Mwungano wa Tanganyika na Zanzibar - Uhalisia Haukufikiriwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwungano wa Tanganyika na Zanzibar - Uhalisia Haukufikiriwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bams, May 30, 2012.

 1. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,581
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania inapita katika kipindi kigumu cha Mwungano. Mwungano huu, kwa muda mrefu umedumu kwa kushikiliwa kwa nguvu, na hasa Mwalimu Nyerere ambaye bila ya mashaka yeyote, alikuwa ni kiongozi mwenye nguvu, aliyeheshimiwa na kuogopwa Bara na Visiwani. Laiti kama kungekuwa na uhuru wakati wote wa uhai wa Mwungano wa watu kusema wanautaka mwungano au hawautaki, kuna uwezekano mkubwa mwungano huu usingekuwepo. Kadiri demokrasia inavyozidi kujengeka nchini na Duniani kote, hata kama tukavuka hapa tulipo, kuna uwezekano mkubwa Mwungano huu utakuja kufa tu. Hauwezi kudumu kwa sababu uhalisia haukuzingatiwa.

  Tofauti kubwa ya idadi ya watu na ukubwa wa nchi

  Hata katika maisha ya kibiashara, ukiwa na kampuni na unataka kampuni nyingine ya kuungana nayo, ni lazima utaitazama kampuni ambayo inakaribiana na yako, kwa kuangalia aina ya biashara anayofanya huyo unayetaka kuungana naye, mtaji wake na uwezo wake. Pale utakapoona mnakaribiana karibu kwa kila jambo ndipo mnaweza kuungana. Huwezi ukasema unaunganisha kampuni yenye mtaji wa U$10 billion na kampuni yenye mtaji wa U$10,000; uwezekano ambao ni rahisi ni kwa kampuni yenye mtaji wa U$10 billion kuinunua kampuni yenye mtaji wa U$1 million.

  Nimetoa mfano huu mdogo, si kwa nia ya kuidhalilisha Zanzibar bali ndiyo hali halisi katika maisha ya kila siku.
  Mwungano wa Tanganyika na Zanzibar haukustahili kuwepo. Ni vigumu sana kuungana, na mwungano ukaendelea kuwa na nguvu, unapokuwa na nchi kubwa kama Tanganyika yenye mamilioni ya watu, eneo kubwa (zaidi ya mara 100 ya Zanzibar), rasilimali mara 100 ya zile za Zanzibar bila kuwa na hisia toka Zanzibar kuwa wanapuuzwa, kuonewa au kudhihakiwa kwa vile tu wao ni wachache au nchi yao ni ndogo. Na pia kwa upande wa Bara, lazima zitakuwepo hisia kuwa ni kupoteza muda kutafuta maoni ya Zanzibar (yenye watu milioni 2) katika kila jambo kwa mambo yanayohusu maisha ya Wabara zaidi ya 40 milioni.

  Ni Kinyume cha Misingi ya Kibiashara na Uchumi

  Katika biashara tunasema kuwa hisa zako ndiyo nguvu yako katika kampuni. Kama mimi namiliki mtaji wa U$100 milioni katika kampuni basi nina nguvu katika kila jambo ikiwa ni pamoja na maamuzi mara 100 ya yule anayemiliki mtaji wa U$1 milioni. Haya mambo japo hayazungumzwi lakini ndiyo ukweli uliopo kila mahali. Hata kule Umoja wa Mataifa, nchi za Kiafrica zinapuuzwa kwa sababu mchango wao katika kuendesha mashirika ya kimataifa ni mdogo mno. Haitegemewi uchangie shilingi 100 halafu thamani yako katika kampuni iwe sawa na anayechangia shilingi bilioni 1. Mimi ninayechangia zaidi ni lazima niwe na maamuzi makubwa zaidi kwa sababu, kama kutakuwa na hasara mimi ndiye nitakayeathirika zaidi, wewe shilingi yako 100 hata ikipotea hakuna madhara makubwa. Gharama za Mwungano zinachangiwa kwa 96% na Tanganyika. Hakuna namna ambayo inaweza kuifanya Tanganyika iione Zanzibar kuwa ni 'Equal Partner'. Usawa wa Tanganyika na Zanzibar katika mwungano ni wa kisiasa na nadharia zaidi, na hauwezi kudumu wenyewe bila kusimamiwa na nguvu ya sheria na dola.

  Kutenganishwa na Bahari

  Wengine wanaweza wasione kama hili ni tatizo kubwa lakini kutengwa na kitu kikubwa kama bahari huleta fikra ya utofauti na yule uliyetengwa naye. Hali hii ipo hata kwa visiwa vya nchi moja inayotengenezwa na visiwa kadhaa, ndiyo maana katika maeneo mengi kumekuwepo na matatizo ya visiwa kutaka kujitenga kutoka visiwa vingine. Na wala sitashangaa Zanzibar ikijitenga na Tanganyika, tukasikia tena Unguja inajitenga na Pemba.

  Siku zote mwungano wa mwenye nguvu kubwa iwe ni kirasilimali au eneo na aliye mdogo sana kwa maana ya uchache wa rasilimali au udogo wa eneo, unakuwa ni mwungano wa Tahadhari kubwa. Mdogo kila mara hufikiria kuwa kutokana na udogo wake, anapuuzwa. Hata kama itakuwa ni kwa bahati mbaya hakushirikishwa ni lazima atadhania imefanywa makusudi kutokana na udogo wake. Na kwa mkubwa anaweza pia kuona kuwa kila mara kujadiliana na huyu mdogo ni kupoteza muda maana hana mchango wa kubadilisha jambo.

  Fikra zangu: Ili mwungano wa Tanganyika na Zanzibar udumu ni lazima ulindwe kwa nguvu za dola na udikteta wa kiwango fulani lakini kwa demokrasia ya 100% ni lazima ufe kama si leo basi ni kesho.
   
 2. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145

  Many questions are continuing to be raised regarding the legal basis of the Union:

  Whether the two Presidents on their own had the powers to sign such a Union Agreement; Why the Zanzibar's Attorney General, as the Principal Legal Advisor to the Government, was not consulted; Why there was no referendum; and whether in joining such a Union, Zanzibar was not in fact 'swallowed' and 'annexed' by Tanganyika. Discussions on the Union were conducted very secretively, why?
   
Loading...