Mzazi afarikia zahanati, azuiliwa kwenda Amana

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE Sabela Mganga [31] ameaga dunia katika zahanati binafsi iitwayo COH iliyopo Ukonga Mazizini jijini Dar es salaam, kwa kuishiwa damu baada ya kujifungua watoto mapacha katika zahanati hiyo.

Mwanamke huyo mara baada ya kujifungua watoto hao hali yake ilikuwa imebadilika na kuishiwa damu na daktari kumuandikia mama huyo ahamie katika hospitali ya Wilaya ya Ilala ya Amana kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo mwanamke huyo aliweza kuzuiliwa na muuguzi mmoja wa zahanati hiyo kwa kuwa mwanamke huyo alikuwa hajamalizia deni lake alilokuwa akidaiwa zahanati hapo lililofikia shilingi laki moja hamsini na tano elfu na mia nane, l55,800 kwa huduma ya kujifungulia katika zahanati hiyo.

Mwanamke huyo alifika katika zahanati hiyo Februari 5 mwaka huu na kuendelea kukaa katika zahanati hiyo hadi Februari 7 na hatimaye aliweza kufariki dunia juzi kutokana na kukabiliwa na uhaba huo wa damu aliokuwa nao baada ya kufanikiwa kujifungua watoto wake mapacha.
 
Hivi huko mjini wenzetu,serikali imeruhusu dispensary kulaza wagonjwa?....R.I.P my sister.
 
Hivi huko mjini wenzetu,serikali imeruhusu dispensary kulaza wagonjwa?....R.I.P my sister.

nimesikitika kwa kuwa alizuiliwa kwa kutokumaliza deni sasa hapo amefariki na hata hivyo hilo deni mpaka anafariki alikua hajalipa kweli maisha yamekua magumu sana!
 
Hao ndo wauuguzi tulionao kwenye hospitalini, hawajali kabisa uhai wa watu, kwao pesa iko mbele! Na utakaposhangaa zaidi ni pale hakuna atakachofanyiwa huyo muuguzi kwa kusababisha kifo cha huyo mama! Mungu awafariji wanafamilia wote!
 
Ni nani anayejali uhai wa watu hapa Tanzania siku hizi? Nchi yooote imeoza! Kila mtu anatumia uhalifu, ujambazi, uhuni na ushetani kusaka fedha!!! Kuanzia rais, wabunge, manesi..... ni ushetani ushetani tuu!!!!
 
Where is proffessional ethic and on top of that why would they offer widwifery service if they're not fully equiped with necessary stuff. Blood is very crucial in this regard, I wonder no prior arrangement were made available for emergency issue like this one.

I think its time someone should revoke their licence, simply negligence
 
Hao ndo wauuguzi tulionao kwenye hospitalini, hawajali kabisa uhai wa watu, kwao pesa iko mbele! Na utakaposhangaa zaidi ni pale hakuna atakachofanyiwa huyo muuguzi kwa kusababisha kifo cha huyo mama! Mungu awafariji wanafamilia wote!

Usimlaumu muuguzi, ni hali ya kutoaminiana tuliyoijenga wenyewe watanzania, muuguzi hayuko tayari kukatwa mshahara wake...
 
nimesikitika kwa kuwa alizuiliwa kwa kutokumaliza deni sasa hapo amefariki na hata hivyo hilo deni mpaka anafariki alikua hajalipa kweli maisha yamekua magumu sana!

Labda watazua mwili wake kuchukuliwa pia. RIP
 
Yale ya mwimbaji Mbaraka - nasikia naye alinyimwa damu kwa kukosa fedha kama sikosei. Pesa kabala ya utu!
 
masikini binadamu tumepoteza utu kabisa, masikini malaika wale sasa watalelewa na nani??? huyu muuguzu ni mnyama hana huruma hata kidogo. Mungu ailaze roho ya marehemu pema. Amina
 
usimlaumu muuguzi, ni hali ya kutoaminiana tuliyoijenga wenyewe watanzania, muuguzi hayuko tayari kukatwa mshahara wake...

hapa ni issue ya uhai wa mtu - ina maana huyo muuguzi ameshindwa hata kumsainisha mahali akadai baadaye?? Wauguzi wengine roho mbaya tu ..............yaani yuko radhi mama wa watu afe?? Na watoto si watapata shida sana??? Mauaji aliyofanya yatamfatilia for the rest of her life ............hiyo ni laana na lazima tumlaumu
 
Kweli inauzunisha sana hasa ukiangalia unyama hu umefanywa na mwanamke @$%^&*& sijui huyo nesi hajawai kuzaa hadi amfanyie mwenzie unyama huo!!? Why serikali isiifungie hiyo zahanati na hatua kali za kisheria zikachukuliwa kwa huyo nesi aliesababisha kifo cha huyo mzazi? na pia mume au familia walipwe fidia na wahusika ili iwe fundisho kwa wengine?
 
Back
Top Bottom