Uzoefu wangu kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye anajiweza kiuchumi

Hii mada imenigusa mnoo lakini naomba niseme kitu kimoja mwanaume kama hujiamini na mwanamke wako akagundua udhaifu wako basi atakuburuza kama gali bovu,utasimagwa, utapelekeshwa,n.k

Kwa kifupi mwanamke akishajua mwanaume unajuamini hata ukiachana nae unaona huna cha kupoteza lakini pia ukawa mtu wa misimamo mwanamke atakuheshimu,atakusukiliza,

Shida inakuja vijana wengi wakikutana na Aina za wanawake waliowazidi kipato basi vijana wengi wao huwekeza moiyo yao ktk kupenda tuu kujibebisha wakifokewa kidogo bby am sorry kibao
 
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuingia katika mahusiano na mwanamke ambaye alinizidi kipato.

Mdada alikuwa anafanya kazi katika idara fulani serikalini. mazingira ya kazi ya idara yake yalitengeneza mianya ya rushwa, hii ilimfanya awe anatengeza pesa nyingi za ziada nje ya mshahara. ifahamike hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa JK, mzee wa Msoga.

Mdada alijiimarisha sana kiuchumi kuanzia kumiliki majumba, magari na biashara mbalimbali.

Sikuwa vizuri kiuchumi wakati nikiwa nae kwenye mahusiano. there was a big financial gap between me and her. Hali hii ilinifanya niwe very loyal to her.

Girlfriend wangu alinizidi kipato licha ya kwamba nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani binafsi na kunifanya nisikose pesa mfukoni.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyojifunza katika aina hii ya mahusiano.

1: Mwanamke wa namna hii huwa very independent and confident. Hapendi umpangie ratiba zake wala kumuingilia kwenye mambo yake. Kama mmeenda kwenye starehe, muache ajiachie mpaka achoke, kwa mfano ukimzuia asiendelee kunywa bia ili mrudi mapema nyumbani atakasirika maana anajua anatumia pesa yake.

2 : Kuwa mvumilivu pale anapopiga story na mashosti zake zinazohusu mikasa yao ya starehe au mahusiano na wanaume wengine. Usije ukaleta kiherehere cha kutaka kuhoji. Atakupiga biti.

3: Kubali kusimangwa, sina hakika kama wote wapo hivi, ila huyu wa kwangu alikuwa ananisimanga hasa akiwa amelewa. Kuna siku wakati tunarudi kutoka kwenye starehe nililazimika kushuka njiani baada ya kushindwa kuvumilia masimango ndani ya gari yake.

4 : Jiamini, kuwa vizuri kimwili na kiakili. Mwanamke wa aina hii hapendi kudate na mwanaume legelege. Yaani uwe legelege kwenye kipato na kimwili?, hapana.
Vaa vizuri, nukia vizuri and don't forget to put your body in good shape by doing different exercises. wa kwangu alikuwa ananiambia kabisa nimekupenda kwasababu upo vizuri kimwili na kiakili. Possess knowledge about certain common things. Angalau uwe unajua baadhi ya vitu kuhusu computer au matumizi ya vifaa vya kidijitali. Be street-smart, usiwe mshamba mshamba.

5: Kubali kukatisha ratiba zako na kufuata ratiba zake. Usitoe excuse pale anapokupigia simu kukutaka umsindikize sehemu. Ukifanya hivyo atahisi unamdharau, jiandae kukaripiwa au kununiwa.

6: Kwenye mapenzi hakikisha unamridhisha yeye kwanza, yaani mpe dozi ya kibabe mpaka moyo wake uridhike na umfanyie vile vitu anavyopenda kufanyiwa kitandani. Usilete utundu wako wa kutaka kufanya vile vitu unavyovipenda wewe. Utamkwaza.

7 :Usipende kuhoji mahusiano yake ya nyuma wala wewe usipende kusimulia mazuri ya EX wako. Atakwazika.

8 :Usimpangie matumizi hata kama unahisi fedha anazotumia zinazidi kiwango. Muache atumie vile anavyotaka. Kumbuka ni zake.

9 : Sifia umbile lake au mavazi yake hata kama unahisi siku hiyo hakupendeza.

10 :Mzawadie zawadi hata kama ina gharama ndogo. ataipokea na ataithamini.

