My First sale baada ya kuwafikia watu si chini ya 100 katika kipindi cha Corona nikifanyia kazi nyumbani

Hypolite

JF-Expert Member
Jul 6, 2017
226
459
IMG_20200522_110027_747.jpeg
IMG_20200522_110058_901.jpeg
IMG_20200522_110102_988.jpeg
IMG_20200522_110040_911.jpeg
IMG_20200522_110055_231.jpeg
IMG_20200522_110044_899.jpeg



Jifunze kuuza, jifunze kutengeneza kama una uwezo wakufanya vyote viwili kwa pamoja hushikiki!~Naval Ravikant.

Kuna balaa niloliona katika salesmen/women wengi hasa hawa wa door to door wakikuapproach wanajitambulisha nakuanza kutema maneno kama automated robotics, shida kubwa wengi wao humezeshwa maneno kweny trainings na sio kila utakachofundishwa utakikuta kama kilivyo, mteja aweza onesha hali tofauti na kile ulichofundishwa ukaishia kupoteana na kushindwa kumake a sale kua flexible na uende na beat la soko linavyoenda sio kila sehemu utacheza beat ya singeli.

Kutengeneza mteja kwa mara ya kwanza ni ngumu ila kuuza kwa mteja uliyemtengeneza mwanzoni ni rahisi.

Ukienda kinyonge hutouza watu hawanunui kwa sababu yakutia huruma kwako, onyesha kuchangamka nakua na imani na kile unachokiuza.

Well niende moja kwa moja kweny ujumbe baada ya hzo highlights

Niliwafikiaa watu si chini ya 100 kwa pamoja kwa wakati mmoja katk platform ya whatsap kwa njia ya direct messaging(Dm/inbox), watu hawa nlkua na option yakuwafikia kwa message moja katka whatsap group niliona kufanya hivyo ni less effective maana
ni rahisi message yakupromote bidhaa zangu ikafunikwa na mrundikano wa message kweny group.
Ni rahisi jamaa mmoja from no-where asiyejielewa kuzikosoa bidhaa zangu ambayo inaweza msababisha mteja mweny nia yakununua, kubuy maneno ya mkosoaji na kughairi kununua bdhaa.

Target ilkua ni kupromote Youtube channel yangu niliyoifungua 2 weeks ago sambamba na kupromote tangible artwork kwa mtu ambae angehitaji, Niliandika ujumbe wangu uliosomeka;
U hali gani mkuu, naitwa (..........)
Support kazi yangu ya uchoraji(hyper realisim arts) kwa kutembelea na kusubscribe katika youtube channel yangu.
Kama hutojali waweza ntumia screenshot ya subscription nkushukuru.

baada ya ujumbe zilifuata picha za kazi zangu nilizofanya kipindi cha nyuma kama sample kwa mtu nilyemfikia kama zinavyooneka hapo juu

Nilizima data kabla yakutuma message zote kwa watu si chini ya 100, nilifanya hivyo ili
kuepuka watu wakatishaji tamaa wawezao kuleta uzito katka mchakato mzima wakumfikia mteja niliyemtarget
Nilihitaji kuattend message iliyoonyesha muelekeo mkubwa wakutaka kuungisha kuliko kujikuta natumia muda mwingi kwa mtu asiye na muelekeo wakununua

Nilivomaliza kuandika kwa watu si chini ya 100 nkawasha data ya simu kudeliver jumbe zangu kwa watu nakukaa standby kuanza kuattend message yenye muelekeo mkubwa wakutaka kununua

Message za feedback zikaanza kuja i.e uko vizuri, kazi nzuri, nkaanza kupata na subscription screenshots na kila alyentumia subscription screenshot na aliyecomment kazi nzuri nilimuomba anisaidie kurepost kweny whatsapp status link pamoja na kuambatanisha kazi zangu ili kazi yangu ipate leverage iwafikie watu wengi zaidi hakika niliiona effect yake
subscription to my youtube channel ilipanda to 50 kwa muda mfupi na views maradufu

kuna baadhi walizani nafanya for hobby wakantumia picha zao niwatengenezee nkawapa gharama ya kutengeneza na time frame kulingana na muonekano wa picha na all detailed features zinazotakiwa kuonekana wakasema basi ntakuchek boss.

