Uzoefu wangu kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye anajiweza kiuchumi

Huu utumwa wanawezaga wanaume wa kinondoni sana sana....bhasi wanajirizikia wenyewe hadi wananenepa kabisa na vitambi vyao vya chips.
 
Ulishindwa kusimama kama mwanaume, does it really matter ukwasi wake? Dadeq wa hivyo hata wiki haiishi.
 
We jamaa bure sana unakubali kuendeshwa na mwanamke kiasi hicho kwa kuwa ana pesa?
Nimekuwa na mtu aina hiyo na under control Sana
Sijamnyima uhuru kwa kuwa Ni mtu ambaye yuko smart sana
Lakini katika vitu vingine nimefit kwenye nafasi yangu wanawake hata wawe na pesa Ni mabaili kukupa pesa kukusaidia Kama una shida inawezekana lakini lazima tu aje kukusimanga siyo asili yao kumuhudumua mwanaume
Kuna wakati hadi namuonea huruma ila naona sawasawa tu ninge delay ningeburuzwa Mimi
Ananiambia ningejua kazini kwake yeye ni nani watu wanavyomuheshimu nisingecheza na yeye ningekuwa namuogopa
Nlichomwambia hata ungekuwa rais wa Tanzania ndiyo vilevile tu na hicho ndiyo kinakuharibia mizozo ya kila siku
Kisa we nifulani
 
We jamaa bure sana unakubali kuendeshwa na mwanamke kiasi hicho kwa kuwa ana pesa?
Nimekuwa na mtu aina hiyo na under control Sana
Sijamnyima uhuru kwa kuwa Ni mtu ambaye yuko smart sana
Lakini katika vitu vingine nimefit kwenye nafasi yangu wanawake hata wawe na pesa Ni mabaili kukupa pesa kukusaidia Kama una shida inawezekana lakini lazima tu aje kukusimanga siyo asili yao kumuhudumua mwanaume
Kuna wakati hadi namuonea huruma ila naona sawasawa tu ninge delay ningeburuzwa Mimi
Ananiambia ningejua kazini kwake yeye ni nani watu wanavyomuheshimu nisingecheza na yeye ningekuwa namuogopa
Nlichomwambia hata ungekuwa rais wa Tanzania ndiyo vilevile tu na hicho ndiyo kinakuharibia mizozo ya kila siku
Kisa we nifulani
Safi..vijana wanakuwa wapumbavu sana
 
Mwanamke ambaye ni independent na anajiamini haianzii from no wheree! Malezi yanachangia!

Nkupe mfano tu, kuna dada mmoja, namfahamu muda Sana. Yuko independent, anajiamini, na alikuwa na kazi ya kawaida sana, akafight akapanua biashara yake, sasa ako na pesa, ana Mme ambaye hana kipato km yeye mwanamke ila wanainjoi sana maisha wale wapuuuzi!

Sasa siku moja nikagundua mwanaume sometimes hajiamini, mkewe akipigiwa simu na wateja tu, mwanaume ananuna! Ha ha haaa...mwanamke wake anampa card ya bank akatoe hela wakutane jioni hotelini wale maisha huku wananyumba Kali kishenzi!

Ila wanaume tafuteni pesa bhana, mambo ya kujinunisha ndo nini? Mfyuuuu zenu, hata walio na hela wanatamani wanaume anaeweza nunua hata chupi km zawadi ,,wacheni zenu tupeni zawadi
 
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Nasema Uongo Ndugu Zangu
😁😂😀😄😃😃😂🤣😅😄😄😄
 
Nakazia hoja..
Na mimi nina pesa jaman..
Mtu aje kunitongoza ila afuate muongozo wa mtoa mada hapo juu
emoji3.png
emoji3.png
Sportslady tz na wewe unatafuta Mario!!
 
That's simp traits. Siwezi fanya hivyo aende na pesa yake akafie mbele.
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuingia katika mahusiano na mwanamke ambaye alinizidi kipato.

Mdada alikuwa anafanya kazi katika idara fulani serikalini. mazingira ya kazi ya idara yake yalitengeneza mianya ya rushwa, hii ilimfanya awe anatengeza pesa nyingi za ziada nje ya mshahara. ifahamike hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa JK, mzee wa Msoga.

Mdada alijiimarisha sana kiuchumi kuanzia kumiliki majumba, magari na biashara mbalimbali.

Sikuwa vizuri kiuchumi wakati nikiwa nae kwenye mahusiano. there was a big financial gap between me and her. Hali hii ilinifanya niwe very loyal to her.

Girlfriend wangu alinizidi kipato licha ya kwamba nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani binafsi na kunifanya nisikose pesa mfukoni.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyojifunza katika aina hii ya mahusiano.

1: Mwanamke wa namna hii huwa very independent and confident. Hapendi umpangie ratiba zake wala kumuingilia kwenye mambo yake. Kama mmeenda kwenye starehe, muache ajiachie mpaka achoke, kwa mfano ukimzuia asiendelee kunywa bia ili mrudi mapema nyumbani atakasirika maana anajua anatumia pesa yake.

2 : Kuwa mvumilivu pale anapopiga story na mashosti zake zinazohusu mikasa yao ya starehe au mahusiano na wanaume wengine. Usije ukaleta kiherehere cha kutaka kuhoji. Atakupiga biti.

3: Kubali kusimangwa, sina hakika kama wote wapo hivi, ila huyu wa kwangu alikuwa ananisimanga hasa akiwa amelewa. Kuna siku wakati tunarudi kutoka kwenye starehe nililazimika kushuka njiani baada ya kushindwa kuvumilia masimango ndani ya gari yake.

4 : Jiamini, kuwa vizuri kimwili na kiakili. Mwanamke wa aina hii hapendi kudate na mwanaume legelege. Yaani uwe legelege kwenye kipato na kimwili?, hapana.
Vaa vizuri, nukia vizuri and don't forget to put your body in good shape by doing different exercises. wa kwangu alikuwa ananiambia kabisa nimekupenda kwasababu upo vizuri kimwili na kiakili. Possess knowledge about certain common things. Angalau uwe unajua baadhi ya vitu kuhusu computer au matumizi ya vifaa vya kidijitali. Be street-smart, usiwe mshamba mshamba.

5: Kubali kukatisha ratiba zako na kufuata ratiba zake. Usitoe excuse pale anapokupigia simu kukutaka umsindikize sehemu. Ukifanya hivyo atahisi unamdharau, jiandae kukaripiwa au kununiwa.

6: Kwenye mapenzi hakikisha unamridhisha yeye kwanza, yaani mpe dozi ya kibabe mpaka moyo wake uridhike na umfanyie vile vitu anavyopenda kufanyiwa kitandani. Usilete utundu wako wa kutaka kufanya vile vitu unavyovipenda wewe. Utamkwaza.

7 :Usipende kuhoji mahusiano yake ya nyuma wala wewe usipende kusimulia mazuri ya EX wako. Atakwazika.

8 :Usimpangie matumizi hata kama unahisi fedha anazotumia zinazidi kiwango. Muache atumie vile anavyotaka. Kumbuka ni zake.

9 : Sifia umbile lake au mavazi yake hata kama unahisi siku hiyo hakupendeza.

10 :Mzawadie zawadi hata kama ina gharama ndogo. ataipokea na ataithamini.

11 :play your part by becoming her comforter during her difficult times. Kuna wakati anaweza kukuelezea changamoto mbalimbali za kazini kwake, biashara zake, ndugu zake au marafiki zake. Usiwe sehemu ya kuzidisha tatizo. Wakati wa mazungumzo msikilize na mwisho uje na masuluhisho sahihi.
 
Hahaaa yaan mwamba kafunguka kiasi kwamba niliondokana na fikira ya kwamba ninasoma kilichoandikwa bali ananisimulia live
 
Back
Top Bottom