Mzalendo yachakachua taarifa ya maaskofu kuhusiana na Katiba

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Gazeti la Mzalendo la leo lina kichwa cha habari kisemacho.................Katiba isisabishe vurugu- Maaskofu.........................

Na maudhui iliyomo ni kuwa mchakato wa kudai katiba mpya au marekebisho yake usifanyike katika mazingira ya kusababisha vurugu...........................

Lakini pamoja na ukweli hayo yaliongelewa lakini la muhimu ni kuwa Maaskofu hao walitahahdharisha ya kuwa raia wasipotendewa haki amani itatoweka na vurugu kutokea.............................hivyo walikuwa wanatahadharisha juu ya mazingira ya uvunjwaji wa amani ambao waweza kutokea............................

Kwenye gazeti la habari leo............lenyewe lina kichwa cha habari kisemacho........................Maaskofu wahofu amani kuchezewa....................................

Na the Daily News lenyewe limeweka habari hii kama ifuatavyo..................

Clerics extol virtues of good leadership, peace

DAILY NEWS Reporters, 25th December 2010 @ 11:59

12_10_eex9c2.jpg


CHRISTMAS SERMONS: Worshippers listen as Bishop Steven Wang'ana (inset) of the Mennonite Church of Tanzania delivers Christmas sermons at Upanga Mennonite Church in Dar es Salaam on Saturday. (Photos by Staff Photographer)

The Arch-Bishop of the Mennonite Church of Tanzania, Mr Stephen Wang'ana, has called on government leaders to serve the people of this nation efficiently and with integrity.

"Let ministers, permanent secretaries and all other entrusted leaders serve the people fairly, fight injustice and corruption.

President Jakaya Kikwete appointed them to be exemplary," Bishop Wang'ana said when delivering sermons at Christmas mass on Saturday.

He told worshippers that Jesus Christ brought salvation and peace, in the same way, leaders have been entrusted to serve the nation not to accumulate wealth.

"The nation is sick and tired of bad news such as frequent power cuts, poor infrastructure, corruption, dubious contracts," he said, adding that it was high time dishonest leaders repented and walked on the clean path.

On healing the wounds that stemmed from last October elections, Bishop Wang'ana said rival groups should now iron out their differences and join forces to build the nation. "It is time for reconciliation. Separated families should forgive each other and open a new chapter in life. Social frictions undermined unity, prosperity and peace," he observed.

Quoting from the book of Luke Chapter 1 verse 79, that says; "Jesus came to give light to those still in darkness and in the shadow of death, to guide our feet into the way of peace," the bishop said peace would never triumph where there is resentment.

"We need a country that is free from corruption, deprivation and demonstrations. Low income earners suffer a great deal because there are no drugs in public hospitals," he said, adding that for peace to prevail, that situation must change.

Reverend Agutu Oballa of Sinza Mennonite Church challenged the national leadership to remember the down-trodden of society.

"Africa has witnessed the suffering of her people in poverty, road accidents, disease, corruption and senseless wars. Nearly three quarters of the news that we received everyday is about bad incidents. Our leaders must change this scenario," Rev Oballa suggested.

At national level, Christmas Eve prayers were held at St Joseph Cathedral of the Roman Catholic Church in Dar es Salaam.

Delivering a homily, Auxiliary Bishop Eusebius Nzigirwa, implored Christians to fear God and stand for peace and love. He told worshippers on Friday night that it was only through worshipping God that Tanzanians would be able to enjoy living in peace and harmony. He called for peaceful resolutions of emerging conflicts in the country and urged Christians to follow the ways of Jesus Christ who was a symbol of holy life.

Meanwhile, Saint Alban Anglican Church Assistant Provost, Father John Solomon, said the proposed constitutional review should serve the interests of the nation and not a group of people.

"The birth of Jesus Christ that we celebrate today brings peace to us.We should pray for this peace to prevail always," said Father Solomon.

He cautioned that for peace and tranquility to prevail, the people must be empowered economically. "Peace and harmony will prevail only if people are assured of a better life...There will be no peace if people live in poor conditions," he cautioned.

Meanwhile, the Christmas Eve was celebrated peacefully in most parts of the city and the police were on the alert.

A random survey at some police stations showed that until midnight, there was no major criminal incident that had happened.
 
"Let ministers, permanent secretaries and all other entrusted leaders serve the people fairly, fight injustice and corruption.

Ujumbe wa muhimu wa maaskofu ni kuwa bila ya haki hakuna amani.........................au penye dhuluma panajenga misingi ya kutoweka kwa amani......................

Mzalendo yafaa wajirekebishe kwa kutanguliza mkokoteni kabla ya farasi.....safari hiyo itaendeka kweli?
 
Ujumbe wa muhimu wa maaskofu ni kuwa bila ya haki hakuna amani.........................au penye dhuluma panajenga misingi ya kutoweka kwa amani......................

Mzalendo yafaa wajirekebishe kwa kutanguliza mkokoteni kabla ya farasi.....safari hiyo itaendeka kweli?

Mzalendo lipo kwa maslahi ya chama na si kwa maslahi ya nchi!
 
Maaskofu wambana JK
Saturday, 25 December 2010 21:23

11pengo2.jpg
Waandishi Wetu
VIONGOZI wa dini wamemuonya Rais Jakaya Kikwete kwamba matatizo mengi ya kiutawala anayoyapata yanatokana na usaliti wa wasaidizi wake wa karibu huku wakisisitiza serikali itende haki ili kuepusha vurugu.

Wakihutubia kwa nyakati tofauti juzi usiku katika mkesha na jana wakati wa ibada sikukuku ya Krismas, viongozi hao walionekana kukerwa na nchi kukosa dira pamoja na masuala mazito nchini kuendeshwa kwa kubahatisha.

Vilevile, wamehofia kutokuwepo kwa mikakati ya makusudi ya kuwanusuru wananchi na matatizo yanayowakabili.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite, Stephen Mang'ana alisema baadhi wa viongozi wa CCM na serikali wanamsaliti Rais Kikwete kwa kumpa taarifa za uongo na uchochezi ili wapate nafasi ya kuendelea kuwepo madarakani.

Kauli hiyo ya Mang'ana inakuja siku chache baada mtandao wa Wikileaks kuchapisha habari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Dk Edward Hosea, kudaiwa kufichua siri za Rais Kikwete akisema hawezi kupambana na rushwa kwa vile amemzuia kuwafikisha mahakamani vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa.

Akizungumza jana katika misa ya kitaifa ya Sikukuu ya Krismasi jijini Dar es Salaam, Mang'ana alisisitiza baadhi ya viongozi wa serikali sio waadilifu, hawana utashi wa Mungu wa kuongoza wananchi na kwamba wanachangia kuwepo migogoro.

Alisema viongozi wamekuwa wakitumia migogoro kujisafisha kwa wananchi jambo ambalo amesisitiza linahatarisha amani na utulivu nchini.

"Baadhi ya viongozi hawana utashi wa kuongoza, wapo kwa ajili ya kumsaliti Rais Kikwete na kusababisha kuwepo kwa migogoro kila sehemu, kuchochea vurugu na maandamano hasa katika baadhi ya maeneo," alisema Mang'ana.
Kufuatia hali hiyo amewataka wananchi kuwa makini na viongozi hao, kwa kuwa hawana huruma na wapo kwa mslahi yao binafsi.

Alisema kitendo cha kutokuwa na washauri wazuri kumechangia baadhi ya wajanja kutumia nafasi hiyo kupandikiza chuki, jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.
Mang'ana, aliwakumbusha viongozi kuwa wanapaswa kuwa waadilifu ili waweze kufanya kazi zao kwa matakwa ya Mungu na si vinginevyo na kwamba waonyeshe uaminifu wao kwa kutenda mema.
Mwadhama Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebio Nzigilwa alisema hatua ya mtandao wa Wekileaks kuingia nchini na kutoa siri za serikali na viongozi wake ni fundisho kwa viongozi wabadhirifu.

"Mtandao huo ni sawa na chombo chochote cha habari kinachoweza kuandika habari za uchunguzi kuhusu serikali yoyote duniani hivyo basi, kama ina ushahidi wa kutosha kuhusu taarifa zao wanapaswa kuendelea," alisema Askafu Nzigilwa.
Alisema kuwa, "Viongozi wabadhirifu wanapaswa kutambua kuwa wamewekwa madarakani na wananchi ili wawatumikie hivyo wanapaswa kuwa waaminifu wakati wote."

Alisisitiza kauli yake kuwa ingawa hilo sio tamko la kanisa na wala kanisa halijakaa na kutoa tamko lolote kuhusu hatua ya mtandao, huo kuendelea kuwaumbua viongozi wa mataifa mbalimbali duniani, lakini hapendezwi na tabia ya viongozi wadanganyifu kwa wananachi wao.

Aliwataka wanadamu kuwa waaminifu mbele ya Mungu na hata mbele ya binadamu wenzao kwa sababu kukosa uaminifu ndiyo chanzo cha siri zao kuvuja.
Kuhusu hatua ya mtandao huo kumgusa Dk Hoseah alisema, "Viongozi waliotajwa na ambao hawajatajwa na mtandao huo wanapaswa kujirekebisha".

Alisema hapendi kuona binadamu wakiumbuana wala mtu akiingilia kazi ya mwingine ama kufuatilia mambo binafsi ya mtu, lakini kama hiyo ndiyo itakuwa njia sahihi ya kuwarekebisha wanaofanya makosa, jamii haina budi kuukubali utaratibu huo.

"Twendeni tukasheherekee sikukuu ya kuzaliwa bwana wetu Yesu Kristo kwa amani na upendo na msijihusishe na vitendo vyovyote viovu wakati wa sikukuu na hata baada ya sikukuu," alisisitiza Askofu Nzigilwa.

Kuhusu Katiba, alisema: "Katiba sio Biblia, ni maandishi yaliyoandikwa na wanadamu na kila mwanadamu anaweza kukifanyia mabadiliko kitu alichokiandaa."
Alisema Biblia ndiyo kitabu pekee kilichoshushwa moja kwa moja kutoka mbinguni na ambacho mwanadamu hawezi kukifanyia mabadiliko na sio katiba ya nchi.

Alisema katiba ya nchi inaweza kubadilishwa muda wowote kulingana na mahitaji ya wananchi ambapo madai ya katiba mpya yameanza kupata baraka ya viongozi wa juu serikalini baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukusudia kumshauri Rais kuhusu suala hilo.

"Nisingependa kulizungumzia suala hilo kwa undani zaidi kwa sababu Waziri Mkuu ameshalizungumzia na ukizingatia kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi mkubwa serikalini mimi sina cha kuongeza sana."

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe alisema tathmini zilizofanywa baada ya uchaguzi mkuu hazikuwa za haki.
Kakobe alisema tathmini hizo zililenga kumjenga mgombea wa chama tawala ambaye anadai hakustahili kupewa haki hiyo.

"Makusudi ya kuja kwa Yesu Kristo ni kuleta amani iliyoambatana na haki, inapotokea katika nchi au jamii fulani haki ikakosekana, amani pia itapotea na kuleta machafuko," alisema Kakobe

Akaongeza:"Chanzo cha machafuko ni inapofikia mtu amepewa haki isiyokuwa yake na yule anayestahili haki hiyo akanyimwa,".

Kakobe alisema Tanzania inasifika kwa amani na utulivu, kutokana na waasisi wa nchi kutoa haki kwa wananchi na kwamba kwa sasa misingi hiyo haizingatiwi.

Alisema kila chama cha siasa kinatakiwa kupewa haki kama chama kingine na kuwa watu wanatakiwa kuondokana na fikra za kuwa na chama kimoja kinachoshika madaraka ndio chenye haki.

"Jamii inatakiwa kuondokana na fikra potofu za chama kimoja kushika hatama ya uongozi, huo ni ukale, na hiki ni kizazi kingine," alisema Kakobe.

Hata hivyo, Kakobe aliwataka viongozi kuacha kuzungumzia udini badala yake wazungumzie haki na masuala yanayochochea maendeleo ya taifa.
Mkururugenzi wa Shirika la Familia la Farijika nchini Tanzania na Kenya, Padri Baptiste Mapunda alisema viongozi wa siasa ndio wanaochochea udini.

Padri Mapunda alisema viongozi wa siasia wamekuwa wakiibua hoja kwamba nchi ina udini ili waendelee kutawala.
Padri huyo aliyekuwa akizungumza kwa ukali huku akipigiwa makofi na mamia ya waumini alisema, "Nchi haina udini kama wanavyodai wanasiasa, wanatapatapa tu, walitakiwa watuulize sisi viongozi wa dini kama kweli nchi hii ina udini.
Alikwenda mbali na kusema viongozi wa siasa wanataka kuleta vita ya udini iliyokemewa vikali na serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na akawataka Watanzania kuikataa dhambi hiyo.

Kuhusu katiba, alisema umefikia wakati kwa Watanzania wote kushirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya na si kuziba kubadilisha vipengele.

"Napingana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu suala la katiba mpya, hapa hoja si kumshauri rais wala kuziba viraka, Katiba ni ya wananchi si ya rais, tunataka katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi," alisema Padri Mapunda.
Alisema hivi sasa nchi inaelekea kubaya hadi kufikia hatua Jeshi la Polisi kuwapiga wabunge na wanafunzi wanaozungumza mambo kwa maslahi ya taifa na afafanisha matendo hayo na utumwa.

"Yesu alikuja duniani kukemea utumwa, sasa iweje mambo haya yatendeke Tanzania, umeme bei juu?, nchi ina wasomi wengi lakini wanashindwa kutumia elimu zao kuikomboa, hawa wasomi wamebaki na usomi wa darasani tu," alisema Padri Mapunda.

Alifafanua kwamba wasomi wanatumia ujinga wa Watanzania kuwaburuza kutokana na ufinyu mdogo wa uelewa wa elimu ya uraia.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Katoliki, Mwashamu Kadinali Pengo, amewataka wenye uwezo kutokuwa na ubinafsi wa kujilimbikizia mali nyingi na badala yake wawasaidie wenye hali ngumu ya maisha.
"Najua kuna baadhi ya matajiri tena wanauwezo wa kifedha lakini wanakuwa wabinafsi," alisema Askofu Pengo.

Alisema jamii inaamini kuwa, mtu akijilimbikizia mali ndio zitazidi kuongezeka siku hadi siku na kwamba hayo ni mawazo potofu na kutoweza kuwasaidia maskini ni kujitafutia hasara.
Alisema yeyote anayehubiri amani, lazima kwanza awe na amani moyoni mwake na suala la kuleta ama kulinda amani ni jukumu la kila mtu na haiwezi kuletwa na viongozi au mataifa makubwa kama ambavyo baadhi ya watu wanafikiria.

"Amani haiji kwa mabavu bali kwa paji la Mwenyenzi Mungu, amani haitegemei wenye mamlaka bali ni kila mmoja wetu bila kujali mali zetu, ilimradi tumtumikie bwana na kutenda mema.

"Siyo kama wakuu wa nchi ambao huketi chini kusaini mikataba ya amani, lakini kabla hata wino haujakauka, damu zimeshatapakaa mitaani kutokana na upotevu wa amani," alisema Pengo

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa aliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kuwataka wananchi waliochukua viwanja vya wazi kuvirudisha.

Mokiwa alisema viwanja hivyo ni mali ya watoto na wananchi kwa ujumla na kwamba havikutengwa kwa ajili ya biashara na makazi.

Aliwataka wadau wa elimu na ardhi kuhakikisha viwanja hivyo hasa vya michezo vinarudishwa ili watoto wapate sehemu za kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kuwajenga katika maisha yao.



Paroko wa kanisa Katoliki parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Mugumu Serengeti, Padri Alois Magabe alisema vitendo vya uchakachuaji vinazaa dhuluma,uonevu,manyanyaso na mateso kwa watu wengi na ni matunda ya nguvu ya shetani aliyeteka nyoyo za watendaji.

Alisema uchakachuaji wa mambo yanayogusa jamii una madhara makubwa kwa jamii husika na wanaofanya hayo hawana roho ya Mungu ndani yao, kwa kuwa ni mateka wa ibilisi na kuzaliwa kwa Kristo kunatakiwa kuwabadilisha.

"Hata zamani uchakachuaji ulikuwepo, Eva alimchakachua Adamu kwa kutumiwa na shetani na matokeo yake dhambi iliingia duniani na mateso yakaanza na wanaofanya kwa sasa vitendo hivyo vinavyoleta mateso kwa jamii wanahitaji kuzaliwa upya na Kristo," alisema Padre Magabe.

