Mzanzibari aliyekamatwa na FBI kwa ugaidi arejeshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzanzibari aliyekamatwa na FBI kwa ugaidi arejeshwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chuma, Sep 2, 2008.

 1. C

  Chuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na Salma Said, Zanzibar

  MTANZANIA aliyekamatwa na makachero wa Marekani kwa kuhusishwa na ugaidi, Suleiman Abdallah Salim (Morris), amerudishwa Zanzibar juzi na Shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Afghanistan baada ya kubainika kwamba si gaidi.


  Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao maeneo ya Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, huku akionekana mchovu, alisema alikamatwa na makachero wa FBI nchini Somali mwaka 2003 akiwa katika shughuli zake za kibiashara na kuingizwa katika gari bila ya kufahamu anapopelekwa.


  Akielezea mkasa uliomkuta akiwa eneo la Abusasu, Mjini Mogadishu alisema baada ya kukamatwa na kuingizwa katika gari hilo huku akipata kipigo kutoka kwa maafisa

  hao alisafirishwa hadi Nairobi, Kenya na kutakiwa apeleke mtu wa kumdhamani, lakini aliwaambia kuwa yeye ni Mtanzania na kwamba hana ndugu yeyote jijini humo.


  “Waliniambia mimi ni Msomali nilikataa nikiwaambia kuwa ni Mtanzania. Kisha wakasema ni Myemen nikasema ni Mtanzania walipoona nasema Kiswahili wakaniambia mlete ndugu yako akuwekee dhamana, nikawaambia sina jamaa Nairobi mimi kwetu ni Tanzania,” alisimulia Salim.


  Alisema baadaye alirejeshwa tena Somali na kuwekwa kwenye kambi ya jeshi na kila mara alikuwa akiulizwa maswali huku akipata kipigo wakati akijibu maswali yao.


  Alisema baadhi ya maswali aliyoulizwa yalihusu kama anawafahamu Khalfan, Marwan na Fahad na kutakiwa kusema hao ni akina nani kwake na kwamba aliwajibu kuwa anawafahamu kwa kuwa ni rafiki zake wa karibu aliokuwa akifanya nao kazi ya uvuvi maeneo ya Mombasa kabla ya kwenda Somali.


  ''Wamarekani wao wanakamata watu tu, yaani wakiona mtu ana ndevu wao wanamkamata na kusema ni gaidi kama Osama, lakini mimi kila mtu ananifahamu kuwa kazi yangu ni kuvua samaki na si Muislamu wa msimamo mkali.


  Mimi si mla unga watu wananifahamu mpaka jina langu kwamba naitwa Morris, sasa huo uislamu wa msimamo mkali uko wapi?” alisema na kuhoji Salim.


  Alisema kutoka Somali alisafirishwa akiwa amefungwa pingu mikononi na miguuni hadi Afghanistan katika jela la Kimarekani liitwalo Darkness ambalo alisema mtu anapoingia humo hawezi kufahamu kama ni mchana wala usiku kutokana na giza totoro lililopo.


  ''Sisi tunaliita darkness kwa sababu huwezi kujua leo ni lini? Sasa hivi saa ngapi wala kama ni usiku au mchana ni giza tupu huoni mtu huko,'' alisema.


  Alifahamisha kuwa katika jela hiyo ambayo inatisha husikika sauti za muziki wa kutisha huku baadhi ya nyimbo za Kiswahili zikisema hakuna Mungu pamoja na sauti za baadhi ya wanyama kama mbwa, paka na simba.


  “Nyimbo za Kiswahili nilizisikia zinasema hakuna Mungu, Uislamu sio dini lakini pia kuna milio mikali ya sauti za kutisha kama mabati yanavunjwa, kengele za kanisani, sauti za mbwa anayebweka na milio ya kutisha,” alisema.


  Salim alisema baadaye alihamishiwa katika gereza lingine liitwalo Chatem bila ya kufahamu siku kwani hakuwa anafahamu kama siku imemalizika kwa sababu kulikuwa na mwanga wakati wote.


  ''Mimi sikuwa najua kama leo ni siku gani wala sikuwa na mtu wa kumuuliza ingawa kulikuwa na watu wengine, lakini hatukuwa tunaruhusiwa kuzungumza kwani wanajeshi walikuwa wametusimamia.


  Ukimuuliza mwenzako chochote unaambiwa unyanyue mikono juu kama vile Yesu anasulubiwa kwa masaa mawili bila ya kushusha na kama utashusha kwa uchovu unaambiwa anza yaani ilikuwa balaa,'' alisema huku akitokwa na machozi.


  Salim alisema baadaye alihamishiwa katika Kambi ya Jeshi iitwayo Bagram akiwa amefungwa minyororo na vioo vya macho.


  ''Nilivalishwa minyororo na vioo vya macho kama mwendesha pikipiki na walikuwa wananipa chakula kila baada ya siku mbili, wakati huo nilikuwa naumwa sana na afya yangu haikuwa nzuri. Kuna siku makachero wa FBI walinifanyia interview mara mbili nikapata asilimia mia moja,'' alisema.


