Mzazi kuaanza kukutegemea wewe kwa kila kitu bila kujali mshahara wako mdogo

Ni wajibu wa lazima kwa mzazi kumhudumia mtoto.

Ila siyo jukumu kisheria kwa mtoto kumhudumia mzazi.

Mtoto anawajibika kimila tu kwa mzazi katika kumsaidia ila siyo kisheria.

Mzazi hawezi kumshitaki mtoto kwa kutokumhudumia.

Hii ni changamoto sana kwa vijana, bado kuna wazazi wana fikra za kijima kwamba wamezaa ili wapate wa kuwahudumia kila kitu.

Yaani, umlipie bill ya umeme, chakula , pombe, mavazi, vocha, na malazi.

Yaani, unabeba jukumu, hili siyo sawa.

Kuna kumsaidia mzazi pale hali ikiruhusu ila kuna wengine wanataka wakupruni kila kitu yaani kwa mwezi unatuma hata laki mbili mfano, wakati unalipwa laki tano.
Namzazi akijua umepata kazi ukimwambia sina Pesa hakuelewi kelele zinaanza anisaidii atakua ana honga Sana'a huyu mjini kuna mchanganya
 
Kwanza shukuru kuwa wazazi wako wapo hai mpaka sasa. Wapo wanaotamani wazazi wao wangekuwa hai....haijalishi hali zao za kiuchumi!

Kulea wazazi sio wajibu wa kisheria kama kulea watoto. Lakini ni "wajibu" wa kijamii (kiafrika) na hata kidini. Kuna mtu aliwahi kunambia kuhusu levels za baraka...nitataja mbili za mwanzo kwa umuhimu.
1. Baraka kutoka kwa Mungu.
2. Baraka kutoka kwa wazazi wako ambao kupitia kwao Mungu alichagua kukuleta wewe duniani kwa makusudi maalumu. Kuna baraka kubwa sana katika kuishi vema na wazazi wako ikiwemo kuwasaidia kwa kadri uwezavyo. Mzazi wako akikunenea mema ni bara ka kubwa sana. Vivyo hivyo, mzazi wako akikunenea mabaya au kukosa radhi ya mzazi wako ni laana.

Kuna mambo huwa yasikitisha sana (hasa sisi wanaume kwenye kauwezo kidogo). Baadhi yetu tunaona rahisi kuhonga, lakini vigumu kumsaidia wazazi wetu. Ndio kama hivi, mzazi anaomba tuhela kidogo twa chakula, tunakuja kumnanga huku JF.

Ni kweli in muhimu kujiandaa maisha ya uzeeni, lakini unapokuwa na resources chache unaona ni bora usomeshe na kuendeleza watoto kwanza ili waweze kujitegemea na pengine kuja kukusaidia ("social insurance"). Hili haliwezi kuwa jambo baya.
 
Kwa Tz(Africa yetu)
Ni bora kufanya biashara hutotegemew na ndugu au wazazi kulko uajiriwe/sekta binafsi au serikali Ni balaa
Ushauri
Wachane live unapokea Tshs ngapi
 
Mwinge analipwa laki tatu wazazi wanataka kila mwezi laki baado matumizi madogo mado pi we we mwenyew una majukumu yako we we kama we we daah! Ulipe kod ya nyumba umeme maji ule uvae ujenge ujiajili watkiwa kutafuta mtaji haphapo kwenye lakitatu upande daradara kilasiku mmh! Tunafika kweli

Kazi sana
 
Ni wajibu wa lazima kwa mzazi kumhudumia mtoto.

Ila siyo jukumu kisheria kwa mtoto kumhudumia mzazi.

Mtoto anawajibika kimila tu kwa mzazi katika kumsaidia ila siyo kisheria.

Mzazi hawezi kumshitaki mtoto kwa kutokumhudumia.

Hii ni changamoto sana kwa vijana, bado kuna wazazi wana fikra za kijima kwamba wamezaa ili wapate wa kuwahudumia kila kitu.

Yaani, umlipie bill ya umeme, chakula , pombe, mavazi, vocha, na malazi.

Yaani, unabeba jukumu, hili siyo sawa.

