MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako!

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,984
Ndugu wadau wa Jukwaa la Matangazo Madogo,

Tunafarijika kuona mnaendelea kutumia vizuri jukwaa hili katika kufanya biashara.

Hata hivyo, kuna changamoto kwa baadhi ya wenzetu kushindwa kuzingatia vigezo vya kuweka matangazo yao hivyo kupelekea matangazo yao kuondolewa hewani.

Vigezo vya msingi unavyopaswa kuzingatia kabla hujaweka tangazo;
  1. Elezea huduma/bidhaa unayouza kwa maelezo machache yanayojitosheleza
  2. Kama ni bidhaa, elezea hali yake (mpya au imetumika muda gani) huku ukiambatanisha na picha yake halisi.
  3. Taja bei
  4. Taja mahali huduma/bidhaa hiyo inapopatikana pamoja na mawasiliano yako.(Usiwaambie watu wakufuate PM kwa Mawasiliano. Weka namba ya simu)
  5. Weka taarifa mpya kuhusu bidhaa hiyo kwenye uzi husika, usianzishe uzi mpya.
  6. Usiweke tangazo moja mara nyingi.
Ni vyema kuzingatia hatua hizo chache. Kinyume na hapo, tangazo lako litaondolewa hewani.

Kuna baadhi ya matangazo hayaruhusiwi kabisa JamiiForums. Mfano matangazo ya kurasa za Blogs, Facebook, Instagram, Twitter, au mtandao wowote yataondolewa mara moja. Pia haturuhusu matangazo ya madawa ya asili, vipodozi, Tiba ya asili nk.

Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili

NB: Matangazo yote yakae Jukwaa la Matangazo.

Karibuni kwa maswali na ufafanuzi zaidi..
 
Sababu zilizo tumika na serikali kumfungia Dr.Mwaka ofisi yake ya dawa za asili ndiyo sababu hiyo hiyo inayo tumiwa na Jf kuondoa mabandiko yote yenye mrengo huo.....
hakuna waraka wwote uliotolewa na serikal wa kuzuia matangazo ya dawaasilia zile zilikua ni chuki tu je na nyie mna mrengo huo
 
kwa nn matangazo ya dawa asilia mmnayafuta


Mkuu Jenseny, umefanya vizuri sana kuuliza. Kupitia swali lako, wengi zaidi watafahamu sababu za nyuzi za aina hiyo kuondolewa.

Matangazo ya dawa asilia tunayondoa kwa sababu Serikali kupitia Wizara ya Afya ilipiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba/dawa kwa kuwa ni kinyume na miiko ya taaluma hiyo.

Taarifa hiyo iliwekwa hapa >> Serikali yapiga marufuku matangazo ya tiba za asili

Asante.
 
Naashukuru Mmmeliona hilo, Ila muwaambie TANESCO hilo Tangazo lao linatuvuruga sana especialy picha ya huyo mdada watafute mtu mwengne.
Tanesco.PNG
 
Ni sahihi kabisa. Kinyume na hapo tangazo litaondolewa na huenda likaondolewa pasipo taarifa..
Ahsanteni kwa kutoa muongozo wa kutoa Matangazo ya Biashara.

Mimi nikiona Tangazo halijajitosheleza huwa nalikosoa hapo hapo, hasa mtu hataji sehemu alipo, inakera sana.
 
Swali langu kuna akaunti ya jamaa microsafi imefungiwa kwasababu ya hot link ya matangazo, je lipoje ili nimfikishie

pia huo uzi wa zamani unaupataje, kwani unakuta umepost wiki imepita

Naomba ufafnuzi wa hili "You have been banned for the following reason: We do not allow Spamming and Hotlinking[OFA YA MWEZI: Jipatie Website kwa Bei Nafuu!!!" hiyo ni akaunti ya jama microsafi imefungwa
 
Taja mahali huduma/bidhaa hiyo inapopatikana pamoja na mawasiliano yako.

Shukrani sana Modi.

Kuweka Tangazo na kumalizia kwa ujumbe "Nifuate PM", si sahihi hata kidogo.

Kwanini nikufuate PM na usielezee kwa ubayana sote tufahamu?. Unaficha nini haswa?. Nadhani huku ndiko chanzo cha kuibiana na kutapeliana.

Pia muwe na desturi ya kujibu malalamiko ya wanabodi kwa muda sahihi (kama uwezekano upo). Kama uwezekano upo, basi muanzishe uzi maalum wa Maswali, ushauri na malalamiko kwa Jamii Forums.

Live Long Jamii Forums.
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom