Mwongozo wa ufugaji wa kuku wa nyama (Broiler)

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,750
15,641
HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba

Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.

Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.

Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.

Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.

Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba

Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.

Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.

Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.

Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

JOTO

Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.

Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).

Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

RATIBA MWANGA
AGE(DAYS) .......................HOURS(DARK)
0-7 ---------------------------------------------------->0
8-21---------------------------------------------------->9
22 ------------------------------------------------------->8
23 ------------------------------------------------------->7
24 ------------------------------------------------------->6
5 Days before Slaughter/Sale ------------>5
4 Days before Slaughter/Sale-----------> 4
3 Days before Slaughter/Sale ------------>3
2 Days before Slaughter/Sale ------------>2
1 Days before Slaughter/Sale ------------>1

Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35

MAJI

Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida)

Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

CHAKULA

Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders. Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).

Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.

Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

· Chick starter

Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

· Grower
Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

· Finisher
Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza.

BROILER TIPS

SIKU 1-5

Wape glucose na mchanganyo mmoja wapo kati yah ii ifuatayo;
· Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
· Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

CHAKULA
· Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

SIKU YA 6
· Vitamini (vitastress)

SIKU YA 7
· Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

WIKI YA PILI
· Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

WIKI YA TATU

· Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

WIKI YA NNE
· Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

WIKI YA TANO
· Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

WIKI YA SITA
· Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni
· Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo
 
Nimekuelewa boss iko vizur sana, vp sasa kuhusu ratio ya kuchanganya chakula labda minerals, vitamin etc inakuwa vp
 
Mkuu inamaana kulea kifaranga cha broilers ni sawa na layers na kama ni tofauti, utofauti wake ukoje?
 
HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)
Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba

· Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.
· Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.
· Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.
· Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.
· Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba

· Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.
· Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.
· Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.
· Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

JOTO

· Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.
· Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).
· Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

RATIBA MWANGA
AGE(DAYS) .......................HOURS(DARK)
0-7 ---------------------------------------------------->0
8-21---------------------------------------------------->9
22 ------------------------------------------------------->8
23 ------------------------------------------------------->7
24 ------------------------------------------------------->6
5 Days before Slaughter/Sale ------------>5
4 Days before Slaughter/Sale-----------> 4
3 Days before Slaughter/Sale ------------>3
2 Days before Slaughter/Sale ------------>2
1 Days before Slaughter/Sale ------------>1

Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35

MAJI

· Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida)

· Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

CHAKULA

· Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders. Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).
· Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.
· Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

· Chick starter
Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

· Grower
Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

· Finisher
Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza.

BROILER TIPS

SIKU 1-5
Wape glucose na mchanganyo mmoja wapo kati yah ii ifuatayo;
· Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
· Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

CHAKULA
· Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

SIKU YA 6
· Vitamini (vitastress)

SIKU YA 7
· Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

WIKI YA PILI
· Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

WIKI YA TATU
· Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

WIKI YA NNE
· Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

WIKI YA TANO
· Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

WIKI YA SITA
· Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni
· Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo
Unapatikana wapi mkuu
 
Mkuu nakupa hongera kwa nondo ulizotoa. Lakini kuhusiana na Lighting Programme kwa wafugaji wachanga nadhani ni mapema kuipractise hususani ukiangalia broiler wengi hutoka ndani ya majuma manne, kufanya lighting programme na kuwaweka vifaranga 5-9hours of dark ni kutowapa access ya feed and water which will impact their growth rate. Minimum hours of darkness i recommend ni 3hrs tena hii ikiwa kati ya juma la pili kwenda la tatu. Lakini mfugaji lazima azingatie vitu vingine kama idadi ya vyombo vya chakula na maji, stocking density, na upatikanaji wa umeme pindi unapohitajika vinginevyo i don't recommend lighting programme kwa wafugaji wadogo.
 
Machine ya kuondoa manyoya
Nicontact hapa kama unahitaji
 
Attachments

  • IMG_2767.JPG
    IMG_2767.JPG
    41.1 KB · Views: 213
  • IMG_2768.JPG
    IMG_2768.JPG
    33.3 KB · Views: 239

Similar Discussions

Back
Top Bottom