11 :play your part by becoming her comforter during her difficult times. Kuna wakati anaweza kukuelezea changamoto mbalimbali za kazini kwake, biashara zake, ndugu zake au marafiki zake. Usiwe sehemu ya kuzidisha tatizo. Wakati wa mazungumzo msikilize na mwisho uje na masuluhisho sahihi.
Kwanza ukiwa mwanaume wa hivi unakua ni mpumbavu mkubwa na ni mtoto yamkini,na yeye akiwa wa hivyo kamwe hatakua na mtu maalumu isipokua wanaume wajinga wajinga

Yamkini hamjui sifa ya MWANAUME
 
Hii mada imenigusa mnoo lakini naomba niseme kitu kimoja mwanaume kama hujiamini na mwanamke wako akagundua udhaifu wako basi atakuburuza kama gali bovu,utasimagwa, utapelekeshwa,n.k

Kwa kifupi mwanamke akishajua mwanaume unajuamini hata ukiachana nae unaona huna cha kupoteza lakini pia ukawa mtu wa misimamo mwanamke atakuheshimu,atakusukiliza,

Shida inakuja vijana wengi wakikutana na Aina za wanawake waliowazidi kipato basi vijana wengi wao huwekeza moiyo yao ktk kupenda tuu kujibebisha wakifokewa kidogo bby am sorry kibao
Kabisaaa, mwanaume jiamin na utaheshimiwa sanaaa. Na wanawake wenye kipato zaidi akipata mwanaume muelewa na anayejiamin aisee couple yao itakua perfect.
 
Nipo ktk mahusiano na mdada wa aiba hiyo ila cjawahi kuwa boya kiasi hicho na sitokuwa boya kihivyo.

Ninachozinhatia ni kusimama ktk position yangu kaa mwanaume basi.Kitandani ndio nakomaa zaidi maana ni jukumu langu kumridhisha.

Ila asiniletee ujinga kabisa.
Kama unataka hiyo unayoiita ā€œposition yakoā€ tafuta mdada unayemzidi kipato. You donā€™t have any position there, stop being delusional!

Hata hivyo wanaume ni watu wema sana sisi huwa wanatulea mpaka mwisho wa maisha yetu, hapa ndio huwa naamini uwepo wa ā€œuasiliā€ na ā€œuhalisiā€.
 
Nakazia hoja..
Na mimi nina pesa jaman..
Mtu aje kunitongoza ila afuate muongozo wa mtoa mada hapo juu
emoji3.png
emoji3.png
hahah ninecheka balaaa
 
mwanamke akiwa na pesa ndio mzuri, kama nina zangu za kunitosha mimi za kula nyama ninapotaka aisee hawezi nipeleka atakavyo
 
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuingia katika mahusiano na mwanamke ambaye alinizidi kipato.

Mdada alikuwa anafanya kazi katika idara fulani serikalini. mazingira ya kazi ya idara yake yalitengeneza mianya ya rushwa, hii ilimfanya awe anatengeza pesa nyingi za ziada nje ya mshahara. ifahamike hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa JK, mzee wa Msoga.

Mdada alijiimarisha sana kiuchumi kuanzia kumiliki majumba, magari na biashara mbalimbali.

Sikuwa vizuri kiuchumi wakati nikiwa nae kwenye mahusiano. there was a big financial gap between me and her. Hali hii ilinifanya niwe very loyal to her.

Girlfriend wangu alinizidi kipato licha ya kwamba nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani binafsi na kunifanya nisikose pesa mfukoni.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyojifunza katika aina hii ya mahusiano.

1: Mwanamke wa namna hii huwa very independent and confident. Hapendi umpangie ratiba zake wala kumuingilia kwenye mambo yake. Kama mmeenda kwenye starehe, muache ajiachie mpaka achoke, kwa mfano ukimzuia asiendelee kunywa bia ili mrudi mapema nyumbani atakasirika maana anajua anatumia pesa yake.

2 : Kuwa mvumilivu pale anapopiga story na mashosti zake zinazohusu mikasa yao ya starehe au mahusiano na wanaume wengine. Usije ukaleta kiherehere cha kutaka kuhoji. Atakupiga biti.

3: Kubali kusimangwa, sina hakika kama wote wapo hivi, ila huyu wa kwangu alikuwa ananisimanga hasa akiwa amelewa. Kuna siku wakati tunarudi kutoka kwenye starehe nililazimika kushuka njiani baada ya kushindwa kuvumilia masimango ndani ya gari yake.

4 : Jiamini, kuwa vizuri kimwili na kiakili. Mwanamke wa aina hii hapendi kudate na mwanaume legelege. Yaani uwe legelege kwenye kipato na kimwili?, hapana.
Vaa vizuri, nukia vizuri and don't forget to put your body in good shape by doing different exercises. wa kwangu alikuwa ananiambia kabisa nimekupenda kwasababu upo vizuri kimwili na kiakili. Possess knowledge about certain common things. Angalau uwe unajua baadhi ya vitu kuhusu computer au matumizi ya vifaa vya kidijitali. Be street-smart, usiwe mshamba mshamba.

5: Kubali kukatisha ratiba zako na kufuata ratiba zake. Usitoe excuse pale anapokupigia simu kukutaka umsindikize sehemu. Ukifanya hivyo atahisi unamdharau, jiandae kukaripiwa au kununiwa.