Kuna kumsaidia mzazi pale hali ikiruhusu ila kuna wengine wanataka wakupruni kila kitu yaani kwa mwezi unatuma hata laki mbili mfano, wakati unalipwa laki tano.
Ni wajibu wa lazima pia mtoto kumhudumia mzazi.

Wewe unataja eti sio wajibu wa kisheria hiyo sheria unayosema ni ya nani??
 
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, zote kwa pamoja zinatamka kwamba wazazi wana wajibu wa kuwapa watoto mahitaji yao na ni lazima.

Ila sheria hizo na nyingine, hazisemi kwamba mtoto anawajibika kumhudumia mzazi.

Ulishasikia wapi mtoto kawajibishwa kwa kushindwa kuwahudumia wazazi?

Lakini itakuwa umewahi kusikia wazazi wakiwajibishwa kwa kushindwa kuwahudumia watoto, na pia mwanaume kushindwa kumhudumia familia.

Iko hivi, mzazi akishamaliza kazi ya malezi inatosha.

Na hata kule Moshi huwa mtoto akimaliza shule anaambiwa aende zake akatafute na hana chake tena.
 
Na mimi nakwambia kwa mujibu wa sheria ya dini yangu kumtunza mzazi ni jukumu la lazima kwa mtoto na sio hiyari.
 
Sasa sheria ya dini haiwezi kuipiku sheria ya nchi.

Sheria ya dini inatakiwa ifuate sheria ya nchi.

Taasisi za dini zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kama sheria ya dini inasema kuwa ni lazima, huku ya nchi ikikataa, basi sheria ya nchi ndiyo inazingatiwa.

Hiyo ndiyo tafsiri sahihi
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng

kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza

mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza

hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote

jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz

Duh Unatafuta laana sasa
 
Hivi bwana mkubwa hapa tunazungumzia ishu kwa mujibu wa sheria za nchi??

Mleta mada hajazungumza kwa mlengo wa kisheria.

Kama wewe unatumia sheria ya nchi inayotungwa na akina msukuma, kibajaji and the like sawa wewe endelea.

Mimi natumia sheria ya dini kwa kuwa ndio sheria kuu juu ya mwanadamu.

Kukumbusha tu sheria za akina kibajajaji haziwezi kuwa juu ya sheria ya mola muumba hata siku moja.
 
Laiti kama ungejua faida za kuwahudumia wazazi usingesema ivyo kabisa bora wewe unafanya kazi, kuna watu wanahudumia wazazi bila hata yakua na kipato cha uhakika
Mzazi kumhudumia mtoto ni jukumu lake lakino sio jukumu la mtoto kumhudumia mzazi, ndio maana wazazi waliotengeneza mazingira na wakajiandaa hawawasumbui watoto kuomba omba hela kila wkt
 
Nieleweke sijaja kulala mika nime post ili tushauliane wadau
Samweli, uzuri wa wazazi wetu wengi wa Kiafrika ni Waelewa. Ninaamini kuwa ukikaa nao na ukawaeleza kuhusu hali yako watakuelewa na ninaamini kuwa mtafika mahali mtapata muafaka tu...
 
Amaaaaa kweli
Nimeamini, baba mmoja asiye na kazi anaweza kulea watoto 10 na wakaishi kwa kumtegemea kwa kila kitu. Lakini watoto 10 wenye kazi wanaweza kushindwa kumlea baba mmoja.
 
Ni wajibu wa lazima kwa mzazi kumhudumia mtoto.

Ila siyo jukumu kisheria kwa mtoto kumhudumia mzazi.

Mtoto anawajibika kimila tu kwa mzazi katika kumsaidia ila siyo kisheria.

Mzazi hawezi kumshitaki mtoto kwa kutokumhudumia.

Hii ni changamoto sana kwa vijana, bado kuna wazazi wana fikra za kijima kwamba wamezaa ili wapate wa kuwahudumia kila kitu.

Yaani, umlipie bill ya umeme, chakula , pombe, mavazi, vocha, na malazi.

Yaani, unabeba jukumu, hili siyo sawa.

