My experience on how to date with a Woman who is 'Financially Stable'

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
1,600
2,000
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuingia katika mahusiano na mwanamke ambaye alinizidi kipato.

Mdada alikuwa anafanya kazi katika idara fulani serikalini. mazingira ya kazi ya idara yake yalitengeneza mianya ya rushwa, hii ilimfanya awe anatengeza pesa nyingi za ziada nje ya mshahara. ifahamike hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa JK, mzee wa Msoga.

Mdada alijiimarisha sana kiuchumi kuanzia kumiliki majumba, magari na biashara mbalimbali.

Sikuwa vizuri kiuchumi wakati nikiwa nae kwenye mahusiano. there was a big financial gap between me and her. Hali hii ilinifanya niwe very loyal to her.

Girlfriend wangu alinizidi kipato licha ya kwamba nilikuwa nimeajiriwa katika kampuni fulani binafsi na kunifanya nisikose pesa mfukoni.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyojifunza katika aina hii ya mahusiano.

1: Mwanamke wa namna hii huwa very independent and confident. Hapendi umpangie ratiba zake wala kumuingilia kwenye mambo yake. Kama mmeenda kwenye starehe, muache ajiachie mpaka achoke, kwa mfano ukimzuia asiendelee kunywa bia ili mrudi mapema nyumbani atakasirika maana anajua anatumia pesa yake.

2 : Kuwa mvumilivu pale anapopiga story na mashosti zake zinazohusu mikasa yao ya starehe au mahusiano na wanaume wengine. Usije ukaleta kiherehere cha kutaka kuhoji. Atakupiga biti.

3: Kubali kusimangwa, sina hakika kama wote wapo hivi, ila huyu wa kwangu alikuwa ananisimanga hasa akiwa amelewa. Kuna siku wakati tunarudi kutoka kwenye starehe nililazimika kushuka njiani baada ya kushindwa kuvumilia masimango ndani ya gari yake.

4 : Jiamini, kuwa vizuri kimwili na kiakili. Mwanamke wa aina hii hapendi kudate na mwanaume legelege. Yaani uwe legelege kwenye kipato na kimwili?, hapana.
Vaa vizuri, nukia vizuri and don't forget to put your body in good shape by doing different exercises. wa kwangu alikuwa ananiambia kabisa nimekupenda kwasababu upo vizuri kimwili na kiakili. Possess knowledge about certain common things. Angalau uwe unajua baadhi ya vitu kuhusu computer au matumizi ya vifaa vya kidijitali. Be street-smart, usiwe mshamba mshamba.

5: Kubali kukatisha ratiba zako na kufuata ratiba zake. Usitoe excuse pale anapokupigia simu kukutaka umsindikize sehemu. Ukifanya hivyo atahisi unamdharau, jiandae kukaripiwa au kununiwa.

6: Kwenye mapenzi hakikisha unamridhisha yeye kwanza, yaani mpe dozi ya kibabe mpaka moyo wake uridhike na umfanyie vile vitu anavyopenda kufanyiwa kitandani. Usilete utundu wako wa kutaka kufanya vile vitu unavyovipenda wewe. Utamkwaza.

7 :Usipende kuhoji mahusiano yake ya nyuma wala wewe usipende kusimulia mazuri ya EX wako. Atakwazika.

8 :Usimpangie matumizi hata kama unahisi fedha anazotumia zinazidi kiwango. Muache atumie vile anavyotaka. Kumbuka ni zake.

9 : Sifia umbile lake au mavazi yake hata kama unahisi siku hiyo hakupendeza.

10 :Mzawadie zawadi hata kama ina gharama ndogo. ataipokea na ataithamini.

11 :play your part by becoming her comforter during her difficult times. Kuna wakati anaweza kukuelezea changamoto mbalimbali za kazini kwake, biashara zake, ndugu zake au marafiki zake. Usiwe sehemu ya kuzidisha tatizo. Wakati wa mazungumzo msikilize na mwisho uje na masuluhisho sahihi.
 

Sainya Jnr

Member
Mar 14, 2019
66
125
Nakazia hoja..
Na mimi nina pesa jaman..
Mtu aje kunitongoza ila afuate muongozo wa mtoa mada hapo juu
 

Nduka Original

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
790
500
Kiongozi ulichoandika ni sahihi kabisa ila ni ngumu sana kuishi na wanawake wa design hii. Mimi sisemi mwanamke aliekuzidi kipato bali mwanamke ambae anajitegemea (Independeent)

Mwanamke akishakuwa hivyo hawezi sikiliza mwanaume muda wote na issue ni kwamba atapigania uhuru wake na akishaupata atakuwa anachepuka pia. Hivi imagine mwanamke kila week end aende ku party na mashost lazima adokolewe tu!! Najuwa madada comments kama hizi watazipinga lakini ukweli huwa tunawadonoa kwenye starehe
 

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
4,612
2,000
Na mimi wa jinsia Ke naunga mkono hoja, washkaji wanateseka sana jamani, mpaka huruma ila ndiyo hivyo wameganda zao hapo wanakula matunda ya uvumilivu wao.!

Vumilieni tu mazee, mlipenda na kuchagua wenyewe..! Ila sometimes wanaume baadhi yenu muache uphaller akii, hebu kazeni basii.!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom