MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako!

Ahsanteni kwa kutoa muongozo wa kutoa Matangazo ya Biashara.

Mimi nikiona Tangazo halijajitosheleza huwa nalikosoa hapo hapo, hasa mtu hataji sehemu alipo, inakera sana.
Mimi pia naonaga sawa na demu kavaa dera hana msambwanda na leo nimpasha jamaa na nyumba yake ya Kihonda naona jamiiforums wameliona hilo.
 
T
Ndugu wadau wa Jukwaa la Matangazo Madogo,

Tunafarijika kuona mnaendelea kutumia vizuri jukwaa hili katika kufanya biashara.

Hata hivyo, kuna changamoto kwa baadhi ya wenzetu kushindwa kuzingatia vigezo vya kuweka matangazo yao hivyo kupelekea matangazo yao kuondolewa hewani.

Vigezo vya msingi unavyopaswa kuzingatia kabla hujaweka tangazo;
  1. Elezea huduma/bidhaa unayouza kwa maelezo machache yanayojitosheleza
  2. Kama ni bidhaa, elezea hali yake (mpya au imetumika muda gani) huku ukiambatanisha na picha yake halisi.
  3. Taja bei
  4. Taja mahali huduma/bidhaa hiyo inapopatikana pamoja na mawasiliano yako.(Usiwaambie watu wakufuate PM kwa Mawasiliano. Weka namba ya simu)
  5. Weka taarifa mpya kuhusu bidhaa hiyo kwenye uzi husika, usianzishe uzi mpya.
  6. Usiweke tangazo moja mara nyingi.
Ni vyema kuzingatia hatua hizo chache. Kinyume na hapo, tangazo lako litaondolewa hewani.

Kuna baadhi ya matangazo hayaruhusiwi kabisa JamiiForums. Mfano matangazo ya kurasa za Blogs, Facebook, Instagram, Twitter au mtandao wowote yataondolewa mara moja.

NB: Matangazo yote yakae Jukwaa la Matangazo.

Karibuni kwa maswali na ufafanuzi zaidi..
1.Tangazo moja linaweza kuchukua mudagani kurudiwa hasa kama halikusomwa?
2.Nini maana ya PM (yaani waskufuate PM)
 
Nimepost tangazo leo halija tokea kwenye ukurasa wa Marangazo madogo madogo..

Na halija kiuka sheria yoyote.. Kuna nini??
 
Vizuri. Mmekuwa mkiruhusu matangazo yenye vigezo vya chini. Napendekeza wakati wa kujaza tangazo muweke sehemu za kujaza ili mtu asipojaza maeneo hayo isi postiwe. Nyie mnabaki na ku approve au kuruzuia. Nyie wa IT mtaelewa zaidi
 
Naweza kuweka tangazo la Haina gani !!?
Na ni matangazo ya Haina gani huwa yanafutwa mara kwa mara .. na sababu ni Nini .. please mwenye uelewa wa hii jamii forum vzr naomba anisaidie
 
Ndugu wadau wa Jukwaa la Matangazo Madogo,

Tunafarijika kuona mnaendelea kutumia vizuri jukwaa hili katika kufanya biashara.

Hata hivyo, kuna changamoto kwa baadhi ya wenzetu kushindwa kuzingatia vigezo vya kuweka matangazo yao hivyo kupelekea matangazo yao kuondolewa hewani.

Vigezo vya msingi unavyopaswa kuzingatia kabla hujaweka tangazo;
  1. Elezea huduma/bidhaa unayouza kwa maelezo machache yanayojitosheleza
  2. Kama ni bidhaa, elezea hali yake (mpya au imetumika muda gani) huku ukiambatanisha na picha yake halisi.
  3. Taja bei
  4. Taja mahali huduma/bidhaa hiyo inapopatikana pamoja na mawasiliano yako.(Usiwaambie watu wakufuate PM kwa Mawasiliano. Weka namba ya simu)
  5. Weka taarifa mpya kuhusu bidhaa hiyo kwenye uzi husika, usianzishe uzi mpya.
  6. Usiweke tangazo moja mara nyingi.
Ni vyema kuzingatia hatua hizo chache. Kinyume na hapo, tangazo lako litaondolewa hewani.

Kuna baadhi ya matangazo hayaruhusiwi kabisa JamiiForums. Mfano matangazo ya kurasa za Blogs, madawa, vipodozi, Tiba, Facebook, Instagram, Twitter au mtandao wowote yataondolewa mara moja.

Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili

NB: Matangazo yote yakae Jukwaa la Matangazo.

Karibuni kwa maswali na ufafanuzi zaidi..
Nimeweka tangazo langu na mkalifuta. Tena nimeweka Hadi picha ila mmenionea, sijui kwa nini?
 
Back
Top Bottom