Kuna kumsaidia mzazi pale hali ikiruhusu ila kuna wengine wanataka wakupruni kila kitu yaani kwa mwezi unatuma hata laki mbili mfano, wakati unalipwa laki tano.
Kweli mkuu. Alikuwa wali anaula siku ya Eid na Krismas tu sasa kwa kuwa mwanawe umepata kijikazi anataka ale wali kila jumamosi, kama sio kila siku!
Wapo wengi tu wazazi wa namna hii wa kuona mwanae kupata kazi ni mwisho wa matatizo yake ya Uzeeni....
 
Mmmmm, Eclat, hebu twende tena hapo taratibu... Kumsaidia/kumtuna mzazi ni fadhila, kwamba una hiyari ya kufanya hivyo ama la, na sio Jukumu lako, kwamba unalazimika kufanya hivyo??
Tunajukumu la kuwatunza na kuwalea watoto tuliowaleta duniani, kumsaidia mzazi ni fadhila ya malezi aliyokupa lakini si jukumu.
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng
kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza
mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza
hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote
jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz
Na wazazi wengine usipowatumia pesa wana waka kama mbogo wengine hufika mbali zaidi wakisema kama hutumi pesa basi tafuta mama mwingine ye sio mama yako tena wakati huo umefanya kazi na bos kakupiga shoka wengine wakijua upo mjini wanajua una pesa kumbe chenga ila hamna namna ni kupambana tu huwezi mtupa mzazi
 
vijana wenzangu ningependa tuweksne sawa katika hili swala ambalo lina tukuta weng

kwa mfano umepata kazi wazazi nao wanategemea sana wewe kupata kazi baada baada ya wewe kapata kazi kuna maisha yako inatakiwa uyatengeneza changamoto ina kuja hapa mzazi mzazi akishajua kwamba umeshapata kazi hapo ndipo changamoto zinaanza

mzazi anaanza kuku tegemea wew kwakila kitu bila kujali mshara wako Mdogo pia afikilii kwamba nawew unahitaji kutengeneza maisha yako kwanza

hatukatai kumsaidia mzazi nilazima lakini kuna muda unaweza jikuta kwenye maisha unakwama malengo yako yana potea bila kujua nini chanzo kumbe hata wazazi wana changia wakisha jua mwisho wamwezi umekaria sim zinaanza zakuomba Pesa unajikuta malengo ulopanga kwamba nikipokea mshahara nifanye hiki unavuruga unamtumia mzazi usipo mtumia lawama kama zote

jamani wazi mtuache kwanza makampuni yenyewe saivi wana lipa mishahara midogo pengine hata Mimi mahitaji yangu haunisholezi tushsulisne hapa Vijana wenzangu hasa sisi tunao anza maisha tuwekane sawa by Fundy_samwely_tz
Wazazi wa ki Afrika ni changamoto kwa kweli, wao wanafikiri ukisoma ukawa na kazi basi ule mshahara wako ni kwa ajili ya matumizi yao kwa kuwa wametuzaa. Nilipata tabu sana na mzazi wangu, nilitumia njia nyingi za kistaarabu kumuonyesha kuwa nina kipato kidogo kisichokidhi hata mahitaji yangu kwa hyo apokee tu hicho ninachompa na ajitahidi kukitumia kwa utaratibu mzuri. Hakunielewa na akawa analeta ukali. Aisee nilichokuja kumfanya sitasimulia ila aliishia kupata ugonjwa wa moyo na amerudi kwenye mstari. Akipewa kilichopo anashukuru na wala haleti zile lawama zake za kutoridhika. Nilijitahidi kuwa muungwana hakutaka kunielewa. Nilipomuumiza alinielewa. Si vyema kumuumiza mzazi lakini sikuwa na alternative nyingnie ya kumuonyesha kuwa madai yake yamenilemea zaidi ya ku inflict pain. Baada ya kumuumiza kwa sasa kaacha na akipewa kilichopo anashukuru na kukitumia vizuri. Sikushauri utumie mbinu yangu. Mimi niliitumia baada ya kutumia njia ya kistaarabu na kiungwana kushindikana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom