kibavu
Senior Member
- Oct 15, 2008
- 136
- 82
Kwako Luteni, kwanza naomba nikushukuru kwa kusoma mchango wangu na kuchokoza hoja; jibu langu ni kama ifuatavyo:-kibavu unavyoiona tanzania imefikia wakati wa kuongozwa na mwanamke nauliza tu.
Mkuu jibu langu halitakuwa la moja kwa moja, i.e. litakuwa na mzunguko kidogo, na nitarejesha baadhi ya hoja kwako. Nipo tayari kukosolewa.
Mosi, Kwa mtazamo wako unadhani Anna Makinda alikua mgombea bora zaidi kwa nafasi ya uspika kuliko wagombea wote ndani ya chama cha mapinduzi? Je ni kweli ilikua ni dhamira ya dhati kumuweka mwanamke kwenye ile nafasi ambayo ni muhimu kwa kuzingatia kwamba bunge ni moja ya mihimili mitatu ya dola? Jibu la hapa linaweza kukupa picha ya kwanini nimedhani kwamba 2015 kunaweza kusimamishwa mgombea mwanamke toka CCM.
Pili, kama ukirejea hotuba ya mwalimu J.K. Nyerere mwaka 1995 kwamba mgombea anayeteuliwa na CCM kwa kiasi kikubwa ni kama ni Rais tayari. Sababu unaweza kuwa unazijua kwani sina shaka na utashi wako. Moja wananchi bado wanachagua chama zaidi kuliko mgombea, mbili CCM bado ina faida ya kucheza kama mwenyeji na bingwa mtetezi na mtunga kanuni za mchezo na waamuzi pia.
Tatu, suala la msingi hapa kujiuliza liwe huyo mwanamke ni nani kuliko kuuliza kama Tanzania iko tayari kuongozwa na mwanamke. Binafsi si muumini wa mfumo dume naamini katika uwezo zaidi kuliko jinsia, dini, kabila au eneo mtu anakotokea. Nadhani wewe pia unaweza kuungana nami kwamba tuna mawaziri na viongozi wengine ambao ni wanawake na ambao utendaji na uongzi wao ni bora mara mia zaidi ya baadhi wanaume. Nakumbuka nilishawahi kumueleza jamaa yangu mmoja kwamba ni bora kuwa na kiongozi mwanamke anayewaza na kutenda kama binadamu kuliko kuwa na kiongozi mwanamke anayewaza na kutenda kwa kujaribu kuwaonesha wanaume kwamba yupo sawa na wanaume au ni zaidi ya wanaume.
Na mwisho ningependa swali lako uniulize kwamba je kuna mwanamke ambaye yupo tayari kuongoza Tanzania(kwa maana ya uwezo), na sio kama watanzania wapo tayari kuongozwa na rais mwanamke? Kwani kwa mtindo huo mwingine atakuja na kuuliza je Watanzania wapo tayari kuongozwa na Mmasai, mchagga, Mngoni n.k. Wengine watasema je Tanzania ipo tayari kuendelea kuongozwa na Mkristo/Muisilamu/Mkatoriki.n.k. Au wengine watasema je Tanzania ipo tayri kuongozwa na mtu wa kusini/Kaskazini/magharibi/Mashariki .nk. Matokeo ya huo mvurugano nadhani yapo wazi sina haja ya kuyaelezea hapa
Najumuisha hoja yangu kwa kusema suala ni uwezo wa huyo atayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali jinsia yake, dini yake, kabila lake, au kule anakotokea(nikimanisha eneo) au Chama chake.
Asante komrade Luteni...tuendelee kulumbana kwa hoja.