LazyDog
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 2,473
- 199
Kufuatilia mjadala bofya hapa chini,
CHADEMA yafikiri kujiengua ushirika wa wapinzani!
What is your favorite?
CHADEMA yafikiri kujiengua ushirika wa wapinzani!
Gustanza vita dhidi ya Mafisadi si ya wachache. Ni ya Watanzania wote wenye nia njema na nchi hii. Ningelikusifu ungelikuwa unatoa way forward. Sioni courage katika criticism yako. Ninaona dalili za kukataa tamaa. sina hakika na sababu lakiini inatisha na kusikitisha kwa kizazi chetu. Wajukuu na vitukuu hawatakuelewa kabisa. Walioko ndani ya Bunge tumetimiza majukumu yetu, tumefungua milango, vita hivi vinahitaji kupokelewa na kila sekta katika jamii yetu. Hata wananchi wa kijiji waliopokea ujumbe, wakashika mabango, wakazomea waliotaka kupotosha, wakadai kabla ya kuelezwa chochote mabilioni yao yarejeshwe yanawazidi wasio na ujasiri na pessimists.
Mkuu labda hufahamu Bungeni tunafanya kazi kwa Kanuni. Tukinyamaza ni kwa vile Kanuni zinaratibu hatua inayofuata. Ngojea uone Courage siku itakapofika. Lakini tunategemea kama nawe ni 'mwana wa nchi' utaunga pia vita hii' kwa ujasiri wote, tena huna Kanuni zinazokuratibu...angalau kutoa mawazo Constructive humu JF.