Maxence Melo: My love for my Country, Tanzania

Nalipenda Taifa langu kwakuwa lina kila Rasilimali, ingawa Wananchi wake wamekuwa na maisha Duni, na baya zaidi ule usawa umekosekana, inauma sana.

Nilitegemea leo watu wanaweza kupata Mwanga au Elimu juu ya Taifa lao kupitia majukwaa Siasa na watu wengi kufatilia kwenye vyombo mbali mbali vya habari lakini inasikitisha kuona maeneo mengi hadi hivi sasa Umeme wameshakata, hili ni tatizo na wenye uwezo wa kulitatuwa ni Watanzania wenyewe, niwaombe huu ni mwaka wa Uchaguzi, tufanye maamuzi magumu na si yakishabiki, ili tusije nung'unika baada ya Uchaguzi.

Asanteni
Nawasirisha...
 
Kwa hali inayoendelea sasa na matamko yanayotolewa na wanasiasa, napata picha halisi ya nani ataijenga Tanzania.

Wanasiasa wengi wa chama tawala na upinzani katika vipindi tofauti huwa wanatuaminisha wana uchungu na tanzania na wapo tayari kuivusha Tanzania.

Nimegundua Tanzania itajengwa na wazalendo..kwa bahati mbaya wazalendo wapo wachache na huwezi kuwasikia wala kuwajua.

Nakumbuka katika sakata la madini mimi nilikacha masomo yangu nikaenda kumsikiliza zitto kabwe pale karibu na mlimani city kulikuwa na local hall ikiitwa DDC..siku hiyo ccm nao walikuwa na mkutano pale ubungo plaza na walipewa posho..wazalendo tukaenda kwa zitto kusikia tunavyopigwa kwenye madini.

Dr silaa alikuwepo ila uwanja ulikuwa wa zitto..alieleza namna mirabaha inavyopigwa na mikataba waliyoingia jamaa yaani life expectancy ya migodi ile kupitia uchimbaji jumlisha miaka ya mikataba..yaani mkataba ukiisha na mgodi wameumaliza.

Ni kipindi alichoondolewa bungeni kwa ishu ya buzwagi..nilipata kujua migodi mingi siku hiyo ikiwemo tulawaka, buzwagi, bulyanhulu na north Mara.

Cha kushangaza leo hii katokea mzalendo anaye dili na critical ishuz za nchi..lakini wanatokea wanasiasa kina zitto wanaanza kudili na personalities.

Kibaya zaidi ni pale zitto anapotetea mchanga uondoke wakati keshaambiwa kilichomo ni zaidi ya mchanga..ila ye kwake ni bora uondoke tu hivyo hiyo..ye hajali.

Ndio maana nimejifunza kuwa mwanasiasa ni mchumia tumbo, pretender, muongo, mnafiki, mbinafsi.

Kwa tabia hizo si rahisi mwanasiasa kuisaidia nchi au kuleta maendeleo bila ye kunufaika kwa namna yoyote ile.

Na ndio tunasema Tanzania itajengwa na wazalendo..si wanasiasa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom