Mwongozo wa kutibu mfumo wa upumuaji unaadaliwa. Je, ni ugonjwa gani?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwa mujibu wa chama cha madaktari nchini MAT kimeandaa jopo la madaktari bingwa ili kutoa mwongozo namna wagonjwa wanaoumwa mfumo wa kupumua wapate tiba ya namna gani.

Kwa mujibu wa Dk Mwaibambe ni kuwa mwongozo huo utaelekeza ni dawa zipi ambazo mgojwa aliyeathirka mfumo wa kupumua anatakiwa apewe,sababu mpaka sasa madaktari wanajitolea dawa bila kuwa mwongozo hivyo kila daktari kujitibia anavyoamua.

Mwongozo huo utakuwa tayari ifikapo kesho na utaandaliwa na madaktali bingwa wa mfumo wa upumuaji.

Lakini swali la msingi ambalo tunatakiwa kujiuliza. Je, huo ugonjwa unaothiri mfumo wa kupumua ni upi?
 
Nchi nyingine haya yalifanyika tangu mwaka jana April. Kadiri madaktari walivyokuwa wanapata uzoefu kwenye kuutibu huu ugonjwa ndivyo walivykuwa wana-update mwongozo na mpaka sasa wameboresha matibabu kwa kiwango kikubwa. BTW Wasije wakaweka mwongozo wa dawa za kienyeji ambazo hazijafaniwa utafiti.

Hii nchi iko kwenye kipindi kibaya sana kiuongozi na lolote linaweza kutokea. Kingine hivi shirikisho la Africa Mashariki lina faida gani kama siyo kushirikiana kwenye mambo kama haya? Ilitakiwa Afrika Mashariki madaktari washirikiane kwenye kuandaa mwongoza wa matibabu kulingana na uzoefu na changamoto wanazokutana nazo.
 
Madaktari “hawajui” jina la ugonjwa lakini muongozo wa kutibu wanaujua!

Wimbi la pili lilipoibuka wananchi wangepewa taarifa mapema ili wale walio kwenye makundi hatarishi wangejilinda na maisha ya wengi tu yangeokolewa. RIP wote hao.
 
Madaktari “hawajui” jina la ugonjwa lakini muongozo wa kutibu wanaujua!
Wimbi lapili lilipoibuka wananchi wangepewa taarifa mapema ili wale waliokwenye makundi hatarishi wangejilinda na maisha mengi yangeokolewa. RIP wote hao.
INCHI kwa sasa inamuogopa mtu mmoja tu imrfika point watu wanakana hadi taaluma zao ili wateteee uongo wa mtu mmoja.
 
Nimeona mkurugenzi wa kinga amejizuia katakata kutaja barakoa kwenye kinywa chake kama kinga ya corona bali anasema watu wanawe mikono
 
Kwa mujibu wa chama cha madaktari nchini MAT kimeandaa jopo la madaktari bingwa ili kutoa mwongozo namna wagonjwa wanaoumwa mfumo wa kupumua wapate tiba ya namna gani...
Sasa jamani na nyie madaktari tena madaktari bingwa si mseme tu Covid 19.Mmeshakuwa wanasiasa sasa.Madaktari mlituambia kuwa ni nimonia,mkatuambia tena, sasa mnakuja na mfumo wa upumuaji.Covid 19 ni sawa na magonjwa mengine kama ebola nk.msiogope kutuambia ili tuchukue tahadhari.

Endeleeni kutoa elimu ya kutosha kama ilivyokuwa 2020.Acha kikombe kiwe kikombe na sio kikombe kiwe kibakuli.Maji tiririka,barakoa,distance,kutokushikana mikono,sala na maombi ya kina nk.

Kingine.Mabwana afya wahakikishe kila duka,mgahawa,sokoni,misikitini,makanisani,mahotelini,mashuleni,kwenye mabasi sehemu za kazi kila mahali nk.maji ya kunawa na sabuni na elimu visikosekani.Piga vita covid 19 itanyamaza kimyaaaaaaaaaaaa.
 
kama wanaogopa kutaja jina la ugonjwa basi hata huo muongozo wao ni feki siyo wa kuuamini. Bora tuendelee kupiga nyungu kwa kasi mpya!
 
kama wanaogopa kutaja jina la ugonjwa basi hata huo muongozo wao ni feki siyo wa kuuamini. Bora tuendelee kupiga nyungu kwa kasi mpya!
Huu upuuzi wa nyungu hapana
IMG_20210219_211227.jpg
 
Nimeona mkurugenzi wa kinga amejizuia katakata kutaja barakoa kwenye kinywa chake kama kinga ya corona bali anasema watu wanawe mikono
Hao Madaktari wamekubali kugeuzwa kuwa Waganga wa kienyeji bila shaka! Sasa ugonjwa wa kushindwa kupumua na kushauriwa kunawa mikono, wapi na wapi!

Si wanyooshe tu maelezo ya kwamba Corona imetamalaki mtaani ili mapambano dhidi ya huyo mdudu yapambe moto!!
 
Hao Madaktari wamekubali kugeuzwa kuwa Waganga wa kienyeji bila shaka! Sasa ugonjwa wa kushindwa kupumua na kushauriwa kunawa mikono, wapi na wapi!

Si wanyooshe tu maelezo ya kwamba Corona imetamalaki mtaani ili mapambano dhidi ya huyo mdudu yapambe moto!!
Woga ni kitu kibaya sana, viongozi wote waandamizi hakuna anayevaa barakoa wakiogopa kutumbuliwa.
 
Back
Top Bottom