeba mimi na sikuwa na huruma kipindi kile ila sasahivi najuwa tabu alizokuwa anazipata.

Hivyo nimejiwekea jukumu la kuwatunza kila ninapopata mshahara wangu tena kabla hawajaniomba na wameshalizoea hilo hivyo nikikwama wao wanakuwa wananiombea dua ili nipate nao niwatumie, japo ni kiasi kidogo ila ni bora naamini inawaokoa.

Tatizo langu mimi lipo kwa ndugu watoto wa baba zangu wakubwa, wadogo... shangazi, mjomba, kaka, dada marafiki tuliosoma nao tena wamekaa nyumbani wakisubiri ajira hawa ndiyo simu zao, sms zao huwa zinafanya nijisikie vibaya sababu nikisaidia huyu na yule anaomba labda huwa wanaambizana.
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng

kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza

mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza

hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote

jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz
Wazazi wawili wanalea watoto.6! Watoto sita wanashindwa kulea wazazi wawili!
 
Wazazi wawili wanalea watoto.6! Watoto sita wanashindwa kulea wazazi wawili!
Kumbuka hapo anakaa na watoto zake wote. Wanakula pamoja wanalala nyumba 1. Even me nina uwezo wa kulea wazazi wangu kwa kama mm walivyonilea nikiishi nao sehemu moja. Mjini nimepanga najitegemea kodi,umeme,maji, chakula, nalipa dada wa kazi, nalipa ada kwa kijana wangu. Na mzazi aliokuwepo kijijini naye anataka nimpatie pesa ya kula, umeme, nilipe bill za maji, pesa ya kuandaa shamba,pesa ya kununua mbegu na mbolea, pesa ya kuvuna, akiumwa malaria nimtumie pesa aende hospital, akifiwa na ndugu yake nimtumie pesa ya nauli.
My dear ni rahisi kwa nyie wenye mishahara yenye unafuu kidogo lakini kwa sisi ambao kipato chetu cha kati ni ngumu kuhudumia familia mbili.
 
Duuh wengine ni mmekua maisha ya kibinafsi mno mpaka unawaza kumuhudumia mzazi wako unaleta uzi humu daa umasikini ni ugonjwa mbaya sana sasa hapo jamaa ako au ndugu yako yeyote utaweza kumsaidia kweli wakati haya maisha tumeumbwa kwa kutegemeana...uzi za hovyo nilizowahi kusoma humu na hii mojawapo..
 
Mzazi kuzaa ni mipango yako hivyo ni jukumu lako kujilea na kumlea mtoto wako. Tatizo tumejiwekea kuwa tunawalea watoto wetu ili nao waje watulee, sio lazima ni fadhila tu. Hivyo inatakiwa uwasaidie kwa kiasi chako ili nawe uweze kujijenga kwaajili ya watoto wako lasivyo tutaendelea kutengeneza chain ya umasikini milele.
 
Wazazi wa ki Afrika ni changamoto kwa kweli, wao wanafikiri ukisoma ukawa na kazi basi ule mshahara wako ni kwa ajili ya matumizi yao kwa kuwa wametuzaa. Nilipata tabu sana na mzazi wangu, nilitumia njia nyingi za kistaarabu kumuonyesha kuwa nina kipato kidogo kisichokidhi hata mahitaji yangu kwa hyo apokee tu hicho ninachompa na ajitahidi kukitumia kwa utaratibu mzuri. Hakunielewa na akawa analeta ukali. Aisee nilichokuja kumfanya sitasimulia ila aliishia kupata ugonjwa wa moyo na amerudi kwenye mstari. Akipewa kilichopo anashukuru na wala haleti zile lawama zake za kutoridhika. Nilijitahidi kuwa muungwana hakutaka kunielewa. Nilipomuumiza alinielewa. Si vyema kumuumiza mzazi lakini sikuwa na alternative nyingnie ya kumuonyesha kuwa madai yake yamenilemea zaidi ya ku inflict pain. Baada ya kumuumiza kwa sasa kaacha na akipewa kilichopo anashukuru na kukitumia vizuri. Sikushauri utumie mbinu yangu. Mimi niliitumia baada ya kutumia njia ya kistaarabu na kiungwana kushindikana.
na ww utakuwa mzaz either tayar ni mzaz subil ufikie level ile ya wtt wako kuwa wamepata kaz,na ukute ulitumia ngv nying kuwasomesha,mali na vyote ulivyokuwa navyo uliwapeleka shule,, wamepata kaz mda huo ww ushazeeka!,,45+yrs utakikumbuka hiki ulichokiandika hapa acha kabisa hilo jambo ni swala la kumushukuru mola tu!,kikubwa ni bajet zako ujuwe namna ya kuzicontral,s kila wakat watakuomba hapana kuna wakat utakaohitajika ww kufanya hivyo,,hasa kabisa mbo hili linategemeana sana na umri wa wazaz wako....
NB; usijaribu kumnanga mzaz hata siku moja et kisa amekuomba hela au kumusaidia,,musaidie kadri ya uwezo wako ulipofikia kwa level inayokuruhusu mkuu
 
Kama hawajiwezi ni jukumu letu kuwatunza! Lakini kama bado wana nguvu ya kufanyakazi,ni vyema ukaendelea na majukumu yako.Unachotakiwa ni kuwasupport mfano kama wana nguvu ya kulima,kuwapa fedha ya kununulia mbegu,kuandaa mashamba,nk au kuwapelelekea zawadi.Lakini siyo kila kitu wanabweteka wanakaa maadamu wanajua mtoto ana kazi wanataka kila kitu,hapana!
Hayo ni mawazo yangu!
 
Back
Top Bottom