My Opinion: Kati ya hawa watatu LAZIMA mmoja awe rais 2015

suala la wapinzani kuchukua urais 2015..!ni jambo gumu ila kama zikitokea jitihada bas ni selikal ya mseto.kwa sababu wachakachuaji ndo wananjia mpya za kuchaka chua..!
 
:A S 465:EAST OR WEST LOWASA IS THE BEST ana Msimamo, Muwajibikaji na Mwepesi wa kufanya Maamuzi magumu na kuyasimamia.Haya mambo mengine ya Kumchafua yanatokana na Vita vya Kisiasa kwa vile ili upate nafuu kisiasa hauna budi kumchafua unayedhani ni tishio kwako, hao wengine wawili hata huyo Asharose na Membe hakuna kitu labda kidogo Anna Tibaijuka sioni kama wanastahili kwa vile hakuna kubwa walilokwisha fanya tukaona "impact" yake.KEEP IT UP EDWARD NGOYAI LOWASSA niko nyuma yako naamini yo shall MAKE A FIFTH TANZANIA PRESIDENT:A S 465:
 
Kumshindanisha dr Slaa na hawa jamaa ni kumshushia hadhi yake mbele watz wanaomwamini kupita mtu yeyeto kwa sasas ndani ya taifa hili.

tuache porojo!!!!tufanye kazi kweli kweli!!!Dr Slaa kwa mazingira ya sasa hawezi kuwa rais!!!!!Satta alifanya kazi kubwa sanana hiyo ndio Slaa anapaswa kuifanya kwani hata robo yake hajaifanya mpaka sasa!!!
 
:A S 465:EAST OR WEST LOWASA IS THE BEST ana Msimamo, Muwajibikaji na Mwepesi wa kufanya Maamuzi magumu na kuyasimamia.Haya mambo mengine ya Kumchafua yanatokana na Vita vya Kisiasa kwa vile ili upate nafuu kisiasa hauna budi kumchafua unayedhani ni tishio kwako, hao wengine wawili hata huyo Asharose na Membe hakuna kitu labda kidogo Anna Tibaijuka sioni kama wanastahili kwa vile hakuna kubwa walilokwisha fanya tukaona "impact" yake.KEEP IT UP EDWARD NGOYAI LOWASSA niko nyuma yako naamini yo shall MAKE A FIFTH TANZANIA PRESIDENT:A S 465:

Maamuzi gani magum alishawahi kuyafanya ELunayokumbuka kwa haraka...

kama amefanyiwa fitika kama kumtoa chambo kisiasa,je huoni angetaja waziwazi wahusika wa ufisadi angeonesha msimamo unaosema wewe na kuongeza credit yake ktk kufanya mamuzi magum?

Je mambo yote ya upotevu wa fedha za umma yeye alikuwa wapi kwa nafasi aliyokuwa nayo? na kama kiongozi imara,shupavu,muwajibikaji na mwenye msimamo alisubiri nini kutotaja mambo yanayoendelea hadi yaje yaibuliwe na wengine badae.
 
hata kama kiongozi ni mlaji kupita kiasi,ni wajibu ila tu nasi wananchi tufaidike.uchumi ukue,mfumuko wa bei usiwepo,barabara,maji,umeme, visiwe vya shida! Kiongozi ale tu.RUKSA!
 
Tatizo ninaloliona hapa ni kumwangalia Dr. Slaa katika ulingo wa siasa za Tanzania kuanzia 2010,rafiki zangu historia siku zote inaweza ikakufundisha mambo mazuri na mabaya.Dr. Slaa bado ni mwanasiasa ambaye sijawahi kumtilia wasiwasi,uozo mkubwa wa viongozi wetu ndiyo katufumbua yeye,ni kiongozi jasiri,yuko tayari kufia nchi yake na watu wake. Dr. Slaa 80% is Tanzania president 2015 otherwise kwa kweli sijui
 
Mh.Edward lowasa hebu turudi nyuma hiyo rich mond epa sijui rada imefanyika wakati gani maana mnawaacha mawaziri wa mambo yanje wao ndio wanajua habari zote usione lowasa aliamua kujiuzulu kirahisi ukadhani alipenda huyo alichafuliwa sana jina kutokana na Nguvu kubwa ya kisiasa aliyenayo pia anajiamini sana kwanini hujiulizi ex-spika ndio anaendeleza mambohayo. Tafuta chanzo ndio ulaumu kuwa hafai atakapo pata hiyo nafasi nchi hii on line so Lowasa na slaa nawatazamia kwa nafasi kubwa
 
Mambo Kama ni hivi, 2015 Hanna rais kutoka CCM Tanzania.
We are comparing incomparable! Kwa ukweli wa Mungu, Mh Hussein Mwinyi uwezo wake siyo mdogo sana ila uwezo wake hauendani na wakati hata wizara inamwiya nzito pamoja na kuwa kazi nyingi zinafanywa na wanajeshi.
Mh Lowasa yeye anaelewa ukweli. Hata kama itaonekana alichokifanya Mh rais alikifahamu haimaanishi kuwa kosa halikuatendeka. Nadhani kwa busara aliyoitumia kujiuzulu inatakiwa itumike kuachana na urais! Uongozi ni mzuri ila hali imechafuka, watu wamezidi kuwa waelewa na nyakati zimebadilika.
Nadhani watanzania wanaanza kuwa na uelewa. Nchi zilizotutangulia zimeweza kuwa na watu waelewa na ndiyo maana wanachagua viongozi wanaowathibitishia jinsi watakavyokabiliana na challenges wanazokuwa nazo badala ya kukimbizana na watu wanaotoa maneno matamu. Hii ndiyo sehemu watanzania wanapoelekea. Wanataka viongozi watendaji na bora na si bora viongozi.
Anjo
 
