My Power Windows Polisi wameshindwa kabisa kuzuia wizi wa kwenye magari?

Hivi hawa polisi wa TZ wanalipwa mishahara ya kufanya nini haswa jamani! maana mbona sieleweio kabisa.
Ni kweli tatizo la wizi wa vifaa vya magari limekuwa sugu sana DSM nzima
na kwamba vifaa hivyo huuzwa kwenye mnada K'koo/Gerezani
Kwamba wezi wanajulikana....
LAKINI TATIZO NI KUBWA SANA KULIKO WATU WANAVYOLIONA...
Pale ambapo Jamii ilipowaruhusu Polisi wetu kuwa ombaomba kwa kivuli
cha Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi, ndipo Serikali ilipojivua wajibu wa kulihudumia Jeshi hilo
ipasavyo...magari yao hayana mafuta, hayapati matengenezo,hawapati vifaa vya ofisi
kama vile karatasi na wino hawalipwi mishahara na posho zao kwa wakati matokeo yake
wafadhili wakubwa ambao huonekana hadharani ama ambao hulisaidia Jeshi hilo kwa kificho baadhi yao ni wezi ama wanaofadika na vitendo vya wizi wa vifaa vya magari, wezi wa fedha nyingi za serikali(Mafisadi),
Matapeli maarufu kama akina ...milionaire..,Papa.... na ....Security, na wezi wakubwa wa madini ya shaba KUWA ni
marafiki wakubwa wa akina kamanda Suleiman wakiwafadhili makamanda wetu, pikipiki/simu aukuandaa mashindano ya mpira kwa vijana kuhamasisha ulinzi shirikishi bila kupata fedha toka serikalini.(Amtuzaye mpiga zumari ndiye huchagua wimbo)
TUSILAUMU TULIPOANGUKIA BALI TULIPOJIKWAA...
 
pole sana ndg...jamaa wamekuibia maeneo ya wapi?maana mi nnayo nissan primera kama yako hii,nilikuwa najipa sana moyo kutokana na uchache wa magari yenyewe hapo mjini...kumbe siku hizi hawachagui
 
nliibiwa kwa staili iyo kwenda police oysterbay eti napewa namba nimpigie mtu anirudishie ivyo vitu kweli hatuna jeshi la police kabisa badala ya wao kwenda kumkamata wananiachia nimfate mwenyewe na namba wananipa nkaachana nao
 
Pole sana mkuu, mie wameishaniliza Power Windows Kinondoni makaburini watakati tumekwenda kuzika.
 
pole sana ndg...jamaa wamekuibia maeneo ya wapi?maana mi nnayo nissan primera kama yako hii,nilikuwa najipa sana moyo kutokana na uchache wa magari yenyewe hapo mjini...kumbe siku hizi hawachagui

Hawa jamaa hawachagui... Mi wameniibia pale oil com ya mwananyamala kwa kopa... Cha ajabu ni namna wizi ulivyofanyika haraka kwenye eneo ambalo wakati wote linakuwa na watu wengi
 
pole sana, lakini usiwalaumu sana polisi wapo wachache na wana mambo mengi, jaribu kuwa unapaki sehemu za wazi na ikiwezekana kuna vijana wanazagaazagaa unaweza kuwaambia wakulindie na kuwalipa 500 au 1000/=
 
Wizi wa Power window vioo vya magari hasa hizi sight mirror, na head rest vinaibiwa sana , waibaji wengi huvaa vizuri sana , wengi ni watoto mashombe wa kiarabu, hawa watu hutembea na gari zuri kuliko hata la kwako, hutembea na nyundo ndogo yenye ncha ya almasi huweka kitambaa kizito kuzuia mlio , ugonga kioo mara moja na kumwagika kisha kufungua kama yao, vitu hivyo huuzwa Arusha, Mwanza kama wewe umeandika kioo cha gari hapo hawasumbuki sana , wanachukua fremu na mashine alafu wanachukua kioo cha gari makubwa kinauzwa elfu nane pale saba general wanakata vizuri na kufitisha alafu wanauza kama kipya au tshs 30,000 mpaka 50,000.00 jamaa hawa wanapatikana kariakoo pale big bon au kidongo chekundu. sasa hivi wapo wengi na police wanawafahamu sana wengine hutumia piki piki kubwa baja hazina namba na police hawana uwezo wa kuwafukuza kwa piki piki wala gari, baja ni sports bike hivyo huruka wanavyotaka.
 
i see.......
ukizingatia polisi hawana hata hayo magari na kama yapo kuu kuu, na vichochoro vya dar hawawezi kuwapata hata wakiwafukuzia.....

na hawa watu wanavaa smart kweli kweli, mie almanusra wanivunjie kioo cha bajaji yangu, millenium tower. bahati nzuri nilifika just in time, na sikumsuspect mapema kwa jinsi alivyo smart, mpaka nilivyofika nyumbani nacheki gari nakuta alianza kupikichua na kutoa zile fito/rubber nyeusi za kwenye kioo.
 
Kwavile Polisi wameshindwa au hawajakuwa na nia ya kudhibiti wimbi la wizi wa vifaa vya magari, ni wajibu wetu kutafuta mbinu ya kutupunguzia hasara zinazotokana na adha hii. Mimi kwa uzoefu wangu, nilifunga 2 way alarm ambayo inakupa notification kwa baadhi ya matukio kwenye gari yako. Gharama yake ni around 250,000, lakini inakuokoa na madhira mengi.
 
Wapi inauzwa hizo alarm hapa Dar?
 
Mkuu nakushauri usivinunue, tafuta wahuni wape laki mbili maliza kazi... ukiweza jitahidi upate mmoja wa wezi washa ya moto au tumia wazee wa kazi (sauzi shop) wafanye kweli, hutaona tena unaibiwa na watakuheshimu

POLISI NDIO VINARA WA HUO WIZI,
 
Ahsante kwa ushauri mkuu.... nahisi kama unajambo la maana unataka kuniambia ila lugha imekuwa ngumu. mimi nataka vitu vyangu niambie nitavipataje bila kuvinunua?
 
1.Kama utafanikiwa kuvipata jaribu kuweka alarm gari yako and never try to ignore alarm ikilia hata kama unadhani ni mtikisiko wa upepo au mlio wa magari makubwa yanayopita, wezi hutingisha gari mara kadhaa na kukaa pembeni kwanza ili litoe mlio na uzoee kama vile linalia lenyewe tu then wanavunja, litakapolia hutaangalia tena utajua ni yale yale.
2.Hata kama hupendi Tint weka hivyo hivyo hata kama ni ile ya kiwango cha kati, inasaidia kuficha vitu ulivyoweka ndani kama laptop, bags n.k. Hivi ndo chanzo cha kuvunjiwa gari mara nyingi vinapokuwa vinaonekana wazi.
3.Unapopark gari popote pale kama kuna mlinzi au mtu wa parking system jaribu kumuona na kuzungumza nae kirafiki sana ili ajue hio ni gari yako, mwahidi ukirudi utampa nauli so asikae mbali na gari yako, watu wengi huchukulia walinzi wa maenneo ya parking au wanaotoza hela kwenye parking ni walinzi wa magari yao pia kumbe c hivyo, wale wanalinda eneo tu na kukusanya hela, wewe unapark AT YOUR OWN RISK.
 
Unashangaa nin sasa hapo ..Polisi ndio wezi wenyewe kuna thread humu zaidi ya tano kuna nyingine ya juzi juzi tu kuna mdada aliibiwa escudo yake mitaa ya mliman city alipoenda polisi aliambiwa wanajua gari lake lilipo na atoe milion 3 ili wamludishie.Akakubaliana nao wakaenda kuwakamata sinza makaburin baa walipo panga kukutana.

Uliza wanao ibiwaga mliman city wakienda polis wanapewa majibu gan??

Gari zinazo kamatwaga na kupakiwa vituo vya polis huwa zinaibiwa vitu kibao kama power window.Engine control,sensor n.k

soko la vitu vya wizi linajulikana na limeruhusiwa sasa hapo imekaaje?
 
Pole mkuu mali yako alafu uanze mazungumzo na wezi?? Au ulimwibia demu jamaa ameamua kulipiza?
 
pole sana mkuu yalinikuta mimi nikawafuata polisi wakaja wakahakikisha
tukarudi kituoni kuandika maelezo POLICE REPORT, baadae wakaniambie
niondoke watafanya uchunguzi ila niwakatie ya mafuta kwa kweli nilichoka,
Kwa kweli nilimkatia ili aniandikie LOSS REPORT nikapeleka ins. wakanilipa
ila mpaka leo sijapata ujumbe wowote wa police kwamba wamefikia wapi

note:kama una bima compr. utalipwa mkuu 80% OF TOTAL COST!
 
Back
Top Bottom