Akaongeza:"Mfalme wa amani amezaliwa mwenye uweza mabegani kwake anatakiwa kuwabadilisha wale wanaohusika na vitendo hivyo ili kuleta nafuu kwa
wananchi walio wengi,maana hakuna njia tofauti ya kujinasua zaidi ya kukubali kubadilisha maisha na tabia zao kwa njia ya Kristo.

"Vitendo vya uchakachuaji si vizuri kwa kuwa vinabadili haki na kuleta dhuluma ,uonevu,ukatili,na maisha magumu kwa watu. Si vya kunyamazia lazima tuwatake wahusika wazaliwe upya na Kristo mwenye uweza wa ajabu," alisema bila kufafanua uchakachuaji upi.


Paroko Romuald Massawe wa Parokia ya Mwenyeheri Mtoni Kijichi, aliwataka waumini kutotumia nguvu katika kutafuta amani hali ambayo huleta machafuko na kulipelekea taifa katika hali mbaya.

Massawe alisema amani katika familia ni lazima idumishwe kwa kufanya mazungumzo pale inapotokea kutoelewana baina ya wanafamilia wenyewe.

Massawe alisema Watanzania wanatakiwa kukataa tamaa za kidunia kama kujilimbikizia mali na madaraka.

Kwa upande wa Kanisa la Angalikana Jimbo la Zanzibar limesema wakati umefika kwa viongozi wa serikali ya Zanzibar kuangalia mfumko wa bei za vyakula ambayo unaendele kuwaathiri wananchi wanaowaongoza.

Mchungaji Michael Hafidh katika mkesha wa ibada ya krismasi uliyofanyika katika kanisa la Mkunazini Mkoa wa Mjini Magharibi alisema, "Hatuhitaji kusikia maisha bora kutoka kwa viongozi wa serikali wakiwa mjukwaani ila ni
lazima wachukue hatua za makusudi na za lazima kuleta matumaini hayo kwa jamii."

Askofu wa Kanisa la Katoliki Zanzibar, Augostino Shao aliwataka waumini kudumisha upendo, umoja na mshikamano.

Aligusia matumizi ya kondom na kusema kwamba sio kweli kama Papa Banedict karuhusu matumizi ya hayo na kuwataka waumini kujiepusha na vitendo vinavyopelekea kukumbwa na maambikizi ya virusi vya ukimwi.
 
Maaskofu wacharuka
• Wasema Katiba mpya haikwepeki

na Waandishi wetu


amka2.gif
MAASKOFU wa makanisa mbalimbali hapa nchini wamekemea tabia ya baadhi ya Watanzania na viongozi kujilimbikizia mali ilhali huduma za kijamii na maisha ya wananchi yakizidi kuzorota kadri siku zinavyosonga mbele.
Wamesema kuwa kama pengo kati ya walionacho na wasionacho litazidi kuongezeka kamwe amani na utulivu uliopo hivi sasa hautaweza kuendelea kwa kuwa wasionacho wataamua kutumia nguvu kuwanyang'anya walionacho.
Maaskofu hao wametoa kauli hizo kwa nyakati na mikoa tofauti, wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi uliofanyika juzi usiku ambapo walisisitiza kuwa kujilimbikizia mali kwa kutegemea jasho la wanyonge ni dhambi na kutaitumbukiza nchi kwenye machafuko.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam , Kardinali Polycap Pengo, alisema inashangaza kuona mtu mmoja akimiliki magari zaidi ya matatu huku kila moja likiwa na thamani ya sh milioni 300-400 wakati kuna watu hawana uhakika wa kula mlo mmoja kwa siku.
Pengo, alipokuwa akitoa mahubiri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam, alisema haipendi kuona watu wachache wakinufaika na jasho la wanyongea ambao maisha yao yanazidi kuwa duni kila kukicha.
"Wapo watu hivi sasa wamemsahau Mungu kwa kuishi kwa kujilimbikizia mali huku wenzao (maskini) wakihaha na kukata tamaa ya maisha, ni lazima tuwe na uchungu na wenzetu na tuache tabia ya kujilimbikizia mali," alisema.
Alibainisha kuwa ujio wa Kristo, ulilenga kuleta usawa hapa duniani lakini wanadamu hivi sasa wamesahau maana ya ujio huo na uwepo wa Mungu na wanamkimbia kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na maagizo yake.
Alisema ugumu wa maisha unaowakabili baadhi ya watu hapa nchini ndiyo unaowafanya wasiione sikuuu ya Krismasi kuwa na maana kwa sababu ya kukata tamaa ya maisha kutokana na matatizo ya kiuchumi waliyonayo.
Alisema watu ni lazima wafahamu kuwa, Kristo alikuja kwa ajili ya wanyonge, hivyo hakuna sababu kwa mtu kujilimbikizia mali na wakati wapo wenzake wanahangaika hospitalini kwa sababu ya kukosa dawa na huduma nyingine muhimu.
Aliongeza kuwa ni wajibu wa kila mtu kutumia nafasi yake vizuri, pasi na kuiba rasilimali za taifa kwani kwa kufanya hivyo kuudhulumu umma ambao unapaswa ufaidike mgawanyo wake.
"Tuwasaidie wenye shida, tupendane, na hapo ndipo tutakapozungumza kuhusu amani ya kweli, kinyume na hapo tutakuwa tunajidanganya kuwa tuna amani na utulivu," alisema.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex Malasusa, amekemea viongozi wanaojilimbikizia mali na kuwaacha wananchi wakitaabika wasiendelee na tabia hiyo kwani haimpendezi mungu na itachangia utengano ndani ya jamii.
Dk. Malasusa alikuwa akitoa mahubiri katika kanisa la Azania Front, ambapo alisema hivi sasa kumekuwa na tabia isiyopendeza ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakitoa msaada kwa kutaka sifa na kujulikana mbele za watu.
Alisema tabia hiyo inazidi kushamiri hapa nchini ambapo watu hawa wamekuwa wakivialika vyombo vya habari kwenye hafla ya kutoa misaada hiyo ili waonekana kuwa ni watoaji wazuri wa misaada wakati lengo lao si hilo bali ni kutaka kuonekana mbele ya jamii.
Mchungaji wa Kanisa la Mtakatifu Albano, John Solomon alisema suala la katiba linahitaji kufanyika kwa umakini katika ili kustawisha amani na utulivu uliopo sasa.
Alisema kuwa suala la katiba ni la Watanzania wote hivyo halina budi kuendelea kudaiwa katika misingi ambayo dola au wale wanaoidai kutumia nguvu.
Solomon alisema Watanzania wamekuwa na amani lakini wanaishi maisha ya dhiki hivyo uundwaji wa katiba mpya ule kutatua mgawanyo mbovu wa rasilimali za taifa ambao hauwanufaishi walio wengi.
Alisema katiba hiyo ikiundwa isiwe kwa ajili ya kunemesha wachache na kuacha wengine wakiendelea na amani yenye mateso ambayo hata mungu hapendi katika kuangalia baadhi watu wakinufaika kutokana na jasho la wananchi wengi.
Mkoani Iringa, Askofu wa kanisa la Endtime Harvest na mkuu wa kituo cha maombi cha Overcomers Power Sentre, Boazi Sollo alisema kuwa Katiba mpya ni ukombozi wa kweli wa Mtanzania na kuwataka wananchi kuendelea kuidai bila kumwaga damu.
Askofu Sollo alisema kuwa pamoja na Watanzania kuendelea kusubiri kwa hamu kubwa mchakato wa katiba mpya bado kuna haja ya kuendelea kuliombea baraza jipya la mawaziri ili kuhakikisha kuwa mawaziri hao wanafanya kazi kwa uaminifu pasipo kujiingiza katika vitendo vya rushwa.
"Viongozi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu na kuepuka kuongoza taifa kwa mapenzi yao na badala yake wanapaswa kutazama matakwa ya wananchi na kuepuka kula rushwa katika utendaji wao wa kila siku. "
Visiwani Zanzibar, Askofu wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh, amewataka viongozi wa Serikali kutekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila mwananchi kwa vitendo badala ya nadharia.
Alisema pamoja na kuwepo kwa ahadi ya maisha bora kwa Zanzibar wananchi wanaendelea kushuhudia maisha magumu na kupokea habari zisizo njema kwao ikiwemo vitendo vya ufisadi, dhuluma, ubakaji na uonevu ambao unaendelea kutawala katika jamii.
Mchungaji huyo alisema kuwa viongozi wamekuwa hawatoi habari njema kwa wananchi na badala yake wamekuwa wakitoa habari za kukatishwa tamaa watu wanaowaongoza.
"Unafuu wa bei za vyakula haupo na mlaji amekuwa akishuhudia kupanda kiholela wakati viongozi wapo na watu wanategemea kusikia habari njema ya kudhibiti vitendo hivyo," alisema kiongozi huyo wa kiroho.
Huku akinukuu vifungu vya Biblia aliwakumbusha waumini, "Yesu alikuja kuleta habari njema walionewa wawe huru, wenye njaa washibe na haki itendeke."
Alisema wakati umefika viongozi wa serikali na dini kuchukuwa hatua mbali mbali za kuondoa matatizo yanayoikabili jamii ili wananchi wawapunguzie ugumu wa maisha ikiwemo kuondoa tatizo la mfumko wa bei za vyakula.
Alisema uvumilivu kwa wananchi unaweza kumalizika kama kero zinazowakabili au migogoro itachelewa kupatiwa ufumbuzi na kucheleweshja suala zima la maisha bora kwa kila mwananchi.
"Jamii inakuwa na upole pale wanapoona hatua za makusudi zinachukuliwa na viongozi wao, katika kuleta habari njema kwa maisha bora," alisema Mchungaji huyo.
Taarifa hii imeandaliwa na Chalila Kibuda (Dar), Francis Godwin (Iringa) na Hassan Shaaban (Zanzibar)
 
Tutekeleza ya viongozi wa dini

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
JANA ulimwengu mzima ulisherehekea sikukuu takatifu ya kuzaliwa Yesu Kristo, lakini na katika ibada ya sikuuu hii viongozi mbalimbali wametoa kauli za kupinga au kuonya juu ya mwenendo wa taifa letu.
Miongoni mwa viongozi wa dini wanaoheshimika nchini Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Kardinali Polycap Pengo, alitoa kauli ya kuwataka Watanzania kuacha kujilimbikizia mali na kuwa wabinafsi wakati huku wengine wakiishi katika mazingira magumu.
Pengo anasikitishwa kuona kuwa kuna viongozi ambao wanamiliki magari matatu ambayo kila moja lina thamani ya sh milioni 300-400 wakati wengine wanakufa kwa sababu ya njaa au kukosa huduma muhimu.
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Michael Hafidh, amewataka viongozi wa serikali kutekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila mwananchi kwa vitendo badala ya nadharia.
Kwa mujibu wa mchungaji huyo ahadi za maisha bora zilizotolewa na viongozi ni hewa kwa sababu wananchi wanazidi kuishi kwenye maisha magumu.
Tunakubalina na maonyo ya viongozi hawa wa dini na tunawaomba viongozi wetu kusimamia kikamilifu rasilimali za taifa.
Kwa muda mrefu hivi sasa viongozi wamekuwa wakitumia rasilimali za taifa kwa masilahi ya watu wachache jambo linalochangia kuongezeka kwa umaskini.
Ni aibu leo hii, wananchi kuendelea kuwa maskini wakati kuna rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika ipasavyo wimbo wa umaskini usingekuwa ukisikika.
Hospitali, zahanati na vituo vya afya havina dawa kwa sababu ama zimechukuliwa na madakatari au wauguzi.
Kimsingi maisha ya Mtanzania, yamezidi kugubikwa na matatizo kila kukicha hivyo ni jukumu la viongozi kubadili uelekeo huo ambao unaashiria mabaya huko tuendako.
Tunaamini kuwa viongozi wetu watayapa uzito maonyo ya viongozi wa dini ili kuiepusha nchi kuingia kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.
Kama jitihada za kupunguza pengo la walionacho na wasionacho hazitachukuliwa kuna kila dalili za kutoweka kwa amani na utulivu.
Hali ikiendelea hivi haitakuwa ajabu tukiona wasionacho wakikosa uvumilivu pale wakiona rasilimali zao zikiendelea kuwanufaisha wachache.
Tusingependa tufike huko, uwezo na rasilimali tunazo, kinachotakiwa ni utashi wa viongozi kuacha tamaa za kujilimbikizia mali.
 
Back
Top Bottom