Mi naungana na Lil Sun. Tanzania tuna ugonjwa wa kuchagua bora kiongozi na si kiongozi bora. Kati ya waliopita, jembe alikuwa Mwalimu Nyerere tuu. Tunataka kiongozi ambaye hafungwi na misingi ya udini, bali uchungu na uzalendo kwa taifa lake ndiyo nira na dira yake, kama ilivyo kwa Jembe la Rwanda Bw. Kagame. Hapa bongo ni Dr. Slaa pekee.

umuhimu wa lowasa hata output inaonekana sasahivi tunalimwa pakubwa na output ni ziro kabisa, lowasa angekuwepo tusingekuwa hapa tulipo sasa. Tunahitaji mtu mwenye roho ngumu sio wa kulialia tu kila wakat na ndiondio zisizokuwa na msing.
 
Mh.Edward lowasa hebu turudi nyuma hiyo rich mond epa sijui rada imefanyika wakati gani maana mnawaacha mawaziri wa mambo yanje wao ndio wanajua habari zote usione lowasa aliamua kujiuzulu kirahisi ukadhani alipenda huyo alichafuliwa sana jina kutokana na Nguvu kubwa ya kisiasa aliyenayo pia anajiamini sana kwanini hujiulizi ex-spika ndio anaendeleza mambohayo. Tafuta chanzo ndio ulaumu kuwa hafai atakapo pata hiyo nafasi nchi hii on line so Lowasa na slaa nawatazamia kwa nafasi kubwa

naunga mkono hoja
 
Mkuu nimefurahishwa na sentensi yako ya mwisho! Huu mchakato wa katiba uanaoendelea JK anataka ahakikishe viongozi waliomaliza muda wao watahakikishiwa usalama. Why 2014 and not after 2015? Kutunga katiba mpya kwa mawazo yangu tunahitaji si chini ya miaka mitatu. Tume husika inatakiwa ipate muda wa kutosha kusikiliza maoni ya wanachi nchi nzima! Mzee Slaa ndio chaguo langu kwani ana maono ya kuifanyia hii nchi mambo makubwa.
 
BUNGENI: Mgomo wa madaktari na Sheria ya Bodi ya Mikopo
Asubuhi ya leo Naibu Spika Job Ndugai alitumia kanuni vibaya kuzuia hoja ya dharura bungeni kuhusu mgomo wa madaktari. Kimsingi, sikuwasilisha hoja ila niliomba muongozo wa Spika ili niweze kupatiwa nafasi ya kuwasilisha hoja ya dharura. Kwa kuwa hoja kama hiyo iliwasilishwa juzi na ikaungwa mkono lakini Spika akasema ameshakubaliana na serikali kuwa ingewasilisha kauli. Hata hivyo, jana hakukuwa na kauli ya serikali huku wananchi wakiendelea kupata madhara ya mgomo. Hivyo nikata muongozo kwa kuwa Spika alitumia kanuni ya 49 (2) ambayo kimsingi inatoa mwanya kwa kauli ya serikali kuwasilishwa kwenye wakati atakaoona yeye kuwa na unafaa juu ya jambo linaihusu serikali na lisilozua mjadala. Nilitaka kanuni hiyo isitumike badala yake wabunge tutimize wajibu wa kuisimamia serikali kwa kutumia kanuni ya 47 kuhusu hoja ya dharura. Kwa kuwa ilikuwa muongozo hakukuwa na hitaji la kikanuni la wabunge wengine kuunga mkono lakini akaamua kuilinda serikali kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa. Lakini mwishoni ameahidi kuwa kauli ya serikali itatolewa kesho.

Jioni ya leo bunge litajadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali na.2 wa mwaka 2011 ambao kwa sehemu kubwa ukiondoa sheria nyingine unahusu marekebisho ya kimsingi katika sheria ya bodi ya mikopo. Ni kwa bahati mbaya kwamba muswada huu umeletwa na hoja ya kusomwa kwa hatua zake zote tatu katika mkutano mmoja hivyo hakutakuwa na muda wa kukusanya maoni ya wadau kwa upana wake. Ni sehemu ndogo sana ya vifungu vya muswada huu ndio inapaswa kukubalika lakini kwa ujumla muswada huu unakwenda kuingiza mambo ambayo tuliyapinga kwa makongamano, migomo na maandamano yakaondolewa wakati sheria husika inatungwa mwaka 2004. Maudhui ya muswada huu yamenifanya nikumbuke makala ambayo niliandika mwezi kama huu lakini mwaka 2007: Kikwete anacheza na vichwa vya wasomi Marekebisho haya yanaenda kuweka mazingira mengine ya migogoro katika elimu ya juu nchini kutokana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi. Muswada huu ulipaswa kuja bungeni baada ya ripoti ya Tume ya Rais iliyoundwa tarehe 14 Februari 2011 na kukabidhi taarifa yake tarehe 29 Aprili yenye mapendekezo ya jinsi ya kuboresha utaratibu wa sasa wa ugharamiaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kuwekwa wazi kwa bunge na kwa umma ili kufanya marekebisho mapana zaidi ya kimfumo.
 
Back
Top Bottom