  Salim ambaye vidole vyake vimevunjwa, alisema alipokamatwa aliambiwa kuwa ameiba fedha za Msomali mmoja, lakini alipopelekwa Afghanistan hakutajiwa hata siku moja kama anashtakiwa kwa kosa fulani hadi alipoachiwa na kurejeshwa nyumbani.


  Alifahamisha kuwa baada ya kukaa miaka yote hiyo, maafisa wa kimarekani walimueleza kwamba hana hatia na kama anataka kupelekwa Marekani au Uingereza kuishi huko aseme ili afanyiwe utaratibu wa kuishi huko, lakini alikataa kwa kuwa hajaonana na wazazi wake miaka mingi sana.


  “Unajua waliniambia kama unataka kuishi Marekani sema nikawaambia hapana mimi nataka kurejeshwa Tanzania. Kwanza sikuamini kama nitarejeshwa kweli kwa sababu nilikuwa

  nimeshachoka na nilikuwa tayri nimeshakata tamaa ya kuishi,” alisema kwa huzuni
  *********************************************************
  Wadau Hii imekaaje?..Kuna Haki hapa?
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..hivi hawezi kushtaki na akidai fidia kwa mateso aliyoyapata?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Kwa sababu alikamatwa nje ya Marekani na kuachiwa nje ya Marekani itakuwa vigumu kushtaki. Na sasa hivi hatuna hata serikali itakayokubali kutetea maslahi yake. Nimesoma kuna wengi tu wa aina yake waliopelekwa Guantanamo.
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kuna mbongo mmoja aliyehusika na kubomu balozi ya US bongo, kuna wakati kabla hajafungwa nafikiri maisha kule US, aliwahi kusota sana rumande pale Metro-Fed Manhattan, kule downtown New York,

  Wakulu wanaohusika waliniomba nimtafutie Q'uraani, maana kule rumande hawakuwa nazo, it was very sad indeed kumuona mbongo katika ile situation I hope kweli alihusika.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  Duh! inasikitisha kweli! Sasa wamemharibia maisha yake bila hata kumlipa fidia yoyote. Kuna haja ya watu kama hawa ambao wanaonekana hawana hatia walipwe fidia kubwa ili kufidia unyama waliofanyiwa. Akipata mwanasheria mzuri huyu anaweza kuambulia fidia.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bubu,
  Si huyo tu. Kuna raia wengi kutoka Saudi Arabia ambao walikuwa Guantanamo kwa kosa la kuwa at the wrong place at the wrong time. Iliyonisikitisha zaidi ni pilot mmoja wa Ivory Coast ambaye alikamatwa Miama akiwa na redio yake, akahamishiwa New York, kwa sababu tu alikuwa Muislamu, akafungwa, na baadaye ikathibitika kuwa hakuwa na uhusiano wowote na Al Qaeda, September 11 lakini ameswekwa lupango kwa zaidi ya miaka mitatu. Na huyu hatimaye aliondoka bila kupewa fidia yeyote. Hata serikali yake haikutoa malalamishi kwa sababu waliogopa ile kauli mbiu "either you are with us or you are against us." Subiri baada ya kipindi cha Bush kumalizika utasikia stori nyingi za mateso yasiyo na sababu kama yale yaliyowapata Wamarekani wenye asili ya Kijapan baada ya Pearl Harbour.
   
 7. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Kuna thread nilishawahi kuuliza kuhusu Watanzania wangapi walioathirika na hii War on Terror na waliosombwa na ndege za CIA/FBI.on top of that nilikuwa curious kujua kama viwanja vyetu vya ndege au anga yetu imetumika kwa shughuli hizi..watu wakapuuzia...
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  yupo mcanada mmoja mwenye asili ya kiarabu, aliyekamatwa kwa upuuzi kama huo na akapelekwa majela ya nje ya marekani. baadae ya kuachiwa akapeleka malalamiko kwa serikali ya canada, na ikaifungulia mashitaka serikali ya marekani.
  amelipwa fidia ya mamilion mengi ya dola.

  serikali zetu hazijali watu wake tu.
  nakumbuka pia nilikuwa uingeerza na walirudishwa kutoka guantanamo vijana 4 waliokamatwa pakistan wakawekwa guantanamo kwa miaka mingi sana.
  ilikuwa big issue, na mpaka kuonyeshwa live covarage kwenye tv zote. na walienda kupokewa na serikali.

  nashangaa huyu mtanzania.....membe kazi yako si kwenda kutanua tu marekani, kazi yako ni kama hii pia
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Sep 2, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  gaijin,jasusi,icadon,mwanakijiji,

  ..yaani Watanzania tunateseka mara mbili. tumelipuliwa na hawa magaidi, halafu kama hiyo haitoshi, raia kama huyu anakamatwa na kuteseka namna hiyo.

  ..sasa tuwalaumu Magaidi, au Wamarekani?
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Pole sana Morris...inasikitisha sana anatakiwa adai fidia watamlipa...kwa mateso makali sana ambayo hayasahauliki kabisa.....pole sana inatia sana uchungu....
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  kwanza kuthibitisha kuwa alikamatwa na wamerekani itakuwa kasheshe...hawa fbi ni wahuni sana wakiwa nje ya marekani.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii ni fursa ya akina Mkono na Chenge kuonyesha umahiri wao katika sheria
   
 13. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Wako madarakani kwa sababu wanazozijua wao, wakifanya mambo yasiyopasa!  .
   
 14. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  madawa ya kulevya hayo ndiyo chanzo hasa cha kuwafikiria vibaya ... acheni biashara hii jamani .. maana angekuwa na akili timamu pengine mateso yote hayo asingeyapata na angeachiwa mapema zaidi

  Pole sana kaka (morris) ila shukuru Mungu maana kakuokoa na madawa na jela pia
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Khalfan Ghailan yuko wapi? nilimsikia mama yake akilalama kuwa mwanawe hana hatia....lakini ikumbkwe alikamatwa kwenye battle fire kule Afghanistan....

  Mnamkumbuka na yule Msudan kama sijakosea mpiga picha wa Aljazeera nae hakuwa na ahatia alirudishwa Sudan mwezi wa 5 mwaka huu......hii ni kuonyesha the failure ya US foreign policy.....mpaka leo hao wanaoitwa magaidi wengi wao kumbe ni innocent people.Aibu Bush na Nyani Mcain......
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yupo Guantamano, kesi yake ilishaanza kusikilizwa
   
 17. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana kwa kweli nimetokwa na machozi wakati nikisoma simulizi hizi. Pole sana Mtanzania mwenzetu kwa mateso uliyoyapata
   
 18. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bwana mdogo, nakupa pole sana kwa yote yaliyokukuta. najua imekuathiri sana, ila ichukulie kama ni somo/challenge kwako kuhusu namna ya kuishi. kwamba unatakiwa kuishi kwa utaratibu, usiwe unaenda nchi za watu bila utaratibu, kama nchi hizo hazina utaratibu wa visa kama somalia, basi usiende kama ukienda ukubaliane na yote yatakayokupata huko.

  kwa upande wangu, najua wamarekani wengine wanaweza kuwa wabaya kama walivyo hata watu wengine, walikutesa/walikuinterrogate ili wapate jibu. sio walikuwa wanakutesa. mazingira waliyokukuta nayo ndiyo yaliyokupelekea kuyapata hayo. kufuga ndevu kama osama si vizuri. kuamini dini anayoamini osama sio vizuri. ndo maana yanawapata hayo. ulishawai kuona wapi mkristo hata mmoja amekamata kwenye huo ugaidi wenu? pateni somo basi, acheni hiyo dini yenu ya ajabu, ndo maana yanawapata hayo. ndo maana watu wanadanganywa vihela hata wakakubali kulipua ubalozo Dar wawauwe hata watz wenzao kwasababu tu ya wamarekani. hii dini ni mbaya, ikimbieni. kama hamkimbii, mnaona yanayowapata?na bado. nashukuru umerudi, wewe kama mtz mwenzangu. lakini kwa wale ambao bado wako kule, naomba Mungu kama hawana makosa warudishwe haraka, ila kama wana makosa, wawanyonge tu, ndo sheria ya kule inavyosema. ugaidi ndo matunda yake.

  siamini unachokisema kuhusu nyimbo humo kwenye mashimo, unaonekana unaongea ili watu wawaone wamarekani kwasababu ni wakristo basi dini ya kikristo sio sahihi, inakiri kuwa hakuna mungu kama unavyosema ulisikia. ni shetani tu alikuwa anakutia moyo kumbe anaenda kukunyonga, shukuru Mungu umerudi. ibilisi sio rafiki yako, hayo masauti ulikuwa tu umechanganyikiwa na kifo au mapepo yalikuwa yanakuongelesha wewe rafiki yao, ili uone kama dini ya kikristo wanayomwabudu Mungu ktk kweli ni ya uongo. uislam sio dini sahihi na hawana Mungu kweli, hapo sehemu zingine walisema ukweli. natumaini utabadilisha tabia, ubakie hapa tz ulitumikie taifa, uache kwenda somalia na kushirikiana na magaidi wengine kule kwenye islamic court rebels. sikiaaa!3
   
 19. M

  Masatu JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Atafute competent lawyer afungue madai ya fidia haraka sana. Kulalama bila ya kuchukua hatua hakutasaidia "those who ask for nothing gets exactly what they ask for. NOTHING!" Author: Masatu
   
 20. w

  wajinga Senior Member

  #20
  Sep 2, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa huyu kijana akiwa gaidi kweli mtamlaumu. Aanze kukaba wamarekani nae huko tanzania maisha ni tit for tat. Violence will be treated with violence by any means necesary.
   
Loading...