My confession: Maji yamenifika shingoni, naamini ukweli humuweka mtu huru

Copenhagen tz

Member
Nov 2, 2017
94
86
Habari wana jukwaa,

Kwa utangulizi mimi sio mgeni JF nimeamua tuu kutengeneza I'd mpya nitoe ya moyoni, mnishauri, mniombee nadhani nitapumua.

Mimi ni mtanzania umri wa miaka 24 mama wa mtoto mmoja. Kinachofanya niandike hapa ni kupunguza mzigo wa moyo na akili. Nimezaliwa kwa familia ya kawaida tuu sikubahatika kulelewa na baba tulimpoteza nikiwa na miaka 7 tuu.

Nimesoma katika shule za kawaida tuu sikubahatika kumaliza six ilibidi niachie kidato cha 5 kwakua niliona napoteza muda na gharama zaidi (kipindi chote hichi nilikuwa kimahusiano na mwanaume niliyempenda sana ndo mwanaume wangu wa kwanza kuanzia kidato cha tatu.

Huyu mwanaume ndo tulishauriana kutokana na hali halisi ya maisha ikabidi niache shule akiahidiana na mimi atanisaidia kiasi flani kwa ajili ya ada ya chuo kumbuka yeye ana degree lakini hana kazi ya maana ni driver guide tuu kwa company ya saizi ya kati ivo akanishauri nikasome tour operator mwaka mmoja atanisaidia kupata kazi due ni mzoefu kwenye industry.

Nikaanza maisha mapya Arusha kwenye institution ya kawaida huku akisupport mno baada kama ya miezi5 company yao ilinunuliwa na mtu mwingine lakini wafanyakazi hawakubadilishwa bali waliongezwa baadhi tuu. Hivyo ikaandaliwa hafla fupi kwa ajili ya kutambulishana na mimi nikaalikwa, nikahudhuria nikatambulishwa kama mpenzi wa mfanyakazi mwenzao.

Maisha yakaendelea kawaida baada kama ya siku 4 mpenzi wangu alikuja na furaha akaniambia boss wake mpya amempenda sana na ameomba awe rafiki yake bila kusahau na mimi alimueleza kila kitu kunihusu. Nikaambiwa ameahidi kunipeleka mwaka chuo kikubwa cha utalii Africa mwaka unaofata maana hakukuwa na usahili kwa wakati huo, hivyo nimeambiwa kama nitapenda nikaanza kazi pale kama volunteer nitapewa hela kidogo ya kujikidhi tukaona ni neema.

Nakumbuka nililipewa laki3 kila mwezi ilikuwa nyingi mno kwangu, baada ya mwezi wa kwanza kazini mpenzi wangu alitakiwa akasome South Africa ili aje asimamie company kutokana na owner muda mwingi yuko nje ya nchi (sio mtanzania) kumbuka na cheo kitapanda hapa.

Kufupisha story baada ya mwezi owner alirudi Tz na alikuwa mkarimu na alinisaidia mno bila kuonyesha chochote maana hata hatuonani mara nyingi due yuko busy. Siku moja alinialika dinner hotel flani Arusha akidai anataka kuongea na mimi mengi maana alisikia kwa mpenzi wangu tuu.

Nilikubali mualiko nikaenda tuliongea tulikula apo I was 20yrs tuu alinishauri kunywa wine kidogo kwa ajili ya digestion, sikuwahi kunywa kilevi before nahisi nilizidisha sijui yaani sielewi lakini ilitokea nilispend night pale mpaka asubui na huyo owner.

Niliumia mno asubui lakini akaniambia sikukubaka ilikuwa makubaliano na nimefurahia mno naomba tuwe wapenzi nikamwambia flani ni mpenzi wangu akasema hajawai mwambia alimwambia mimi nirafiki yake wa childhood si vinginevo niliumia mno nikaondoka tuu.

Maisha yakaendelea nikijaribu kumu avoid sana lakini yeye hakuelewa niliongezewa mshahara up to laki7 . Mwezi huu sikuona siku zangu nilianza kuumwa kutapika nakumbuka nilipoteza fahamu kazini nilipopelekwa hospital nikaambiwa nina pressure lakini boss wangu alikuwa karibu sana na doctor baada ya muda nikaambiwa inatakiwa nifanyiwe ultrasound mpaka hapa sielewi chochote.

Nikaruhusiwa baada ya muda nikaambiwa nipumzike siku 7 nizingatie mlo hapa mzungu akazidi kuniganda anashinda kwangu anakuja kila muda bado sikuelewa lakini pia haniambii mambo ya mapenzi no.

Nilikuja kugundua mimba inaenda miezi 3.

In short ni mume wangu wa ndoa mpaka sasa na siishi Tanzania actually amebadilisha history ya maisha na familia yangu lakini tatizo ni mpenzi wangu yule sielewi kama alinipenda kila nikijaribu kutafuta mawasiliano ananimbia nataka kumuaribia maisha ananitumia picha za wanawake mara mtoto wake na ninampenda mno.

Mzungu hataki kusikia Tanzania familia yangu kila mwaka inalipiwa kila kitu kuja kunisalimia, ananimbia tulia usome na uangalie familia yako, niliwahi kuja Tz tukafikia hotelini ameniganda mpaka nimeondoka, sijawahi pata hata nafasi ya kuexplain what happened kwa mpenzi wangu uyo wa zamani.

NB: Mume wangu ananiridhisha onbed, kimaisha ujumla ananipenda ananijali mno lakini ananibana sipumui jamani huku ndani kumejaa dictionary pia ana translator akiona SMS or email anatafsiriwa hili linanikera mno.

Ndio namna niliyompoteza mwanaume wa ndoto zangu ninampenda mpaka Leo sema ndo ivo hajawahi nipa nafasi tena.

Nimejisikia kukiri tuu leo ukweli wa maisha yangu.
 
Wanawake bana anaweza kutoka out na mwanaume mwingine pasipo mwanaume wake kujua hata kumwambia hamna hakika rafiki wa kweli ni Yesu kristo hakuachi hata ukimkosea binadamu mwenzio kamwe hafai usimwamin mwamini Mungu mkuu halleluya kawashwa kakumbuka uovu alofanya anawayawaya anataka uhuru uhuru wa nin: EWE MZUNGU ENDELEA KU TRANSLATE MSG ZOTE NDO DAWA YAKE HUYO DADA
 
Back
Top Bottom