My Take: CCM,Upinzani na Demokrasia ya Ukweli

housta

Senior Member
May 25, 2009
159
27
Wanajamii,

Ni ukweli usio fichika kuwa CCM haikutegemea kilichotokea October 30.Kwa mtazamo wangu CCM walipata kura chache sana ukilinganisha na matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi.Ilikuwa ni lazima kwa CCM kuchakachua matokeo ili kuonyesha kuwa bado ipo in control of this country.Ukweli ni kuwa JK hakupata asilimia hizo 61-ish walizotangaza.Kutoka asilimia 80-ish(2005) mpaka hapo ni aibu kubwa kwa CCM na kumewafanya wajiulize maswali mengi.

CCM wanajua kuwa wasipojipanga vizuri watapoteza nchi na itakuwa vigumu sana kuipata tena.Ukweli ni kuwa wananchi itafika wakati(very soon) watachoka:kuibiwa kura,kudanganywa,kupewa statistics zisizo sahihi na kuibiwa nchi ili hali maisha yakizidi kududumaa.Kwa CCM kuondoka madarakani inabidi tukubali yafuatayo:

1. Upinzani ujiunge pamoja: Sauti mbili zikiungana hufanya hoja iwe na uzito.Wapinzani inabidi wajue kuwa kupigana mmoja mmoja hakutaweza kuikomboa nchi.Awamu iliyopita tulishuhudia wabunge wengi kuungana kwa pamoja kuikosoa serikali lakini wakati wa uchaguzi hakuna hata mmoja aliyethubutu kuvuka mipaka na kuendeleza mapambano.Ukiwa vitani inabidi uonyeshe 'consistency' na sio kupiga ngumi na kurudi nyumbani-ukiamka asubuhi unakuta adui ameshaweka na kambi nje ya nyumba yako.​

2. Viongozi wapinzani waamke sasa: Sijui kama ninaiweka vizuri hii lakini ukweli ni kuwa huwezi kugombea uraisi wa nchi mara 4 na ukawa unashindwa kila siku na bado hutaki kuandaa mtu mwingine aweze kupambana.Haikai akilini hata kidogo kuwa chama hakioni kuwa inabid kubadili strategies za upambanaji.Kila siku unakuja na staili hiyo hiyo,wananchi wanakuchoka.Vyama viangalie mbele na kuwekeza kwenye viongozi wenye mtazamo imara wa mbeleni na siyo kupokea vibaraka kutoka CCM.Ukiwa mpinzani ni lazima ukubali kuwa wewe ni adui wa CCM kwa hiyo strategies zako zote ziwe zinalenga kuikomboa nchi kutoka kwenye mizizi ya CCM.​

3. Kulia lia pekee hakutoshi: The so-called wapiganaji wa ufisadi walikuwa neutralised towards the end of the 2005/10 campaign.Sielewi ni kwa nini walianza na moto wote ule halafu wakarudi nyuma.What was the point ya yote yale?Inashangaza na inafanya tuamini kuwa the fight was personal rather than for the better of this country.Kama nilivyosema hapo juu kuwa ukiamua kupigana,sharti ujitoe mhanga wa kikweli.​

4.Bila kujitoa mhanga uhuru na demokrasia ya kweli haitapatikana: Labda hapa naweza kushambuliwa na wanajamii lakini ukweli ni kuwa discipline ya ukweli na ya kudumu haiwezi kupatikana bila watu kujitoa mhanga kwa ajili ya nchi.Kujitoa mhanga sio lazima iwe kwa njia ya vita.Tumebaki kutishiwa kidogo tu na tunarudi nyuma na kukaa kimya.Unafiki haufai na wapinzani wawe makini kwenye hili.CCM wanatumia vyombo vya usalama kutishia na kwa sababu hatuna ujasiri ulio imara tunarudi nyuma.​

5.WOTE TUAMKE SASA:Inasikitisha sana kuona watu wenye akili timamu kabisa wanatetea upuuzi unaofanywa na chama tawala.Either hatujui purpose yetu hapa kwenye nchi hii au tumekosa elimu bora ya siasa na kutambua jinsi ya kutambua na kumtahini mgombea.Tuamke sasa na elimu ianzie majumbani kwetu kwa watoto wetu kuwa mtu yeyote fisadi na kiongozi asiyeleta maendeleo ni hatari kwa maendeleo ya taifa.Tukubali kuwa CCM haitathubutu kutoa elimu kama hii kwa wananchi au watoto wetu kwa sababu wanataka kuendelea kuwa madarakani.​

6.TUJUE TUNATAKA NINI: Hii inaweza kuingia pamoja na kuweka strategies za uhakika na zenye msimamo imara na kuziuza kwa wananchi.Priorities ziwekwe kiuwazi(upinzani) na siyo kupigana wenyewe kwa wenyewe.Ikiwa ni 'full force' basi twende pamoja na kama ni kumpiga nyundo adui,tumpige pamoja.Katika awamu iliyopita haikuwa wazi Upinzani unataka nini hasa.Tuweke mikakati iliyo imara na tuwe makini kuirudia hii mikakati kuona kama tumefanikiwa na kwa kiasi gani.Kupata wanachama kutoka CCM hakutoshi kusema kuwa tumefanikiwa.What are the effects of being an Opposition party in our country?What level of contributions are we giving and committing for the future of our country?Tukiweza kuvuka haya yote hata msingi wa vita nao utakuwa imara.​

7. MWISHO: Viongozi wakubali kukosolewa:Kiongozi wa kweli ni yule anayekubali challenges kutoka kwa anaowaongoza.Kiongozi anayesikiliza na kulipiza kisasi siyo kiongozi na inabidi akataliwe.Uongozi wa kucheka cheka siyo uongozi.Kumuweka mtu awe kiongozi kwa miaka 30 halafu maisha hayajabadilika ni upuuzi na ujinga wa hali ya juu.​

Nawasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom