Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Nyumba za ibada zikaguliwe mara kwa mara na kuhakikisha zinazingatia yafuatayo;
- Ziweke vifaa vya kunawia mikono (maji safi tiririka na sabuni au Vitakasa mikonoSanitizers) na muumini atakaye simamia unawaji kwa wote.
- Waumini wavae Barakoa
- Waumini wakae umbali unaozidi mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine pande zote.
- Taratibu za kufanya usafi na utakasaji wa viti, meza na maeneo wanapokaa kabla na baada ya ibada ufanyike.
- Alama katika viti ziwekwe kuonyesha umbali wa mita moja.
- Wazee, Watoto na wale wote wenye matatizo ya kiafya yanayotambulika (Mfano. Kisukari, Shinikizo la Damu, Kansa n.k), wanashauriwa kujiepusha na ibada zenye mikusanyiko ya Watu wengi na wachukue tahadhari zote muda wote
- Kama nyumba ya ibada ni ndogo uanzishwe utaratibu wa kusalia nje/maeneo ya wazi au kuongeza idadi ya vipindi vya ibada na kuruhusu idadi ya watu wachache kuingia ibadani na kuzingatia uvaaji wa Barakoa.
- Ibada ziwe za muda mfupi usiozidi masaa mawili.
- Huduma zinazohusisha kugusana ziepukwe
- Kuwepo na ujumbe wa mara kwa mara kwa ajili ya kuwakumbusha waumini kuhusu namna ya kujikinga na UVIKO-19 na namba za kuwasiliana na huduma za afya iwapo atapatikana mgonjwa.