Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,240
- 9,527
Mwaka 2007/2008 nilijiunga degree chuo cha Ushirika, wakati huo MUCCoBS pamoja na Makonda ndani ya program: BA- CMA.
Nikafanya semister ya kwanza na huyu mlokole,mtumishi mtanashati!
Sijui kwa wakati huo tu, labda hata leo.
Ila hakuwa mzuri darasani na alipoteza muda wake mwingi nje ya darasa na inaweza kuwa sababu ya yeye kufeli program hii mapema tu!
Kwenye Semester ya pili ya huo mwaka wa kwanza kukawa na uchaguzi wa viongozi wa chuo, kutokea rais mpaka wabunge.
Mimi sikuingia mapema kwenye kinyang'anyiro hicho.Nilichelea japo nilikuwa mguu ndani mguu nje.
Siku ya mwisho ya kurudisha fomu nakumbuka jamaa zangu watatu walinikomalia sana nigombee.
Nilikuwa nimetokea nyumbani siku hiyo na sikuwa na hela!
Basi jamaa wakasema Watalipia fomu.
Nikasema muda umeisha wa kuchukua Form, mshkaji mmoja a. k. a markfish akasema atashughulikia hilo tatizo.
To make long story short,nikaingia kwenye kinyang'anyiro siku ya mwisho bila ya kuwa na makamu wa rais.
Ikaja siku ya interview, na penyewe ikawa kimbembe.
Nilipoingia chumba cha kukusanyikia nikamkuta Makonda na wengine wamejipigilia kimavazi sio kipolepole.
Walipoanza kujadili siasa ndio nilipojua hawa jamaa wako vizuri nje ila ndani ni weupe.
Wakaitwa watu kuwa interviewed na baadae nikaitwa mimi na nilipotoka nikaenda kulala.
Sikuwa na matumaini makubwa sana kwakuwa sikutimiza kigezo cha kuwa na mgombea mwenza.
Nikiwa nimelala kama saa tisa ya usiku akaja 'afande John' kuniamsha na kuniuliza transcript ya matokeo yangu ya semister ya kwanza.
Alisema nimefanya vizuri kwenye interview ila siwezi kuwa rais kwasababu sina uzoefu wa kutosha.
Ila 'jamaa' aliyekuwa amesimama na Makonda, Makonda kama mgombea mwenza yuko vizuri kwenye urais na tume imeshauri tuwe pair na huyo jamaa. Mimi kama makamu wa rais.
Nikakubali, tukacampaign na tukashinda!
Makonda alikuwa wapi muda huo?
Alikuwa na sisi wakati wote japo siku mfurahia kwasababu ya mambo mawili.
Moja: kila saa anaitaja CCM. Yani hata matukio ambayo ningeweza kutoa tu hela mfukoni alitaka twende ofisi za CCM and God knows how much I hate this party.
Mbili: Sikupata kuamini utashi wake kwakuwa hakuwa muelewa wa mambo, yeye na darasa walikuwa mafuta na maji.
Nilishangaa alipokuwa mkuu wa wilaya, nilitamaani kuzimia alipokuwa mkuu wa mkoa.
Watu wanasema maisha ni bahati bwana na yeye amebahatika.
Ila ninachoona ni kuwa, kila Makonda anaposhinda Tanzania inapoteza!
Nitakuwa hapa kwa majibu na uthibitisho kama Vitatakiwa!
[HASHTAG]#Free[/HASHTAG] Godbless Lema