My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Ndugu yangu Eric,imefika wakati sasa nikueleze wazi kwamba wewe ni mnafiki na huna hofu ya Mungu bali una hofu ya serikali kwa sababu ya kuogopa maslahi yako kuguswa.
Taifa lipo pabaya tangu rais Magufuli aingie madarakani 2015.
Magufuli ni rais wetu sote,haitakiwi tumwogope bali tumwambie ukweli halisi bila kujali madhira yanayotukuta.
Lakini wewe unataka kutufanya siye hatuipendi nchi yetu ila wewe unaipenda sana.
Umeandika waraka wa hovyo mno kupinga maazimio ya EU juu Tanzania, kwamba EU inatuonea kwa sababu eti Rais anatetea raslimali Kama dhahabu baada ya kuzuia makinikia.
Waraka wako umejaa vichekesho kweli,ni waraka wa mtu muoga anayejipendekeza kwa serikali.
Tujadili kuhusu Raslimali,Rais hapigani vita ya raslimali bali anapigana kufuta amani ya nchi ambayo Mungu ametupatia kwa miaka mingi,anavunja katiba aliyoapa kuilinda kwa kunyanyasa wapinzani,mikutano ya kisiasa ipo kwa mujibu wa sheria na shughuli zote za kidemokrasia,lakini yeye anawaona wapinzani ni maadui wakubwa wa nchi.
1. Alphonce Mawazo aliuawa na watu wanaodhaniwa kuwa wana ccm hadi Leo hakuna aliyekamatwa kwa matukio hayo.
2. Ben Saanane alitekwa na kupotezwa na watu wanaodhaniwa TISS,lakini hadi Leo jalada la kesi yake limefungwa na Police
3. Tundu Lissu alipigwa risasi
4. Kanguye wa Kigoma alitekwa na kupotezwa
5. Azori Gwanda alitekwa na kupotezwa
6. Kijana Eric wa Sinza alitekwa na kupotezwa
7. Daniel wa kinondoni alitekwa na kuuawa
8. Makumi ya maiti zikiwa zimefungwa kwenye viroba zimetupwa baharini
9. Akwilina alipigwa risasi na Police kesi kapewa Mbowe
Yote hayo kwako ni sifuri halafu unajiita mcha Mungu, are you serious? Hujawahi kuandika waraka wowote kuumizwa na hayo matukio na wala kuitaka serikali iwajibike.
Umekuja kuibuka unaandika waraka kusema upo pamoja na Rais, unadhani ni nani yupo kinyume na Rais? Sote tupo pamoja naye lakini hili la serikali kukiuka haki za binadamu hatupo naye,na ndo msingi wa maazimio ya EU.
Suala la ushoga, lisiwe kiki, EU haijawahi kuipangia nchi yoyote mambo yake wala kuilazimisha ikubali ushoga.
Inachopinga EU ni tabia ya serikali ya awamu ya tano kutenda ukatili dhidi ya watu wake.
Hii nchi ni yetu sote, unadhani siye tunapenda iharibiwe?
Kwanini EU ionekane mbaya Leo hii na siyo awamu zingine zote? ina maana marais wengine walikuwa hawafai?
Yaani Dunia itazame tu unyama ukifanyika eti wasiseme kwa sababu we're the sovereign state, being a sovereign state doesn't mean you're free to practise inhumanity,tusijifiche kwenye kichaka cha taifa huru kutenda unyama.
Kama kweli una uhakika na waraka wako, mwambie rais pia azuie gesi isiende China, maana gesi ina thamani kuliko dhahabu, acha kujipendekeza simamia ukweli, mwogope Mungu na siyo binadamu, Duniani tunapita tu, our permanent shelters are in heaven.