6: Kwenye mapenzi hakikisha unamridhisha yeye kwanza, yaani mpe dozi ya kibabe mpaka moyo wake uridhike na umfanyie vile vitu anavyopenda kufanyiwa kitandani. Usilete utundu wako wa kutaka kufanya vile vitu unavyovipenda wewe. Utamkwaza.

7 :Usipende kuhoji mahusiano yake ya nyuma wala wewe usipende kusimulia mazuri ya EX wako. Atakwazika.

8 :Usimpangie matumizi hata kama unahisi fedha anazotumia zinazidi kiwango. Muache atumie vile anavyotaka. Kumbuka ni zake.

9 : Sifia umbile lake au mavazi yake hata kama unahisi siku hiyo hakupendeza.

10 :Mzawadie zawadi hata kama ina gharama ndogo. ataipokea na ataithamini.

11 :play your part by becoming her comforter during her difficult times. Kuna wakati anaweza kukuelezea changamoto mbalimbali za kazini kwake, biashara zake, ndugu zake au marafiki zake. Usiwe sehemu ya kuzidisha tatizo. Wakati wa mazungumzo msikilize na mwisho uje na masuluhisho sahihi.
Mahusiano yenye afya ni mwanaume amzidi na awe na uwezo wa kumhudumia mwanamke wake kwa kila kitu. Hii biashara ya mwanaume kutunzwa inanunua akili na uhuru wake hivyo kutojitambua. Wanaume wa hivyo hata kama wanagongewa bado hawawezi chukua hatua yoyote
 
Kama ni kweli basi huyo mwanamke atakuwa ni Mkorofi.

Mwanamke kuwa na financial freedom sio tatizo hata kidogo.

Tena ni jambo jema sana katika mahusiano ya kimapenzi.

Na hiyo ni kwa mujibu wa studies mbalimbali za kisayansi.

Sema huyo mwanamke anapungukiwa na ufahamu wa kuhusu kanuni za mahusiano ya kimapenzi.

Mwanamke kuwa na financial freedom hakuondoi uanamke wako (usikivu, ukarimu, subira, upole, huruma, n.k.)

Tena Kwa mwanamke mwerevu huwa na tahadhari kubwa sana anapokuwa kwenye mahusiano ya hivyo ili kuepukana na hali ya mwenzie kuona eeeh kumbe ananifanyia hivi sababu ya hivi na vile.

Mwanaume anatakiwa kuheshimiwa, kujaliwa, kupendwa , kutumikiwa, n.k hata kama ni lofa ilimradi mnapendana na mmeridhiana.

Kupata huwa ni majaliwa haipaswi kukoseana heshima.

Na. Mpaji huwa ni Mungu.
 
Kwa hiyo sio wanawake wote wenye financial freedom wako hivyo kama huyo isipokuwa ni huyo tu labda na wengine baadhi lakini kikubwa ni ukosefu wa maarifa kuhusu mahusiano ya kimapenzi.

Mambo mengine matharani hulka, ulimbukeni , uhuni, kukosa kuwa na uchaji Mungu, kukosa kujua Mwanaume ni mtu gani n.k. Pia kuchangia katika kuharibu mahusiano Kwa kutomthamini mwenza wako.

Ikumbukwe kuwa hata kama mko kwenye couple ya muda mrefu lakini haindoi ukweli kuwa ninyi ni watu 2 tofauti kwa hiyo msichukuliane Poa kila wakati.
 
Kwa hiyo sio wanawake wote wenye financial freedom wako hivyo kama huyo isipokuwa ni huyo tu labda na wengine baadhi lakini kikubwa ni ukosefu wa maarifa kuhusu mahusiano ya kimapenzi.

Mambo mengine matharani hulka, ulimbukeni , uhuni, kukosa kuwa na uchaji Mungu, kukosa kujua Mwanaume ni mtu gani n.k.

Ikumbukwe kuwa hata kama mko kwenye couple ya muda mrefu lakini haindoi ukweli kuwa ninyi ni watu 2 tofauti kwa hiyo msichukuliane Poa kila wakati.
Wengi wapo hvo wakishakuwa na pesa wanatamani wawe kam wanaume na dharau pia
 
Wanakosea kutaka kufanya hivyo.

Na kwa jinsi asili ilivyo kwa kufanya hivyo mahusiano ya hivyo huwa hayawezi kudumu.

Mwanaume atavumilia kwa muda kisha ataachia ngazi tu.

Lakini mwanamke iwapo unampenda Kwa dhati ya moyo Mwanaume wako utajishusha tu na kuonesha heshima wakati wote.

Tena hata katika kufanya ule utani wa kimahaba inabidi mwanamke uwe makini na umsome Mwanaume wako iwapo si mtu wa kuchukulia mambo negatively au positively la sivyo ataona unamdharau!
 
Back
Top Bottom