Prosper C Manasse
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 635
- 690
SERIKALI AWAMU YA 5 ISHIRIKISHE WADAU.
*Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa mh.JPM ambaye amekuwa na nia njema tena ya pekee kwa taifa letu Tanzania.
*Kwa baadhi ya watu wanaweza kunishangaa kwanini namsifu lakini ukweli ni kwamba, kwa kipindi kifupi ambacho ameshika dola tumeona jinsi alivyojenga umoja wa kitaifa kwa kukemea uovu na kutumbua majipu sugu na jinsi pia anavyoendelea kutumbua majipu hayo.
*Kazi anayoifanya si kazi rahisi maana anajenga chuki kwa makabaila/mafisadi ambao wameona jinsi anavyokwamisha jitihada zao za kuiibia serikali na kufifisha kama si kupoteza ndoto za watanzania.
Operation tumbua majipu imegusa wengi kwa namna moja ama nyingine. wengine ni wahusika wa moja kwa moja, wengine ni tegemezi ambapo baada ya jipu kutumbuliwa wamejikuta wakikosa raha ambazo walizipata kwa wazazi/walezi/wapenzi ama waajiri wao, lakini yote haya ni katika kuimarisha taifa letu tanzania kufikia malengo.
Wadau kushirikishwa:
*Tumeona mambo mengi ambayo serikali imefanya na inafanya kwa nia njema tu lakini wakati mwingine inagusa maslahi ya watu ambao kimsingi si majipu wala vipele.
Mfano:
*Kunabaadhi ya taasisi, kampuni au mawakala ambao wanafanya kazi na serikali eidha ku'supply bidhaa, uchimbaji madini, wakala wa forodha au mengineyo kama hayo ambapo wamejikuta wakiguswa na kutumbuliwa majipu wakati makosa siyo yao na kama ni yao bali si moja kwa moja au wameshiriki kosa katika mchakato fulani, lakini ambaye anatakiwa kuwajibika ni serikali dhidi ya watendaji wake kisha kampuni husika zikapewa elimu, onyo na adhabu kulingana na kosa husika.
Mambo yanayojitokeza sasa.
*Katika harakati za viongozi kufanya kazi zao kwa nia njema tu, kumetokea malalamiko kadha wa kadha kwa baadhi ya makampuni ama mtu mmoja mmoja kutokana na serikali kufanya maamuzi ambayo ni mazuri kwa ustawi wa taifa letu lakini yanaumiza hata wasiohusika na makosa hayo.
Ushauri.
*Ni kweli kwmb haiwezekani uhamishe vyombo nyumba moja kwenda nyingine bila kutokea uharibifu wa chombo hata kimoja kuvunjika, lakini ni vyema serikali ikafanya maamuzi baada ya kuwashirikisha wadau ili itoke na maamuzi sahihi ambayo yatagusa wahusika tu bila kuleta athari hasi kwa wasohusika.Serikali ikumbuke kufanya ichunguzi kwa wadau hao hao ili kupata njia bora ya kutoa maamuzi sahihi yenye tija katika pande zote.
*Watanzania wote wenye nia njema ambao tunaangalia maslahi ya taifa badala ya chama, tumuunge mkono mh.JPM Na kumuombea yeye na serikali yake katika operation tumbua majipu, maana maendeleo si ya chama bali ya watanzania.
Hapa kazi tu.