Nkapata mteja wa kwanza aliyenambia ntakutafuta kesho unifanyie kazi yangu ilipofika kesho akanipa kazi nami nkampa time frame ya 3days kazi itakua tayar i was sure enough ntaimaliza katk sku 1 na nusu nilifanya kuongeza muda ili nkipatwa na emergency still na muda wakuifanya kazi yake nakua katk nafasi yakuonekana ni mtu ninayewalk my talk.

Na wale wote waliopost kazi zangu kweny whatsapp status zangu nikawa narepost kweny my whatsapp status kama jinsi birthday boys na girls wafanyavyo nkawa nacheki pia namna wanavyouza walijitahidi kwa kiasi chake sio mbaya, waliorepost kazi watu wawili wakaniconnect na potential clients ambao nipo intouch mpaka leo hii kuna kazi ziko pending muda wowote watanipatia kuzifanya.

Kuna jamaa wawili out of blue wakajitokeza kudhihaki unaboa& kwa nini unanitumia si ungetuma group nkaattemd message zao katka namna yakuwaelewesha nakuachana nao, i have been used to rejection na mara nyingi ukiwa unamuapproach mteja hasa unapofany door to door selling cha kwanza akuonapo hua ni kama anakukasirikia vile ukiwin moyo wake unaweza tengeneza potential client mzuri
nliendelea kujibu kila ulizo lilo kua linakuja kwa watu wengine masaa kama mawili hali ikatulia na message zkapungua.

Naamu!
Unafahamu nini kuhusu sales na namna gani mtu aweza kua a great sales man/woman?
lets engange kweny comments.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu.

Mimi napenda sana biashara ila nguvu ya ushawishi ndio sina
Nilicho gundua ni kuwa ukiweza kutoa huduma nzuri na sahihi kwa wakati mzuri kuliko wenzako unaweza kuwin soko hatakama ushawishi wako ni mdogo

Kunajamaa naamfahamu alikiwa na kauli chafu kwa wateja lakini huduma aliyokuwa anatoa na bei za vitu vyake watu walikuwa wanapanga foleni dukani kwake.

Kuhusu wakatishaji tamaa wenye roho za husda hao wapo tu, tena wengi wao ni waganga njaa tu,wewe endelea kufanya mambo yako ukiwapa muda wako umekwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mkuu.

Mimi napenda sana biashara ila nguvu ya ushawishi ndio sina
Nilicho gundua ni kuwa ukiweza kutoa huduma nzuri na sahihi kwa wakati mzuri kuliko wenzako unaweza kuwin soko hatakama ushawishi wako ni mdogo

Kunajamaa naamfahamu alikiwa na kauli chafu kwa wateja lakini huduma aliyokuwa anatoa na bei za vitu vyake watu walikuwa wanapanga foleni dukani kwake.

Kuhusu wakatishaji tamaa wenye roho za husda hao wapo tu, tena wengi wao ni waganga njaa tu,wewe endelea kufanya mambo yako ukiwapa muda wako umekwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Naamu boss


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila uwa mna boa kweli sometimes adi uwa nawa block wenginehasa wanao nitumia forwaded txt ile ile kila siku

Dark Side
 
Ni stori ndefu kidogo, ila ukiwa na kaelimu kidogo ka photoshop na design nzuri ya kutengeneza katangazo kako unaweza.

Mfano jamaa hapo juu ni mchoraji, we unaweza kujiongeza kutengeneza tangazo alafu ukipata mteja unaongea na jamaa anakupa discount inakuwa kama ndo wewe umefanya hiyo kazi kumbe wapi, unakula chako, ukijiongeza zaidi unaweza kufanya hata kwenye bidhaa zenye demand kubwa inaitwa affiliate marketing .
 
Back
Top Bottom